Tanzania

Z Anto Asema Wasanii wa Zamani Hawajashindwa Kuendana na Mazingira ya Kisasa Kuimba Muziki

Amemtaja Bushoke kama miongoni mwa wasanii wa zamani waliomkosha walipokuwa wakiimba kwenye tamasha la Serengeti Music Festival

Mkali wa wa kitambo wa ngoma ya Binti Kiziwi, Z Anto amesema hafikirii kama wasanii wa zamani wameshindwa kuendana na mazingira ya kisasa ya kuimba na kufanya muziki.

Hatua hii imekuja baada ya kuzuka kwa maoni tofauti kuhusu namna wasanii wa zamani walivyoonyesha uwezo wao katika tamasha Serengeti Music Festival lililofanyika Dodoma.

Akizungumza na Serengeti Post, Z Anto amemtaja Bushoke kama miongoni mwa wasanii wa zamani waliomkosha walipokuwa wakiimba kwenye tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki hii.

"Ukiangalia orodha ya wasanii waliofanya show vizuri huenda wasanii wa zamani wakawa wengi kuliko wasanii wa sasa au wamebalance 50 kwa 50. Kwa mfano nimemuona mtu kama Bushoke, katika wasanii waliofanya performance mpaka mwenyewe nikasema ehee hi hatari Bushoke mmoja wapo," amesema Z Anto.

Katika hatua nyingine msanii huyo amesema kuwa kuna mambo mengi hutokea kwenye maonyesho wakati ambapo msanii anakua anaimba na kuna muda msanii anaweza akajikuta anafanya nje ya matarajio ya mashabiki hivyo ubunifu wa ziada huhitajika ili kuweza kuendana na mazingira ya mashabiki na kile wanachokihitaji.

Show yote msanii akili ya msanii inatakiwa ijue yani uwe umeshapanga vitu vinne hadi vitano katika akili yako kwamba show ikiwa hivi inabidi nifanye hivi show isipokuwa hivi ntafanya hivi kwahivyo mara nyingi huwa tunajiset kwa design hiyo” amesema Z.Anto

Kupitia Kurasa zake za mitandao ya kijamii msanii wa HipHop nchini, Roma Mkatoliki amekosoa na kusema kuwa baadhi ya wasanii wa zamani wameonyesha uwezo mdogo wa kuimba kwenye tamasha hilo na wengi wametoka nje ya kile ambacho mashabiki walikitegemea.

Roma amesema kuwa baadhi ya wasanii wa zamani wamesahau mashairi ya nyimbo zao na wanachokiimba jukwaani ni kawaida na hakuna ubunifu na kuwataka wasanii hao kubadilika kutokana na mahitaji wa soko la muzikii kwa sasa.

"Tukifika jukwaani tukamuee tuachane na mambo ya DJ zuia unaanza kutoa hotuba afu nyimbo ikipigwa unaanza mikono juu kelele za mikono juu zimekua nyingi kuliko ile delivering, mtu unashindwa kuimba unashindwa kurap haiko sawa," amesema Roma.

Tamasha la hilo lilioandaliwa na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo lilihudhuliwa na viongozi wa serikali akiwemo Waziri wa Wizara hiyo, Innocent Bashungwa pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye pia ni Msemaji wa serikali Dkt Hassan Abasi wengine ni wabunge Antony Mavunde, Patrobasi Katambi na Hamis Tale