Habari

Tanzania Miongoni mwa Nchi 10 Zilizowekewa Vikwazo vya Usafiri kwa Muda Oman

Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa usiku wa Alhamisi wiki hii na itadumu kwa siku 15 ikiwa ni uamuzi wa hivi karibuni uliopitishwa na Kamati Kuu ya kushughulikia janga la corona.

Serikali ya Oman imetoa orodha ya nchi 10 ambazo zimezuliwa kuingia nchini humo chini ya uamuzi wa hivi karibuni uliopitishwa na Kamati Kuu ya kushughulikia janga la corona.

Nchi zilizopigwa marufuku ni Tanzania, Afrika Kusini, Lebanon, Sudan, Brazil, Nigeria, Guinea, Ghana, Sierra Leone, na Ethiopia.

Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa usiku wa Alhamisi wiki hii na itadumu kwa siku 15

Hatua hiyo imetokana na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya udhitibi wa corona nchini humo.

Marufuku hiyo pia inawahusisha watu watakaopita katika nchi hizo ndani ya siku 14 kabla ya kuingia Oman ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda raia wao dhidi ya corona.

Februari 15, Waziri wa Afya wa Oman alisema nchi yake inafikiria kuzuia safari za ndege kutoka kutoka nchi zinazoonesha kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona ikiwa ni baada ya   kuthibitisha takwimu za maambukizi ya Corona kwa wasafiri wanaotokea nchini Tanzania kuwa katika kiwango cha juu sana, ambapo asilimia 18 ya wasafiri walikutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Oman, mkutano wa kamati hiyo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman Hammoud bin Faisal Al Busaid.