
Kenya imeagiza dozi milioni 24 za chanjo ya chanjo
hiyo ambayo inatarajia wiki ya pili ya mwezi Februari Licha ya wasiwasi wa hivi
karibuni uliopelekea Afrika Kusini kusitisha mipango ya kuanza utoaji chanjo ya
AstraZeneca na Oxford kwa madai ya kuwa utafiti umeonesha kuwa chanjo hizo
hazina ufanisi katika kuzuia magonjwa mepesi na ya wastani kutoka kwenye aina
mpya ya virusi,
Nchi hiyo ambayo ina jumla ya idadi ya watu milioni
47 imesharipoti visa 97,398 vya maambukizi ya corona na vifo 1,694.
Waziri wa afya, Mutahi Kagwe alinukuliwa na gazeti
la Standard mnamo Alhamisi iliyopita akisema chanjo hizo zitaanza kutua mwezi
ujao.
Serikali imeagiza chanjo hizo kupitia mpango wa
Umoja wa Afrika unaolenga kuhakikisha mataifa ya Afrika hayaachwi nyuma, Kagwe
alisema.
Wafanyakazi wa sekta ya afya na wafanyakazi wengine
muhimu kama walimu watapewa kipaumbele katika ugawaji wa chanjo hiyo,waziri
alisema ingawa hakuweka wazi ni kiasi gani chanjo hiyo itagharimu.
Licha habari ya wasiwasi kuhusu chanjo ya AstraZeneca kusambaa, jopo la Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema faida za chanjo ya corona iliyotengenezwa na AstraZeneca na chuo kikuu cha Oxford huzidi madhara yote yanayoweza sababishwa na chanjo hiyo hivyo dozi hiyo inafaa kwa matumizi.
Leave a comment