
Serikali
imetangaza tahasusi (Combination) mpya kwa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2020 na Kozi za Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka
2021 lengo likiwa ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini ambayo
imekuwepo kwa muda mrefu.
Akizunguza
jijini Dodoma leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jafo amesema zoezi
hili litafanyika kuanzia tarehe 29/03/2021 hadi tarehe 11/04/2021 saa sita
usiku. Hivyo, wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko wanatakiwa kuingia kwenye
mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi unaopatikana katika anuani ya selform tamisemi.
Tahasusi
mpya zilizoanzishwa kwa wanafunzi wa kidato cha 5, mwaka 2021 ni kama
ifuatavyo:-
1.
Physics, Mathematics, Computer studies (PMC) watasoma shule ya sekondari Dodoma
ni wasichana na Shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ni wavulana.
2. Kiswahili, French, Chinese (KFC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana
na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.
3. Kiswahili, English, Chinese (KEC) watasoma sekondari ya Morogoro ni
wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.
4. Physical Education, Biology, Fine Arts (PEBFA) watasoma wasichana shule ya
sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya
sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya
PEBFA!
5. Physical Education, Geography, Economics (PEGE) watasoma wasichana shule ya
sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya
sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PEGE!
Aidha,
Waziri Jafo ameomba wanafunzi waanze kuchagua kuanzia leo hadi Aprili 11, 2021 saa 6 usiku siku ambayo mfumo
utafungwa.
Leave a comment