
Baraza la Libya linaloongozwa na Umoja wa
Mataifa limepiga kura juu ya uchaguzi wa serikali ya mpito na kumchagua mfanyabiashara
Mohammed al-Menfi kuwa mkuu wa baraza la urais huku balozi wa zamani wa Libya
nchini Ugiriki, Abdulhamid Dbeibeh kama waziri mkuu.
Uchaguzi wa serikali moja unakusudia kumaliza
mgawanyiko uliokuwa nchini Libya ambao umedumu kwa zaidi ya miaka mitano huku
serikali mbili zinazopingana na vikundi vyao vyenye silaha, vikiendesha sehemu
tofauti za nchi hiyo iliyopo Kaskazini mwa Afrika.
Wajumbe sabini na nne wa Baraza la Mazungumzo
ya Kisiasa la Libya (LPDF), ambalo lilijumuisha Walibya kutoka pande tofauti za
kisiasa, walichagua orodha ambayo ilijumlisha waziri mkuu na mkuu wa Baraza la
Rais.
Tangu 2014, udhibiti wa Libya umegawanyika
kati ya serikali 2; moja yenye makao mjini Tripoli ikiongoza upande wa
magharibi, huku nyingine iliyoungwa mkono na makundi kadhaa yenye silaha
ikiidhibiti sehemu ya mashariki ya nchi hiyo.
Katika machafuko hayo, mataifa ya kigeni
yamekuwa yakiunga mkono kambi za wapinzani.
Uturuki inaunga mkono Serikali Tripoli (GNA),
wakati Urusi, Falme za Kiarabu na Misri wanaunga mkono Jeshi la Kitaifa la
Libya (LNA) la Khalifa Haftar upande wa mashariki.
Washiriki wa mazungumzo ya Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya suala la kupigia kura wagombea wa serikali ya mpito mwezi huu ambapo . Mkutano uliofanikisha uchaguzi huo umefanyika karibu na Geneva, ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa.
Leave a comment