Habari

Somalia: Al-Shabab Washambulia Kambi za Kijeshi

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba wanajeshi kutoka kambi mbalimbali walienda kutoa msaada katika kambizilizoathiriwa na kufanikiwa kuwaua wanamgambo kadhaa wa kikundi cha Al-Shabab


Mashambulio hayo yametokea mapema asubuhi ya leo yakilenga kambi za jeshi katika miji ya Barire na Awdhegle kusini mwa Somalia. Mashambulio yalianza na mabomu ya gari ya kujitoa muhanga katika vituo vyote viwili, likifuatiwa na shambulio la kambi za wanajeshi.

Afisa wa jeshi, Hussein Nur alinukuliwa akisema “jeshi lilipoteza askari kadhaa katika shambulio hilo la vituo vya Bariire na Awdhigle.” bila kutoa nambari sahihi ya vifo vya askari

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba wanajeshi kutoka kambi mbalimbali walienda kutoa msaada katika kambizilizoathiriwa na kufanikiwa kuwaua wanamgambo kadhaa wa kikundi cha Al-Shabab ambacho kilitekeleza shambulio hilo.

Baada ya mapigano hayo Jeshi sasa linadhibiti vituo vyote viwili na maeneo ya karibu huku likianzisha msako maalumu. "Tunawafuata wanamgambo katika msitu unaozunguka." Afisa Hussein Nur Alisema

Kundi la kigaidi la Al-Shabab limekuwa likianzisha mashambulio kwa miaka kadhaa nchini Somalia wakitaka nchi iongozwe kwa misingi ya kidini.