Habari

NIGERIA: Wasichana 300 Watekwa Nyara Baada ya Shule Kuvamiwa na Majambazi

Kulingana na ripoti kutoka vyombo vya habari nchini Nigeria, watu wenye bunduki walivamia eneo la shule asubuhi na mapema, Ijumaa ya Februari 26

Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa majambazi wameshambulia Shule ya Sekondari ya Wasichana inayomiliiwa na serikali ya Nigeria, Jangebe katika mkoa wa Zamfara na kuwateka nyara wasichana 300 wa shule hiyo.

Kulingana na ripoti kutoka vyombo vya habari nchini Nigeria watu wenye bunduki walivamia eneo la shule asubuhi na mapema, Ijumaa ya Februari 26

Kamanda wa Polisi kanda hiyo bado hajatoa maelezo ya kina kuhusiana na tukio hilo.

Tukio la Kutekwa nyara kwa wasichana wa shule ya Zamfara linakuja wiki mbili tu baada ya wanafunzi na waalimu wa Chuo cha Sayansi cha Serikali,Kagara nchini Niger kutekwa nyara.