
Tamko la kuahirishwa kwa bunge la Ghana limekuja kufuatia ongezeko la maambukizi kati ya wabunge
na wafanyakazi na linataraijia kurejea tena baada ya wiki tatu.
Spika Alban Bagbin aliliambia bunge siku ya Jumanne ya
tarehe 17 kuwa wabunge 275 na wafanyakazi 151 kati ya 500 walipata virusi vya
corona.
Spika pia aliwataka wabunge wengine na wafanyikazi wa
bunge kupima corona ikiwa bado hawajafanya hivyo.
Bagbin alisema uamuzi wa kusimamisha shughuli ulifanywa
baada ya kuzungumza na uongozi wa bunge.
Alisema kamati ya uteuzi wa bunge itaendelea kukutana na
wateule wa nyadhifa za wizara katika utawala wa Rais Nana Akufo-Addo, ambaye
alichaguliwa tena mnamo Desemba.
Ghana imekwisharekodi zaidi ya kesi 72,300 za maambukizi
ya corona na vifo 472, kulingana na takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Chuo
Kikuu cha Johns Hopkins.
Leave a comment