Habari

Udhibiti wa Makosa Mtandaoni, Silaha na Risasi zilizotiwa Mbaroni Mwaka 2020

Makosa ya 4850 ya Uhalifu mitandaoni yaripotiwa, watuhumiwa 634 wakamatwa kwa makosa hayo na baadhi wametenda uhalifu huo zaidi ya mara moja

Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha za aina mbalimbali jumla yake ikiwa ni silaha 199 na risasi 360, ikiwa ni pamoja na AK47 10, Pistol 16, Shortgun 39 na magobore 134.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Msemaji wa Jeshi la Polisi ASCP David Misime amesema kuwa jumla ya  watuhumiwa 177 Kati ya watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na wanaume 170 na wanawake 7.  Ambapo wamekamatwa wakitumia silaha hizo katika matukio mbalimbali ikiwemo ya unyan’ganyi wa kutumia silaha, mauaji, uwindaji haramu, ujangili na kumiliki silaha kinyume na sheria.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo la polisi limefanikiwa kukamata Madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na bhangi ni kilo 13,230.22 mirungi kilo 11,804.864 cocaine kilo 4.52 heroine kilo 70.5 ambapo  watuhumiwa  waliokamatwa  na  madawa hayo ya kulevya ni 9,265, kati yao wanaume walikuwa 8,514 na wanawake 751.

 

Pia Jeshi hilo limekamata pombe haramu ya moshi (gongo lita 69,295.30,  pamoja na mitambo 379 ya kutengenezea pombe hiyo ambapo, jumla ya watuhumiwa 7169 walikamatwa ambapo wanaume 4647 na wanawake ni 2522.

Kwa upande wa uhalifu kupitia mitandao ya simu kwa 2020 makosa yaliyoripotiwa ni 4850 watuhumiwa waliokamatwa ni 634 ambapo wanaume ni 490 na wanawake ni 144. Watuhumiwa waliokamatwa baadhi wamekutwa wametenda uhalifu huo zaidi ya mara moja

Kesi zilizopata mafanikio mahakamani 2020 kwa maana ya watuhumiwa kupatikana na hatia na kupewa adhabu ni 4499.

Jeshi la Polisi limesema kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa wananchi ambapo wameonekana kuwa na muamko mkubwa  katika  kubaini, kuzuia na kutoa taarifa za kiuhalifu.