Duniani

Mfahamu Robert Wadlow, Kijana mrefu Zaidi Duniani Ambaye Rekodi yake Guinnes Haitokuja Kuvunjwa na Yeyote Yule

Robert Pershing Wadlow ni nani?


Wadlow alizaliwa mnamo Februari 22, 1918 huko Alton, Illinois akiwa na uzito wa kilogram 4, mwenye afya tele na furaha akionekana kama watoto wengine.

Akiwa na umri wa mwaka mmoja Robert Wadlow alianza kukua kawaida lakini tofauti na watoto wengi, alikua haraka sana na alipofikisha umri wa miezi 6, tayari alikuwa na uzito wa kilo 13 (wastani wa kawaida kwa mtoto wa kiume huwa ni nusu yake) huku akiwa na kilo 20 urefu wa futi 3 pindi alipotimiza mwaka mmoja.

Wakati Wadlow akiwa na umri wa miaka 5, alikuwa na urefu wa futi 5, inchi 4 akivaa nguo ambazo za rika la vijana. Chakushangaza pindi Wodlow alipotimiza miaka 8, alikuwa tayari mrefu kuliko baba yake (akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 11).


Robert Wadlow akiwa amesimama na familia yake

Alipotimiza umri wa miaka 13, alikua Skauti Mrefu zaidi ulimwenguni kwa futi 7, cm 4 akivaa sare maalum kwani vipimo vya nguo vya kawaida visingefaa.

Nini kilipelekea awe na Urefu Kupita Kiasi?

Hapo baadae  akiwa na umri wa miaka 12 madaktari waligundua kuwa Wadlow alikuwa na hali ambayo kitaalamu ilifahamika kama hyperplasia iliyosababisha ukuaji wa haraka na wa kupindukia kwa sababu ya kiwango cha juu cha homoni za ukuaji mwilini.

Inasemekana kama Wadlow angezaliwa leo, labda asingekuwa mrefu kiasi hicho kwani sasa kuna upasuaji wa kisasa na dawa ambazo zinaweza kukomesha ukuaji usio na udhibiti bahati mbaya wakati huo madaktari waliogopa kumfanyia upasuaji kwakuwa Imani ya kuweza kumsaidia ilikuwa ni ndogo.

Wadlow aliachwa aendelee kukua lakini licha ya kimo chake kuongezeka, wazazi wake walijaribu kufanya maisha yake kuwa ya kawaida kadri walivyoweza.

Shule zilimtengenezea madawati maalum, zikiongeza nafasi chini ili asikae kwa tabu darasani. Na kwa kuwa Wadlow alikuwa mkubwa zaidi akifuatiwa na wadogo zake (ambao wote walikuwa na urefu wa wastani na uzani), alitarajiwa kucheza na ndugu zake lakini haikuwa hivyo kwani wadlow alipendelea zaidi kazi ya kupiga picha.

Ingawa alikuwa mzima kiafya katika miaka yake ya ujana, baadae alianza kukumbana na matatizo kiafya yaliyosababishwa na urefu uliokithiri, miguu yake ilianza kufa ganzi suala lililopelekea kutoona malengelenge au maambukizo. Mwishowe, pia alihitaji magongo ya kuvaa miguuni yakifahamika kama (braces) na fimbo ili vimsaidie kutembea.

Mnamo 1936, kundi linalojulikana kama Ringling Brothers lilimuona Wadlow na kupendekeza wazunguke nae katika matamasha yao hasa wakati pindi watoto wadogo wakiwa wanafanyamatamasha yao. Kwa furaha yao Wodlow alikubali kufanya nao ziara.


Robert Wadlow akilinganisha ukubwa wa viatu na mtoto wa kundi la Ringling Brothers

Wodlow alikuwa na uwezo wa kuvutia umati mkubwa kila mahali alipokanyaga wakati wa maonesho hayo ya “Circus”. Haikupita mda mrefu Wodlow akawa mtu mashuhuri kama siyo shujaa wa mji wa Alton.

Ingawa maisha ya mtu mrefu zaidi duniani yalikuwa ya kufurahisha, lakini pia yalikuwa magumu sana. Katika Nyumba, sehemu za umma, na vitu vya nyumbani hakukuwa na vitu maalum kwa ajili yake hivyo ilibidi afanye makubaliano na marekebisho ili apate mbadala.

Wodlow alikuwa akivaa magongo miguuni (braces) ili aweze kutembea vizuri cha kusikitisha magongo hayohayo ndiyo yaliyopelekea anguko lake.

 Ilikuaje?

Kutokana na ganzi katika miguu yake, Wadlow alishindwa kugundua shida katika mguu yake ambaye ilitokana na magongo aliyokuwa akivaa miguuni ambayo yalimkandamiza na kumchubua kifundo cha mguu mnamo mwaka 1940.

Wakati Wadlow alikuwa akionekana katika Tamasha la Michigan’s Manistee National Forest Festival, hakugundua kuwa alikuwa na malengelenge kwenye mguu ambayo yalimsababishia homa kali. Wodlow alikimbizwa hospitali ambako alifanyiwa upasuasi wa dharula na kuongezewa hela.

Jambo la kusikitisha madaktari walishindwa kuokoa maisha ya Wadlow. Maneno yake ya mwisho yakiwa, "Daktari anasema sitarudi nyumbani kwenye ... sherehe," akimaanisha sherehe ya kumbukumbu ya ndoa ya bibi na babu yake.

Ingawa alifikwa na umauti akiwa na umri mdogo, Robert Wadlow aliacha urithi mkubwa. Tangu 1985, sanamu ya shaba ya Wadlow imesimama kwa kujigamba huko Alton, kwenye maeneo ya “University School of Dental Medicine” na katika Jumba la kumbukumbu ya Historia na Sanaa ya Alton. Wageni huweza kuona picha za Wadlow pamoja na jozi chache za viatu vyake, dawati lake la shule, kofia yake ya kuhitimu na joho.


Sanamu la Robert Wadlow likiwa limesimama katika makazi alimukuwa akiishi Alton, Illinois.

Kwa sasa sanamu zingine za Wadlow zimewekwa katika Jumba la kumbukumbu la ‘Guinness World Records’. Kumbukumbu hizo mara nyingi hujumuisha fimbo kubwa ya kupimia, kwa hivyo wageni wanaweza kushangaa jinsi Wadlow mrefu alivyosimama na kuweza kujilinganisha nae.

Hata hivyo ni mabaki machache tu yaliyobaki kama ukumbusho wa Wadlow kwani muda mfupi baada ya kifo chake, mama yake aliharibu takribani vitu vyote vilivyowahi milikiwa na marehemu ili kulinda heshima yake na kuepusha watu wenye tamaa ya kutaka kupata faida kutokana na hali ya mwanae.

Jambo zuri ni kuwa hadithi yake ya kusisimua inabaki, picha zake nzuri zimebaki vile vile. Mpaka sasa hakuna mtu aliyewahi kufikia urefu wa Wadlow na wakati huu, inaonekana hakuna uwezekano kwa mtu kuja kuvunja rekodi hiyo.