Duniani

Bob Marley, miaka 40 tangu afariki bado urithi wake unaishi

Gwiji huyo aliyeiunganisha dunia kupitia muziki wa mahadhi ya raggae alizaliwa Februari 6, 1945 na kufariki Mei 11, 1981

Miaka 40 tangu afariki, mashabiki wa muziki na wapenda amani na umoja wanaendelea kusheherekea maisha ya gwiji wa muziki wa raggae, Bob Marley. Bob Marley alizaliwa Februari 6, 1945 nchini Jamaika. 

 

Marley aliibuka katika muziki mwaka 1963 baada ya kuungana na Peter Tosh and Bunny Wailer kuunda kundi la the Wailers na baadae kutoa  albamu 13 zilizojaa vibao vikali vilivyokubalika duniani kote. 

 

Marley anaendelea kuheshimika kama mwanamuziki aliyehamasisha harakati za kupigania uhuru, amani na umoja kupitia kazi yake ya muziki.

 

Mwaka 1976 alinusurika jaribio la kuuawa nchini kwake Jamaika baada ya kupigwa risasi yeye pamoja na mkewe na timu yake. Inasemekana jaribio hili lilikuwa la kisiasa kutokana na harakati zake za kukosoa wanasiasa nchini Jamaika kupitia muziki wake. 

 

Gwiji huyo aliyeiunganisha dunia kupitia muziki wa mahadhi ya raggae alifariki mwaka 1981 kwa kansa ya ngozi.

 

Unamkumbukaje Bob Marley?