
Kyenge aliteuliwa na Rais
Felix Tshisekedi Jumatatu ya Januari 15 ikiwa ni zaidi ya wiki mbili tangu Waziri Mkuu wa zamani
Sylvestre Ilunga ajiuzulu kufuatia kura ya kutokuwa na imani naye kufanyika
bungeni mwishoni mwa Januari.
Baada ya uteuzi huo Sama
Lukonde aliwaambia waandishi habari kwamba kurejesha hali ya usalama ndiyo
kitakuwa mmoja ya vipaumbele vyake vya juu, hasa katika eneo la mashariki na
Katanga, eneo la uchimbaji madini anakotokea.
"Usalama, kama
munavyojua, ni moja ya vipaumbele, haswa mashariki mwa Kongo na huko Katanga.
Pamoja na maswala ya usalama, tuna pia maswala ya kijamii, ile ya maendeleo,
maswala ya kisheria na pia swala la elimu kwa wote. Tuligusia mengi kuhusu
mageuzi kwani yanahitajika katika sekta kadhaa," alisema Lukonde.
Ilunga, mshirika wa Rais wa
zamani Joseph Kabila, alikuwa mkuu wa serikali ya muungano. Kujiuzulu kwake
kulifuata uamuzi wa Tshisekedi kumaliza makubaliano ya kugawana madaraka na
wafuasi wa Kabila baada ya mvutano wa miezi kadhaa kati ya kambi hizo mbili.
Naibu waziri wa zamani wa
vijana na michezo, Kyenge, 43, hivi karibuni aliwahi kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya taifa ya madini ya Gecamanine Juni 2019.Mwaka jana,
bunge la chini lilimpigia kura ya kumuondoa aliyekuwa spika Jeanine Mabunda, mfuasi
mwingine wa Kabila.
Tshisekedi aliingia madarakani mnamo Januari 2019 na kutia saini makubaliano ya siri ya muungano na Kabila, ambaye aliwaweka wafuasi wake wengi bungeni katika nchi hiyo ya Afrika ya kati.
Leave a comment