Habari

LHRC: Tumefarijika na Hotuba ya Rais

Ujumbe huo umeonesha kujengeka kwa imani ndani ya kituo hicho ambacho mara kwa mara kimekuwa kikikosoa mwenendo wa serikali ya awamu ya tano kuhusu ukiukwaji wa haki ya uhuru wa kujieleza uliokuwa ukifanywa na uongozi uliopita

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) kimeeleza kufurahishwa na kufarijika na hotuba iliyotolewa leo na Rais Samia Suluhu iliyogusa mambo mbalimbali ikiwemo uhuru wa kujieleza na uhuru kwa vyombo vya habari.

 

Katika hotuba yake Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni kufungulia vyombo vyote vya Habari vilivyofungiwa pamoja na kusimamia sheria bila uonevu.

 

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii LHRC imeandika “tumefarijika sana na hotuba iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali wa juu serikalini.”


Ujumbe huo umeonesha kujengeka kwa imani ndani ya kituo hicho ambacho mara kwa mara kimekuwa  kikikosoa mwenendo wa serikali ya awamu ya tano kuhusu ukiukwaji wa haki ya uhuru wa kujieleza  uliokuwa ukifanywa na uongozi uliopita.