
Kunyemelewa
na watani zao wa Jadi Klabu ya simba katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania
bara ndio mzimu unaoutesa Klabu ya Yanga kwa hivi sasa wakati ambapo baadhi ya
mashabiki wameonekana kuutupia lawama uongozi wa klabu hiyo kwa kutochukua
hatua za mapema kuzuia Janga hilo.
Matokeo ya sare katika mechi mbili mfululizo walizozipata
Yanga katika michezo yao ya Ligi Kuu Bara yamewaibua viongozi wa timu hiyo
ambao wamezitupia lawama mamlaka za soka nchini wakidai kuwa zinahusika moja
kwa moja na upatikanaji wa matokeo hayo
Akizungumzia shutma hizo katika mkutano na waandishi wa
habari, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela
amesema, kwa sasa timu yao haitendewi haki na mamlaka zote zinazosimamia soka,
kama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kamati
ya Waamuzi pamoja na Kamati ya saa 72.
Mwakalebela amelalamikia matukio yaliyojitokeza katika mchezo wa
Klabu hiyo dhidi ya Mbeya City na kudai kuwa walinyimwa penati mbili za wazi
ambazo walistaili kuzipata na zingepelekea wao kushinda mchezo huo na sio
kupata pointi moja.
Mwakalebela pia amelalamikia mchezo wa timu huyo dhidi ya
Kagera sugar akidai kuwa walinyimwa penati ambazo zingewafanya kupata pointi
tatu badala ya kupata moja, huku akidai kuwa mamlaka husika kuna timu
inayoandaliwa kuwa bingwa.
"Kama kuna bingwa kaandaliwa basi apewe kombe tujue moja,
tunatarajia kamati husika zitatoa maamuzi katika hizo mechi zetu mbili na hao
waamuzi wachukuliwe hatua stahiki tusitolewe kwenye mstari wetu wa kutwaa ubingwa
msimu huu," amesisitiza Mwakalebela.
Mwakalebela amesema, Yanga wametumia gharama kubwa kuiandaa timu
hiyo hivyo namna matukio yanayotokea na kufumbiwa macho na vyombo husika
yanawafanya kutafsiri vibaya juu yao.
Hatahivyo baadhi ya wafuatilizi wa masuala ya soka nchini
wanasema kuwa ni haki ya msingi kwa vilabu kuhoji ubora wa uendeshwaji wa ligi
kuu pale inapohitajika lakini lazima malalamiko hayo yawe na mantiki na
uhalisia. Gharib Mzinga mchambuzi wa masuala ya soka nchini anasema kuwa
mwamuzi kuchezesha chini ya kiwango ni suala ambalo hutokea katika mchezo na
waamuzi huadhibiwa kupitia kamati husika ya waamuzi
Kimsingi suala la performance ya waamuzi kuwa ndogo ni suala la
kitaifa hilo sote tunalifahamu, lakini isionekane tu ni upande mmoja wao ndio
wanaonewa peke yao hapana" amesema Mzinga.
Yanga ambao kwasasa ni vinara katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara wanatàrajiwa kuingia Dimbani leo kuzisaka pointi tatu nyingine dhidi ya klabu ya Mtibwa sugar kutoka Mkoani Mororgoro.
Leave a comment