Afrika

MTV Base watangaza kuahirisha Tuzo za MTV Afrika 2021

Wanamuziki watano kutoka Tanzania akiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, Rostam (Roma Mkatoliki na Stamina) pamoja na Harmonize walikuwa wakiwania tuzo

MTV wametangaza kuahirisha tuzo hizo zilizokuwa zifanyike Kampala Februari 20, 2021 mpaka watakapotangaza tena.

 

Kufuatia hali ya kisiasa nchini Uganda, mashabiki wa muziki kutoka pande mbalimbali za dunia waliwakosoa MTV kwa kupanga tuzo hizo kufanyika nchini humo. 

 

Wanamuziki watano kutoka Tanzania akiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, Rostam (Roma Mkatoliki na Stamina) pamoja na Harmonize walikuwa wakiwania tuzo. Diamond alitajwa kuwania tuzo mbili ikiwemo msanii bora wa mwaka na mtumbuizaji bora wakati wa corona. Zuchu alikuwa akiwania kipengele cha msanii bora chipukizi, Rostam wakiwania kundi bora na Harmonize akiwania kipengele cha msanii bora wa kiume. 

 

Diamond Platnumz pia alikuwa ni moja ya wa wasanii ambao walipangwa kutumbuiza katika hafla ya utoaji wa tuzo. 

 

Una maoni gani juu ya kuahirishwa kwa tuzo hizi?