Habari

Chanjo ya AstraZeneca Yathibitika kuwa Salama kwa 100%

Majaribio ya Marekani pia yanaonyesha kuwa chanjo ya AstraZeneca iko salama na 79% inafaa dhidi ya kuzuia dalili za magonjwa zinazohusianishwa na virusi vya corona

AstraZeneca imethibitishakuwa ufanisi wa chanjo yake baada ya matokeo ya majariio yaliyofanywa kutoa ushahidi kwamba chanjo hiyo imeonesha ufanisi wa 100% dhidi ya magonjwa yanayohusanishwa na corona.

AstraZeneca alisema katika taarifa kwamba uchambuzi wa usalama na ufanisi ulitokana na kuwafanyia majaribio washiriki 32,449 katika majaribio ya Marekani. “Ufanisi wa chanjo ulikuwa sawa kwa kabila na umri. Lakini kwa washiriki wenye umri wa miaka 65 na zaidi, ufanisi wa chanjo ulikuwa 80%, "ilisema taarifa hiyo.

Majaribio ya Marekani pia yanaonyesha kuwa chanjo ya AstraZeneca iko salama na 79% inafaa dhidi ya kuzuia dalili za magonjwa zinazohusianishwa na virusi vya corona, kulingana na Chuo Kikuu cha Uingereza cha Oxford, watengenezaji wa chanjo ya kampuni ya dawa.

Nchi kadhaa za Ulaya zilikuwa zimeacha kutumia chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni kwa sababu ya ripoti iliyoihusisha chanjo hiyo na kuganda kwa damu kwa watu waliopokea chanjo hiyo.Hata hivyo Wakala wa Madawa, Ulaya (EMA) walisema chanjo hiyo ni salama na haisababishi kuganda kwa damu.

Wiki iliyopita, Ufaransa, Ujerumani na Italia zilianza tena kutumia chanjo hiyo baada ya kusimama kwa muda kutokana na uvumi wa chanjo hiyo kusababisha damu kuganda.

Aidha, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliendelea kuhimiza watu uitumia chanjo hiyo wakidai kuwa faida yake inazidi madhara.

Afrika Kusini ilisimamisha matumizi ya chanjo hiyo kutokana na mashaka ya ufanisi wake dhidi ya aina nyingine ya virusi vya corona. Nchi hiyo iliuza kiasi cha dozi milioni ya AstraZeneca COVID19 kwa Umoja wa Afrika.

Dozi zilizouzwa kwa AU zitasambazwa kati ya nchi 14 za Afrika kwani Afrika Kusini sasa inatumia bidhaa za Pfizer na Johnson & Johnson.

Chanjo ya AstraZeneca imekuwa ikiongoza kutumiwa na nchi za ulimwengu unaoendelea.

Kulingana na Associated Press, chanjo ya AstraZeneca imeidhinishwa katika nchi zaidi ya 50. Nchini Marekani, chanjo za Moderna, Pfizer-BioNTech na Johnson & Johnson zimekuwa zikitumika.