Afya

Fahamu Faida za Kusafisha Kinywa Zaidi ya Mara Moja kwa Siku

Kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku husaidia sana afya ya kinywa na kukiweka kinywa kwenye hali nzuri muda wote.

Ni jambo la kawaida kuamka asubuhi na kusafisha kinywa unapotoka kulala. Lakini unafahamu unafahamu kuwa ni muhimu kuendelea kusafisha mchana hata baada ya kumaliza ‘ratiba’ ya kawaida ya asubuhi? Kwa kawaida watu wengi wamezoea hali ya usafi wa kinywa kufanywa asubuhi tunapo amka lakini kwa kiafya inatakiwa kwa binadamu kusafisha kinywa chake angalau Mara mbili kwa siku, pale anapo amka asubuhi na pia usiku kabla hujaenda kulala ukishamaliza mlo wa usiku. Lengo ni kuepusha na kuondoa mabaki ya chakula yanayoganda kwenye meno na kupelekea kuwa na magonywa ya jino, fizi, kunuka mdomo nk.

Kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku husaidia sana afya ya kinywa na kukiweka kinywa kwenye hali nzuri muda wote. Ni sawa na kuchukulia unapotoka kufanya mazoezi ya mwili kama kukimbia au kazi ngumu vile unapotokwa na jasho utakapokwenda kuoga na mwili wako utakavyojisikia vizuri na ndivyo inavokuwa kwenye usafishaji kinywa mara kwa mara utakuwa unajisikia vizuri kwani kinywa kinakuwa kwenye hali nzuri kama unavokuwa kwa mwili unapooga baada ya mazoezi au kazi ngumu.

Hatua za kusafisha kinywa

Unaweza kuwa unafahamu jinsi ya kupiga mswaki, lakini ni vyema kufahamu hatua za kupiga mswaki kwa usahihi. Fuatilia hatua sita za kupiga mswaki.

 

i.             Weka kiasi kidogo cha dawa katika mswaki wako, kwa kiasi kidogo namaanisha saizi ya harage. Kuweka kiasi kikubwa kunaweza kusababisha kujaa kwa mate yenye povu la dawa haraka na kushindwa kuendelea kupiga mswaki. Vilevile kunaweza kusababisha kumeza dawa, na kusababisha madhara.

 

ii.            Anza kupiga mswaki kutokea upande wa nyuma ya kinywa kwa kuweka mswaki wako angalau nyuzi 45 katikati ya fizi. Kuwa makini kutotumia nguvu kubwa ili usiumize fizi zako

 

iii.          Tumia walau dakika mbili hadi tatu kuzungusha mswaki katika maeneo yote ya meno ndani ya kinywa, ukitumia si chini ya sekunde 15 katika maeneo yote ya kinywa: juu kulika, kushoto, chini kulia, kushoto. Hii ina maana kuwa utatumia sekunde 30 kwa kila upande.

 

iv.          Usisahau kusafisha meno ya mbele. Hakikisha unasafisha kwa ndani na nje. Unaposafisha meno ya mbele kwa nje, ni vema ukisugua kwa wima (vertical).

 

v.           Safisha ulimi kwa kuusugua taratibu ili kuondoa harufu mbaya ya kinywa.

 

vi.          Sukutua kinywa. Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa kusafisha kinywa kwa maji kunaondoa floraidi kutoka kwenye kinywa, huku zingine zikionesha kuwa hakuna haja ya kufanya hivyo, unaweza tu kutema masalia baada ya kusafisha kinywa, hivyo uamuzi wa kutumia maji au la ni wa kwako.

Faida za kusafisha/kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku

i.            Kuepukana na magonjwa ya fizi

Dr. Augustine Lukoma anaeleza kuwa usafi wa mdomo husaidia kuepuka magonjwa ya fizi ambayo kupelekea kupoteza meno kwa watu wenye umri mkubwa/watu wazima kutoka na kutozingatia usafi wa meno, lakini tukizingatia usafishaji wa meno na pia kumuona dactari wa meno Mara kwa Mara kunasaidia kuepuka na ugonjwa kama wa fizi ambao Dr. Augustine ameleza pia kupelekea maradhi mengine kama kisukari na kiharusi

ii.            Kuepusha kuoza kwa meno

Kusafisha meno mara kwa mara husaidia kuepusha kuoza kwa meno kutokana na meno kuwa kwenye hali safi na wadudu kutoweza kushambulia na kuozesha meno ambapo kuna mpelekea mtu kung'oa meno na hata kupata vidonda vya mdomoni. Ni vizuri kuzingatia usafi wa meno kwa kusafisha zaidi ya mara moja ili kujikinga na kuoza kwa meno.

iii.          Kuepuka na harufu mbaya mdomoni

Dr. Lukoma anaeleza kuwa takriban asilimia 85 ya watu wenye tatizo la harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya meno na kinywa ambayo kupelekea tatizo hili la harufu mbaya kinywani, magonjwa haya wanaweza kuepukana nayo endapo tutazingaitia usafi wa kinywa kwa kusafisha mara kwa mara hata usiku kabla ya kwenda kulala ili kuzuia vijidudu kuozesha meno na kusababisha harufu mbaya za mdomo.

iv.         Kuepuka magonjwa ya mwili yanayo tokana maradhi ya kinywa

Hapo awali tumeeleza kuwa maradhi ya kinywa kama fizi kuweza kusababisha magonjwa kama kisukari, kiharusi/stroke kwa watu wazima, ili kuepukana na magonjwa haya ni vyema kuwa makini na afya ya kinywa kwa kusafisha mara kwa mara na si tu mara moja kwa siku, kwani kusafisha mara kwa mara hupelekea kuua bakteria wanaoshambulia meno ambao hutokana na mabaki ya vyakula vinavyo baki kwenye meno na utoka kwa kusafishwa na mswaki kwa dawa ya meno.

Imeandikwa na Asma Tuwile.