Duniani

Uingereza kubalili sheria kuibana mitandao kukabiliana na ubaguzi wa rangi

Serikali ya Uingereza itabadilisha sheria kuhakikisha makampuni ya mitandao ya kijamii yanawajibika kukabiliana na ubaguzi wa rangi nchnini humo

Serikali nchini Uingereza imeungana na Chama cha Soka nchini humo (FA) kukemea na kupinga ubaguzi wa rangi dhidi ya wanamichezo. Imeripotiwa kwamba mchezaji wa klabu ya Manchester United Alex Tuanzebe pamoja na Lauren James walikumbana na ubaguzi wa rangi wikiendi iliyopita. Chama cha Soka nchini Uingereza kilitoa tamko kukemea vitendo vya ubaguzi na kuahidi kufanya kila linalowezekana kungo’oa mizizi ya ubaguzi katika soka. 

 

Pia, Chama cha Soka nchini Uingereza kilitoa wito kwa serikali ya nchi hiyo na makampuni ya mitandao ya kijamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na ubaguzi wa rangi unaofanywa kupitia mitandao.

 

Kufuatia tamko la Chama cha Soka nchini Uingereza, Waziri wa Digitali, Utamaduni, Habari, Vyombo vya Habari na Michezo , Oliver Dowden amechukua hatua kwa kuitisha mkutano na chama cha soka na wadau michezo na baadaye kutoa tamko kupitia ukurasa wake wa Twitter akisema kwamba amesikitishwa na mwendelezo wa matukio ya ubaguzi. 

 

Dowden amesema kwamba serikali ya Uingereza itabadilisha sheria kuhakikisha makampuni ya mitandao ya kijamii yanawajibika kukabiliana na ubaguzi wa rangi nchnini humo.

 

“Tunakwenda kubadili sheria kuhakikisha makampuni ya mitandao ya kijamii yanawajibika kwa kinachoendelea  katika mitandao hiyo. Makampuni hayo yanaweza kuanza kutimiza wajibu wao wa kujali wachezaji hata kuanzia leo kwa kuondoa maudhui ya kibaguzi katika mitandao. Wachezaji hawapaswi kunyanyaswa kwa kufanya kazi yao, ubaguzi wa rangi sasa basi,” amesema Dowden. 

 

Akizungumzia tukio la unyanyasaji uliotokea kwa beki wa Manchester United, Tuanzebe, msemaji wa mtamndao wa Facebook ambao pia ni wamiliki wa Instagram na WhatsApp amesema kwamba Instagram hawaruhusu ubaguzi wa rangi na tayari walishachukua hatua kukabiliana na changamoto aliyokumbana nayo Tuanzebe. 

 

“Instagram haturuhusu ubaguzi wa rangi na tayari tumechukua hatua kwa kuondoa kurasa na maudhui yaliyolenga kumnyanyapaa Tuanzebe. Pia, tunaendelea kuibua mbinu mpya ya kukabiliana na ubaguzi unaofanyika kupitia mitandao.

 

Alex Tuanzebe alishambuliwa na maneno ya ubaguzi wa rangi mtandaoni baada ya timu yake kutoa sare na Evarton. Mbali na kuwa taifa lililoendelea kimichezo na kiustaarabu, bado Uingereza imeendelea kukumbwa na ubaguzi wa rangi.

 

Unafiki nini kifanyie kukabiliana na changamoto hii? 

 

 

Chanzo: Sky Sport News