Habari

Netflix Yafikiria Kuzuia Matumizi ya Nywila moja kwa Akaunti tofauti

Netflix inajaribu kuzuia watumiaji wasiostahiki, ingawa haijulikani ni watu wangapi wanaotumia huduma yao bila kuzingatia sheria husika za mtandao huo wa filamu

Baadhi ya watumiaji wameripoti juu ya kuona ujumbe unaosomeka, "Ikiwa hauishi na mmiliki wa akaunti hii, unahitaji akaunti yako mwenyewe kuendelea kutazama."

Inasemekana Jaribio la kutuma ujumbe huo kwa watumiaji wa Mtandao wa filamu wa Netflix limeundwa ili kusaidia kuhakikisha watumiaji wa mtandao huo wameidhinishwa kufanya hivyo.

Maamuzi yakuondoa orodha ya watumiaji ambao bado hawajisajili bado haujafanywa.

Katika jaribio, watumiaji wanaweza kuthibitisha kama ni watumiaji halali wa akaunti ya Netflix ikiwa watafanikiwa kuingiza code iliyotumwa kwenye ujumbe wa simu ama barua pepe.

Kiuhalisia, mazoea yaliyojengeka ya watu kutumia namba ya siri moja ili kupata huduma ya Netflix inakiuka sheria ya mtandao huo ambayo inakataza matumizi ya pamoja ya akaunti na watu wasioishi kaya moja na mteja. "Huduma ya Netflix na maudhui yoyote yanayotazamwa kupitia huduma hiyo ni kwa matumizi yako ya kibinafsi na wala sio ya kibiashara na hayawezi kutumiwa na watu wasio wa kaya yako,"

Watumiaji ambao wamepokea taarifa mpya pia wamepata fursa ya kuchelewesha shughuli ya uhakikishaji wa akaunti zao.

Netflix inajaribu kuzuia watumiaji wasiostahiki, ingawa haijulikani ni watu wangapi wanaotumia huduma yao bila kuzingatia sheria husika za mtandao huo wa filamu.

Majukwaa ya kuonyesha filamu mtandaoni kama Netflix, HBO Go, Amazon Prime na Disney +, huruhusu watumiaji kuwa na wasifu zaidi ya moja ndani ya akaunti moja lakini sheria na masharti zinaonyesha akaunti hiyo hupaswa kutumika na watu wa familia moja.

Akiwasilisha mada kupitia mtandao mnamo 2016, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Netflix, Reed Hastings alinukuliwa akisema kitendo cha watu kutumia nywila moja ni suala ambalo tunapaswa kujifunza kuishi nalo kwani kuna mazingira mengi ambayo yanakaribisha matumizi ya namna hiyo, mfano mpenzi na watoto, hivyo hakuna kizuizi dhahiri.

Mnamo 2020 Netflix ilikuwa na wanachama milioni 37 ambao walipata kuongezeka hadi kufikia milioni 200 ulimwenguni kote mwaka 2021.