Habari

MISRI: Meli ya Ever Given Yawekwa Kizuizini Mpaka Itakapokamilisha Fidia

Misri ilipoteza karibu shilingi bilioni 34.785 ya mapato yatokanayo na Mfereji huo kipindi Meli hiyo ilipoziba njia ya maji

Mamlaka inayosimamia Mfereji wa Suez imesema kuwa Meli ya Evergreen ambayo ilizuia Mfereji wa Suez na kukwamisha shughuli za biashara kwa takribani wiki moja imezuiliwa kwa amri ya mahakama mpaka mmiliki atakapolipa fidia ya dola za kimarekani milioni 900 (shilingi trilioni 2.87).


Misri ilipoteza karibu shilingi bilioni 34.785 ya mapato yatokanayo na Mfereji huo kipindi Meli hiyo ilipoziba njia ya maji.

MV "Ever Given imewekwa kizuizini kutokana na kushindwa kulipa fidia ya dola za kimarekani milioni 900" Mkuu wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez Osama Rabie alinukuliwa akisema katika gazeti la serikali, Al-Ahram.


Meli ya Evergreen inayomilikiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Taiwan ilikwama katika Mfereji wa Suez mnamo Machi 23 huku ikiwa na bidhaa za thamani ya karibu dola bilioni 9.6, kwa mujibu takwimu za usafirishaji.