
Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo imewashtumu waasi wa FDLR wenye asili ya Rwanda, kwa kumshambulia na
kumuua balozi wa Italia nchini humo Luca Attanasio hapo jana karibu na mji wa
Goma, mashariki mwa nchi hiyo.
Hata hivyo, kundi la FDLR limekanusha kuhusika
na shambulizi hilo, kwa kile inachosema vikosi vyake viko mbali na eneo la
shambulizi hilo.
Maafisa katika mbuga ya wanyamapori ya Virunga
wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara lililoshindikana pindi walipoingilia kati mara moja.
Aidha, Ofisi ya Rais, DRC imethibitisha kujiunga na uchunguzi wa mauaji
hayo ambapo Maafisa kutoka ofisi ya rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakitarajiwa
kupelekwa mjini Goma kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia
nchini humo.
Maafisa hao wataondoka leo kuelekea Goma na
watakuwa wakiwasilisha ripoti kwa za mara kwa mara kwa rais.
Balozi Luca Attanasio aliuawa pamoja na watu
wengine wawili katika shambulio baya lililofanywa dhidi yao na kundi la waasi
wenye bunduuki lililoushambulia msafara wa shirika la mpango wa chakula
duniani WFP uliokuwa ukielekea wilayani Rutshuru.
Kwa mujibu wa vyanzo vyengine Balozi Attanasio
alikufa kutoka na majeraha sambamba na dereva mmoja na mlinzi mmoja wa msafara
huo.
Milio ya bunduki iliendelea kusikika katika
maeneo ya kilimanyoka na Kanyamahoro katika mbuga ya wanyampori ya virunga,
hali iliyo sababisha wasiwasi mkubwa kwa wakaazi waishio kandoni na mbuga hiyo.
Carly Nzanzu Kasivita ni Gavana wa kivu ya kaskazini aliye thibitisha vifo vya
watu hao.
Huku hayo yakiarifiwa, Waziri Mkuu wa Italia,
Mario Draghi, ameelezea masikitiko yake makubwa kutokana na mauaji hayo,
akisema kuwa jamhuri nzima inaomboleza vifo vya watumishi hao wa umma.
Leave a comment