Habari

BURUNDI: Wafungwa Zaidi ya 5000 Wanufaika na Msamaha wa Rais

Amri hiyo inatoa msamaha kwa "wafungwa wote waliohukumiwa vifungo vya miaka mitano kushuka chini isipokuwa wale wenye makosa makubwa kama mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita, wizi wa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria, wizi wa kutumia silaha, ugaidi, ubakaji, na usafirishaji haramu wa binadamu

Amri ya Rais Evariste Ndayishimiye ya Machi 5, 2021 Jumatatu ilitoa msamaha kwa wafungwa 5,255 nchini kote isipokuwa wale ambao walifanya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu mwingine mkubwa.

Amri hiyo inatoa msamaha kwa "wafungwa wote waliohukumiwa vifungo vya  miaka mitano kushuka chini isipokuwa wale wenye makosa kama mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita, wizi wa kutumia silaha, kumiliki silaha kinyume cha sheria, wizi wa kutumia silaha, ugaidi, ubakaji, na usafirishaji haramu wa binadamu. 

Wafungwa waliopatikana na hatia ya uhalifu mwingine mdogo, wanawake wajawazito au wale walio na watoto gerezani, watoto wadogo, wafungwa wenye magonjwa sugu, wafungwa wenye umri wa miaka 70 na zaidi na wafungwa walio na shida ya akili wanatarajiwa kunufaika na msamaha wa Rais.

"Wale waliopatikana na hatia ya ufisadi au makosa yanayohusiana na ufisadi bila kujali adhabu iliyotolewa, mradi wamelipa pesa za ubadhirifu, uharibifu na riba iliyotangazwa na korti na mahakama watanufaika pia," inasema taarifa hiyo.

Mnamo mwaka jana, Rais Ndayishimiye alitoa msamaha kwa waandishi wa habari wanne waliopatikana na hatia ya kutishia usalama wa nchi.

Walihukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu gerezani na kuachiliwa usiku wa kuamkia Krismasi baada ya kukaa gerezani siku 430.

Wanahabari hao wanne walikamatwa mnamo Oktoba 2019 wakati wakiripoti katika mkoa wa Bubanza juu ya ukosefu wa usalama uliotokea katika mkoa huo. Walishtumiwa kwa majaribio ya kula njama ambayo ilidhoofisha usalama wa ndani wa nchi mashtaka ambayo yalikanushwa na waandishi hao kwa kudai kuwa walikuwa wakifanya kazi yao tu.

Mnamo Juni 2020, korti ilitupilia mbali rufaa yao na walipelekwa katika Gereza la Bubanza kutumikia kifungo chao, lakini walipewa msamaha wa Rais baada ya mwaka.

 

Chanzo: The EastAfrican