Habari

Tanzania yahusishwa katika mzozo wa majini kati ya Somalia na Kenya katika Mahakama ya Kimataifa ya ICJ

Mawakili wanaowakilisha Somalia walisema makubaliano ya mipaka ya baharini ya Kenya na Tanzania ya mwaka 2009 yalitiwa saini wakati Kenya ikijua wazi kwamba Somalia inadai nafasi yake baharini. Athari za makubaliano ni kwamba walipunguza haki ya umiliki wa mpaka wa bahari upande wa Kenya, Mahakama ilielezwa

Nchi ya Somalia siku ya Jumanne iliiambia Mahakama ya Umoja wa Mataifa kwamba suala la Kenya kumiliki eneo lenye ukumbwa wa kilomita za mraba 160,000 katika bahari Hindi lilitokea baada ya Kenya kutia saini makubaliano na Tanzania mnamo Julai 2009 ambayo yalipelekea nchi ya Tanzania kupata sehemu kubwa zaidi baharini hivyo wao kusogea kumega sehemu ya Somalia.


Mahakama ilisema kwamba makubaliano ya mpaka kati ya Kenya na Tanzania yaliiiponza Kenya kwani sehemu ya umiliki wake ilipunguzwa.

Mawakili wa Somalia walisema makubaliano ya mipaka ya baharini ya Kenya na Tanzania ya mwaka 2009 yalitiwa saini wakati Kenya ikijua wazi kwamba Somalia inadai nafasi yake baharini. Athari za makubaliano ni kwamba walipunguza haki ya umiliki wa mpaka wa bahari upande wa Kenya, Mahakama ilielezwa.

“Kenya ilijiponza yenyewe ilipofanya makubaliano na Tanzania. Kwa hiari yake ilipoteza haki zake.

Iliamua kuipa Tanzania kilomita za mraba 25,000 za nafasi yake ya baharini. Kenya haina haki ya kuifanya Somalia ilipe kile ilichofanya na Tanzania kwa kurekebisha mipaka,”wakili hao walisema.

Wakati wa siku ya pili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo bila uwepo wa Kenya, Mahakama iliambiwa kwamba Kenya ilikuwa imesema kuwa katika makubaliano hayo ilikuwa inalinda maslahi yake na usalama ambapo walijibiwa na mawakili kuwa itakuwa hatari kuibiana mipaka kati ya nchi kwa kigezo tu cha nchi gani ina nguvu, wakisisitiza kuwa Somalia ina haki sawa katika mipaka.


Waliongeza kuwa hata ikitokea Kenya ikaumia ikitokea Somali wakapewa eneo la baharini linalogombaniwa basi hakutokuwa na upendeleo.

Mawakili hao pia waliambia mahakama kwamba Kenya katika hoja zake ilitaka mahakama itumie mkondo wa mstari wa usawa nba umbo la pembe tatu kutoka wakati ambapo nchi hizo mbili zilikutana eneo la pwani katika kuamua mzozo huku Somalia ikisema mpaka wa majini unastahili kufuata mpaka ya ardhini. Walakini, mbinu hiyo haijazoeleka na haitumiki katika masuala ya mipaka. Mawakili hao walisema mbinu hiyo haijawahi kutumiwa na mahakama yoyote na ICJ itakuwa ya kwanza kufanya hivyo.

Wakati wanaelezea Somalia kama nchi ya dhaifu na moja ya nchi masikini zaidi ulimwenguni kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mawakili waliiomba mahakama kuzingatia haki za nchi hiyo kulingana na jambo hilo na kutambua ukiukaji wa haki zake unaofanywa na nchi ya Kenya.

Pia mawakili hao walitaka mahakama iamuru Kenya iache kukiuka haki za kujitawala za Somalia.

"Somalia inataka kutetewa kwa haki zake. Rasilimali ni muhimu kwa maendeleo yake na mustakabali wa watu wake. Somalia ilifika mahakamani kwa ajili ya kulinda haki zake,” wakili hao walisema kwa wanapomaliza kuwasilisha madai yao.

Rais wa mahakama alisema ICJ imepokea barua kutoka Kenya ikijibu madai ya Somalia. Barua hizo zinahusu kutoshiriki kwa Kenya katika vikao.

Jaji alisema barua imepokelewa na mahakama itazungumza baadae.

Chanzo: Afro News