Habari

Rais Mstaafu Ammwagia Sifa Samia, Awataka Wananchi Kumuunga Mkono

Mama ameanza vizuri, ingekuwa ni nyimbo ningesema once more

Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amemtembelea Rais Samia Suluhu Hassan katika makazi yake ya Ikulu ya Dar es Salaam. Mwinyi amemtembelea Samia mnamo Aprili 12, 2021 na kufanya naye mazungumzo, baada ya mazungumzo Mwinyi amempongeza Rais Samia kwa kuanza vyema majukumu yake na kuwataka wananchi kumuunga mkono. 


“Mama ameanza vizuri, ingekuwa ni nyimbo ningesema once more, ameanza vizuri kabisa na kila mmoja ana furaha, kila raia unayemsikia anasema Mama ameanza vizuri. Tuliyekuwa naye tulikuwa na Rais mzuri sana, mzoefu wa mambo ya kiserikali," alinukuliwa Rais Ali Hassan Mwinyi. 


Mwinyi amewataka watanzania wote kwa umoja wao kumuunga mkono Rais Samia.