Habari

Mpenzi wa Rapa AKA Afariki kwa Kujirusha kutoka Ghorofa ya 10

Mashuhuda ambao walikuwa wakikaa katika hoteli hiyo walielezea jinsi walivyosikia mwanamke akipiga kelele, ikifuatiwa na sauti kubwa ya “dufu”

Mchumba wa rapa AKA wa Afrika ya Kusini, Nelli Tembe mwenye umri wa miaka 22, amefariki akidaiwa kujirusha kutoka kwenye ghorofa ya 10 asubuhi ya leo katika hoteli moja ya kifahari ya Papperclub iliyo katikati ya jiji la Cape Town nchini humo.

Familia ya Anele “Nelli” Tembe na mwanamuziki mashuhuri, Kiernan “AKA” Forbes wamethibitisha kifo cha mwanadada huyo.

"Tupo katika hali ya mshituko na tunapambana na hisia zetu, alikuwa wa kipekee aliyebarikiwa na mwenye uwezo wa kufanya mambo mengi sana katika maisha yake," familia hizo zilisema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumapili alasiri.

Mashuhuda ambao walikuwa wakikaa katika hoteli hiyo walielezea jinsi walivyosikia mwanamke akipiga kelele, ikifuatiwa na sauti kubwa ya “dufu”

Pia mashuhuda waliongeza kuwa wenzi hao walionekana usiku uliopita katika lifti ya hoteli wakiwa katika mapenzi mubashara.

Taarifa kutoka kwa familia hizo ilisema: "AKA yupo katika wakati mgumu na amezungukwa na familia na marafiki zake wa karibu."

Watoa huduma ya kwanza walisema walifika eneo la tukio lakini walitawanywa baada ya kuambiwa kuwa binti huyo ameshapoteza Maisha.

Mpaka sasa Polisi bado wapo kwenye Uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho.