Duniani

Mtoto wa Wiki 6 Afariki Dunia Baada ya Kukumbwa na Mshtuko wa Moyo Wakati wa Ubatizo

Baba wa mtoto huyo aliweka wazi kuwa karibu mililita 110 za maji zilipatikana kwenye mapafu ya mtoto huyo

Tukio hilo limetokea Romania katika kanisa la Orthodox hali iliyopelekea kanisa kuwa chini ya shinikizo la kubadilisha taratibu zilizopitwa na wakati zinazotumika kuendesha kanisa hilo.

Kulingana na tamaduni za Orthodox, mtoto alidumbukizwa kwenye maji ya Baraka mara 3 na kuwaishwa hospitalini baada ya kupata mshtuko wa moyo na baada ya muda mchache mtoto huyo alifikwa na umauti huku majibu ya dakltari yakieleza kuwa mapafu yake yalikutwa yamejaa maji.

"Mtoto wa mwezi mmoja na nusu alipata mshtuko wa moyo akiwa kanisani baada ya ibada ya ubatizo," Dan Teodorovici, Msemaji wa hospitali hiyo alisema akinukuliwa na Independent.

"Mtoto alipewa mipira ya kumsaidia kupumua punde baada ya kufika hospitalini hapo. Akiwa na hali mbaya alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi wa hospitali."

Baba wa mtoto huyo aliweka wazi kuwa karibu mililita 110 za maji zilipatikana kwenye mapafu ya mtoto huyo.

Akiwa amekasirishwa na jinsi kasisi huyo alivyofanya ubatizo huo hata baada ya kuona kuwa mtoto ana shida, baba huyo aliliambia chombo cha habari kijulikanacho kama, Monitorul de Suceava, "Mtoto alikuwa akilia lakini mchungaji alimzamisha mara tatu ndani ya maji huku mtoto akavuta maji. Nilimuondoa, nikamfuta, baada ya kufika kwa madaktari nilibaini amevuta milimita 110 za maji ... Ukiona mtoto ana ameachama mdomo na analia hautamzamisha kabisa ndani ya maji, sivyo? "

"Mtoto alikuwa na damu puani. Nilimuinamisha uso chini ili kutoa maji. Lakini Hakupona," alisema baba huyo, alinukuliwa na Global News.

Kifo cha mtoto huyo kikiibua hisia na kusababisha watu zaidi ya 61,000 kutia saini ombi la kubadilisha ibada ya ubatizo. Kukomesha ya Ubatizo kwenye Kanisa la Orthodox sio lengo la ombi, "lakini kubadili tabia hiyo ya kikatili wakati mwingine ambayo inajumuisha hatari ya kuzama, haswa ikiwa ni watoto wenye shida za kiafya," Vladimir Dumitru, ambaye alianzisha ombi hilo aliiambia CNN.

Aliongeza, "Ombi halijaelekezwa dhidi ya taasisi ya Kanisa au dhidi ya makuhani lakini lina nia ya kujenga."

Kufuatia kifo cha kutisha cha mtoto huyo, polisi wamefungua uchunguzi wa mauaji ya kuua kuhusisha kuhani aliyefanya sherehe ya ubatizo.

Ingawa baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wameonesha kuonesha mabadiliko, wengine wamepinga suala hilo, licha ya vifo kadhaa kutokea katika miaka michache iliyopita.