Habari

#Tanzania: Serikali Imekamilisha Malipo ya Ununuzi wa Ndege Mpya Tatu

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amepongeza shirika la Ndege la ATCL kwa kuanzisha safari za kwenda nje ya nchi Guangzhou China, akisema kuwa safari hizo ni chachu ya kuimarisha biashara, utalii na ajira.

Akitoa hoja bungeni juu ya makadirio na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa ndege hizo zinatarajiwa kuwasili katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 na hivyo kuwezesha serikali kuwa na ndege zake 12.

Waziri Mkuu Majaliwa amepongeza shirika la Ndege la ATCL kwa kuanzisha safari za kwenda nje ya nchi Guangzhou China, akisema kuwa safari hizo ni chachu ya kuimarisha biashara, utalii na ajira.

Kauli hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania, Charles Kicheere kutoa ripoti iliyowebainisha kuwa Shirika hilo la ndege limeingiza hasara ya takribani Shilingi Bilioni 150 kwa miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa CAG, kwa mwaka mmoja uliopita, ATCL imeingiza hasara ya Shilingi bilioni 60.