Habari

#KENYA: Kiongozi wa Chama cha ODM, Raila Odinga Akutwa na Corona

Taarifa ya Daktari David Olunya wa Hospitali ya Nairobi pia imethibitisha kuwa Waziri Mkuu wa zamani ana crona wimbi la pili (SARS-CoV-2)

Katika taarifa Alhamisi, Raila amewaambia Wakenya kuwa corona ipo na kuwataka hatua zote zilizoainishwa ili kujikinga na maambukizi hayo.

Aliongeza, "Pamoja na ukweli kwamba ninajisikia mwenye nguvu na mwenye hali nzuri baada ya kukaa siku chache hospitalini, nimekubaliana na madaktari wangu kukaa karantini kwa lazima."

Taarifa ya Daktari David Olunya wa Hospitali ya Nairobi pia imethibitisha kuwa Waziri Mkuu wa zamani ana SARS-CoV-2.

"Anaendelea vizuri na matibabu anayopokea katika Hospitali ya Nairobi na afya yake inaimarika," daktari wake binafsi alisema.

Kauli ya daktari iliondoa minong’ono iliyokuwa ikihoji hali ya afya ya Raila baada ya kutoonekana hadharani Jumanne katika maadhimisho ya miaka tatu ya mapatano na Rais Uhuru Kenyatta.

"Raila alienda kufanya uchunguzi wa kawaida wa matibabu katika Hospitali ya Nairobi mnamo Machi 9 baada ya kuhisi uchovu. Alikuwa ametoka kwenye kampeni nzito na alihitaji kufanyiwa uchunguzi,”alielezea Dk Olunya.

Kiongozi huyo wa chama cha ODM alilazwa hospitalini mnamo Machi 9 baada ya kulalamika juu ya uchovu na maumivu ya mwili.

Katika sasisho la Alhamisi jioni Wizara ya Afya iliripoti kwamba

Kenya imesajili kesi mpya 829 za kesi za corona kutoka sampuli 6239 za vipimo vilivyofanywa ndani masaa 24.