
Tukio
hilo lina kuja siku nne baada ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) kufanikiwa
kuwezesha kutua salama kwa chombo chake cha Perseverance rover katika kreta karibu na ikweta ya sayari hiyo.
"Picha hizi ni matokeo ya ndoto zetu," Al Chen, Kiongozi aliyeongoza kutua kwa chombo hicho alisema.
Now that you’ve seen Mars, hear it. Grab some headphones and listen to the first sounds captured by one of my microphones. 🎧https://t.co/JswvAWC2IP#CountdownToMars
— NASA's Perseverance Mars Rover (@NASAPersevere) February 22, 2021
Picha
kutoka kwa kamera zenye kiwango cha juu zilianza kuchukua maili saba kutoka juu
ya uso wa Mars, ikionyesha kuyumba kwa nguvu kwa parachute ikifuatiwa chombo
cha perverence rover kugusa kwenye kreta.
Kipaza
sauti kutoka kwenye chombo hicho pia kimetoa rekodi ya kwanza ya sauti kutoka
katika sayari hiyo.
Picha
moja ya kustaajabisha ilionesha kutawanyika kwa miamba yenye giza ikiwa
miepesi na yenye mashimo. "Tunatumia maneno haya ya jumla katika hatua
hii ya awali mpaka tutakapopata na data zaidi ambayo inatuwezesha kupima
nadharia zetu na kutoa tafsiri zenye ujasiri zaidi," alisema Ken
Williford, kiongozi wa mpango huo
Kwa
jumla, timu ilisema wamepokea zaidi ya gigabytes 30 za habari, na zaidi ya
picha 23,000 za asili ya vyombo vya moto vilivyotua.
"Najua
umekuwa mwaka mgumu kwa kila mtu na tunatumai kuwa labda picha hizi ...
zitawafurahisha watu," alisema Justin Maki, mwanasayansi wa picha.
Chombo
hicho chenye magurudumu 6 sasa kitakuwa kwenye sayari hiyo kwa takriban miaka
miwili katika mabonde ya eneo hilo, kikitafuta ushahidi unaonesha shughuli za
maisha ya awali.
Ikweta
ya Jezero inadhaniwa kwamba imekuwa na ziwa kubwa kwa miaka bilioni kadhaa
iliyopita.
Na mahali ambapo kumekuwa na maji, kuna uwezekano mkubwa kulikuwa na maisha yalioendelea eneo hilo.
Leave a comment