Habari

Samia: Fungulieni Vyombo Vya Habari Vilivyofungiwa

Rais ametoa maagizo hayo leo tarehe 06/04/2021 Ikulu Dar es salaam, alipokuwa akiwaapisha Watendaji wa Wizara mbalimbali wakiwamo Makatibu Wakuu, Manaibu pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali.

Rais Samia suluhu ameiagiza Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni pamoja na Wizara ya Teknolojia na Mawasiliano kuvifungulia na kuviondolea adhabu vyombo vyote vya Habari vilivyofungiwa kwa makosa mbalimbali.

Rais ametoa maagizo hayo leo tarehe 06/04/2021 Ikulu Dar es salaam, alipokuwa akiwaapisha Watendaji wa Wizara mbalimbali wakiwamo Makatibu Wakuu, Manaibu pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali.

Katika hotuba yake Rais amesema “wizara ya Habari nasikia kuna vyombo vya Habari mmevifungia, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya serikali, tusiwape Uhuru wa kusema tunabinya vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe.” Samia Suluhu Hassan

Wananchi wamedai kuwa maagizo hayo yanaleta sura mpya ya uhuru wa vyombo vya habari ambao ulilalamikiwa kubanwa sana kipindi cha mtangulizi wake, Hayati. John Pombe Magufuli.

Aidha, katika mitandao ya jamii, watu wamepongeza hatua hiyo huku wakija na ombi la kutaka kurekebisha sheria za vyombo vya habari ambazo zilitungwa na zimekuwa kandamizi kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Asante @SuluhuSamia kufungulia vyombo vya habari