Habari

Kagame, Rais wa Kwanza Afrika Mashariki Kupigwa Chanjo ya Corona

Ingawa haijaainishwa ni chanjo gani, Rwanda tayari imeshapokea dozi 100,000 za dawa ya Pfizer-BioNTech na dozi 240,000 za dawa ya AstraZeneca / Oxford

Siku ya Alhamis katika akaunti rasmi ya urais, zilichapishwa picha za Kagame, 63, na mkewe Jeannette wakipokea chanjo ambayo na ujumbe ulioweka wazi kwamba tayari watu 230,000 wameshapokea chanjo hiyo.

Ingawa haijaainishwa ni chanjo gani, Rwanda tayari imeshapokea dozi 100,000 za dawa ya Pfizer-BioNTech na dozi 240,000 za dawa ya AstraZeneca / Oxford.

Rwanda, nchi yenye idadi ya watu milioni 12, imepanga kufikia asilimia 30 ya idadi ya watu katika ugawaji chanjo ndani yam waka huu na asilimia 60 pindi itakapofika mwisho wa 2022.

Mnamo Februari, Rwanda ilikuwa nchi ya kwanza katika Afrika Mashariki kuanza kugawa chanjo dhidi ya corona huku ikilenga makundi ya watu yaliyo hatarini kama wafanyakazi wa huduma ya afya punde tu walipopokea dozi 1,000 za Moderna.

Nchi hiyo imepima corona zaidi ya watu milioni na kugundua visa karibu 20,000 na vifo 271 tangu kuzuka kwa gonjwa hilo.

Mpaka sasa Rwanda, Kenya na Uganda zimeanza kutoa chanjo katika nchi za Afrika Mashariki.