Habari

Rais Samia Ziarani Uganda

Rais Samia atakutana na kufanya mazungumzo na Rais Museveni na baadaye Marais hao wawili watasaini mkataba wa ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania

Rais Samia anatarajiria kukukutana na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni hapo kesho April 11, 2021 nchini Uganda.

Taarifa iliyothibitishwa na Wizara ya mambo ya Nje ya Uganda imesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kufanya ziara nchini humo ikiwa na malengo ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Aidha Akiwa nchini Uganda Rais Samia atakutana na kufanya mazungumzo na Rais Museveni na baadaye Marais hao wawili watasaini mkataba wa ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania.

Mkataba huo ambao uliopangwa kusainiwa katikati ya mwezi Machi uliahirishwa na kusogezwa mbele kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli.