
Emma Coronel Aispuro, mwanamitindo wa zamani mwenye umri
wa miaka 31, amekamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles
jimboni Virginia na anatarajiwa kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kijimbo mjini
DC kupitia kanda ya video, imesema idara ya haki nchini humo.
Bi Coronel Aispuro anashtakiwa kwa kushiriki katika njama
ya kumsaidia mumewe kuendesha biashara yake haramu ya kusambaza dawa aina ya
Cocaine, Methamphetamine, heroin na bangi pamoja na kupanga njama ya kumsaidia
kutoroka kutoka jela moja ya Mexico mwaka wa 2015.
Kukamatwa kwake ni tukio la muendelezo katika sakata la kimataifa linalomhusisha Guzman, aliyekuwa
kiongozi wa muda mrefu wa kundi la ulanguzi wa dawa za kulevya la Sinaloa
Guzman kwasasa anahudumia kifungo cha maisha jela mjini New York kwa kuhusika katika ulanguzi wa mihadarati na fedha.
Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 63 ni kiongozi wa zamani wa kundi la walanguzi wa mihadarati wa Sinaloa ambalo ndilo lililokuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji wa mihadatari nchini Marekani
Leave a comment