
Ripoti mpya iliyotolewa Jumatano na kituo cha Kudhibiti na
Kuzuia Magonjwa (CDC) imedai kuwa "kuvaa barakoa mbili" sambamba na
kuvaa barakoa inayokutosha inaweza kupunguza makali ya kuenea kwa maambukizi ya
virusi vya corona.
Watafiti wamegundua kuwa kuvaa barakoa ya kitabibu huku
ikifunikwa na barakoa ya kitambaa inaweza kupunguza asilimia 92.5 ya chembechembe
za virusi vitakavyoingia mwilini.
Ingawa bado CDC haijapendekeza rasmi kuvaa barakoa mbili,
Mkurugezi wa kituo hicho, Dk Rochelle Walensky alizungumza jumatano ya tarehe
10 februari akidai kuwa watatoa muongozo mpya wa namna ya uboreshaji wa barakoa
ili ziweze funika vizuri pindi zinapovaliwa.
"barakoa inaweza kuwa na changamoto," Mkurugenzi
Rochelle Walensky alisema katika mkutano uliofanyika White House akielezea mwenendo wa virusi vya
corona. "Sayansi iko wazi. Kila mtu anahitaji kuvaa barakoa anapokuwa
kwenye umati wa watu au anapokuwa nyumbani kwake au akiwa na watu ambao sio
sehemu ya familia yake."
Utafiti huu wa CDC ulifanya ulinganifu kati ya mtu ambaye
hajavaa barakoa, mtu aliyevaa barakoa ya kitambaa yule aliyevaa barakoa ya
kitabibu na mwingine akavaa zote mbili; barakoa ya kitabibu ikifuatiwa na
barakoa ya kitambaa ambapo
Utafiti huo uligundua wakati watu wanavaa barakoa ya kitabibu
iliyofunikwa vizuri iliyofunikwa vizuri na barakoa ya kitambaa wanaweza
kupunguza makali ya kusambaa kwa virusi vya corona.
Kituo cha kudhibiti magonjwa, Marekani kilipendekeza watu waanze kuvaa barakoa za vitambaa tangu mnamo Aprili 2020, mwezi mmoja baada ya Marekani kushambuliwa vikali na janga la corona.
Leave a comment