Habari

Dkt. Mpango Athibitishwa kuwa Makamu wa Rais Tanzania

Jina la Dkt. Mpango lilitajwa leo bungeni na Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai baada ya kupokea jina la uteuzi kutoka kwa mpambe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Dkt.Philipo isdor Mpango athibitishwa kuwa Makamo wa Rais Baada ya kupitishwa rasmi na bunge kwa kura 363 za ndio ambazo ni sawa na asilimia 100 ya kura zote za zilizopigwa bungeni. 

Uteuzi wake ulifanywa leo tarehe 30/03/2021 ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa makamo wa Rais. Mh Samia Suluhu Hassan kuchukua nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama isemavyo Ibara ya 37(5) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kifo cha aliekuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.

Jina la Dkt. Mpango lilitajwa leo bungeni na Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai baada ya kupokea jina la uteuzi kutoka kwa mpambe wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akisoma barua kutoka kwa mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, Spika wa bunge amesema “Mh Spika nawasilisha bungeni Jina la Mh. Philip Isdor Mpango kwa nafasi ya Makamu wa Rais ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.” Mh. Job Ndugai.

Aidha, uteuzi wa Dkt. Mpango ulipokelewa kwa mikono miwili kwa wabunge na wananchi kwa ujumla hasa kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wameonesha hisia zao za wazi kukubaliana na uteuzi huo, huku wakimsifu Dkt.Philipo Mpango kama mchapakazi, muadilifu, ana busara na mtu atakaeisaidia Tanzania kufikia malengo yake.