Serikali ya Oman imetoa orodha ya nchi 10 ambazo zimezuliwa kuingia nchini humo chini ya uamuzi wa hivi karibuni uliopitishwa na Kamati Kuu ya kushughulikia janga la corona.Nchi zilizopigwa marufuku ni Tanzania, Afrika Kusini, Lebanon, Sudan, Brazil, Nigeria, Guinea, Ghana, Sierra Leone, na Ethiopia.Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa usiku wa Alhamisi wiki hii na itadumu kwa siku 15Hatua hiyo imetokana na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya udhitibi wa corona nchini humo.Marufuku hiyo pia inawahusisha watu watakaopita katika nchi hizo ndani ya siku 14 kabla ya kuingia Oman ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda raia wao dhidi ya corona.Februari 15, Waziri wa Afya wa Oman alisema nchi yake inafikiria kuzuia safari za ndege kutoka kutoka nchi zinazoonesha kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya corona ikiwa ni baada ya kuthibitisha takwimu za maambukizi ya Corona kwa wasafiri wanaotokea nchini Tanzania kuwa katika kiwango cha juu sana, ambapo asilimia 18 ya wasafiri walikutwa na maambukizi ya virusi hivyo.معاليه يؤكد أن بيانات القادمين من جمهورية تنزانيا للسلطنة سجلت فحوصات إيجابية بنسبة ١٨ بالمائة وهو رقم مرتفع جدا لذلك فإن اللجنة تدرس إيقاف رحلات القادمين من الدول التي ثبت للسلطنة أن لديها نسبة عالية من الإصابات— وكالة الأنباء العمانية (@OmanNewsAgency) February 15, 2021Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Oman, mkutano wa kamati hiyo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman Hammoud bin Faisal Al Busaid.
Watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa majambazi wameshambulia Shule ya Sekondari ya Wasichana inayomiliiwa na serikali ya Nigeria, Jangebe katika mkoa wa Zamfara na kuwateka nyara wasichana 300 wa shule hiyo.Kulingana na ripoti kutoka vyombo vya habari nchini Nigeria watu wenye bunduki walivamia eneo la shule asubuhi na mapema, Ijumaa ya Februari 26Kamanda wa Polisi kanda hiyo bado hajatoa maelezo ya kina kuhusiana na tukio hilo.Tukio la Kutekwa nyara kwa wasichana wa shule ya Zamfara linakuja wiki mbili tu baada ya wanafunzi na waalimu wa Chuo cha Sayansi cha Serikali,Kagara nchini Niger kutekwa nyara.
Rais wa Marekani amefanya mazungumzo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta siku ya Ijumaa na kumhakikishia ushirikiano thabiti wa Marekani na Kenya. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ikulu ya White House, Biden amesisitiza kuendelea kuiunga mkono Kenya katika kusimamia amani ya ukanda huo, ikiwamo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Biden ameupongeza uongozi mzuri wa Kenya katika eneo la Pembe ya Afrika pamoja na juhudi za taifa hilo kupambana na ugaidi, kukuza uchumi, kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi na kusimamia maendeleo endelevu. Rais Biden na Kenyatta pia wamezungumzia hali ya kuporomoka kwa haki za kibinadamu katika eneo lenye mgogoro la Tigray nchini Ethiopia na umuhimu wa kuepuka kupotea zaidi kwa maisha katika eneo hilo na kuhakikisha upatikanaji wa misaada ya kiutu. Vilevile, viongozi hao wamezungumzia ushirikiano zaidi katika masuala ya uthabiti wa kiukanda.
Tukio hilo lina kuja siku nne baada ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) kufanikiwa kuwezesha kutua salama kwa chombo chake cha Perseverance rover katika kreta karibu na ikweta ya sayari hiyo."Picha hizi ni matokeo ya ndoto zetu," Al Chen, Kiongozi aliyeongoza kutua kwa chombo hicho alisema.Now that you’ve seen Mars, hear it. Grab some headphones and listen to the first sounds captured by one of my microphones. 🎧https://t.co/JswvAWC2IP#CountdownToMars— NASA's Perseverance Mars Rover (@NASAPersevere) February 22, 2021Picha kutoka kwa kamera zenye kiwango cha juu zilianza kuchukua maili saba kutoka juu ya uso wa Mars, ikionyesha kuyumba kwa nguvu kwa parachute ikifuatiwa chombo cha perverence rover kugusa kwenye kreta.Kipaza sauti kutoka kwenye chombo hicho pia kimetoa rekodi ya kwanza ya sauti kutoka katika sayari hiyo.Picha moja ya kustaajabisha ilionesha kutawanyika kwa miamba yenye giza ikiwa miepesi na yenye mashimo. "Tunatumia maneno haya ya jumla katika hatua hii ya awali mpaka tutakapopata na data zaidi ambayo inatuwezesha kupima nadharia zetu na kutoa tafsiri zenye ujasiri zaidi," alisema Ken Williford, kiongozi wa mpango huo Kwa jumla, timu ilisema wamepokea zaidi ya gigabytes 30 za habari, na zaidi ya picha 23,000 za asili ya vyombo vya moto vilivyotua."Najua umekuwa mwaka mgumu kwa kila mtu na tunatumai kuwa labda picha hizi ... zitawafurahisha watu," alisema Justin Maki, mwanasayansi wa picha.Chombo hicho chenye magurudumu 6 sasa kitakuwa kwenye sayari hiyo kwa takriban miaka miwili katika mabonde ya eneo hilo, kikitafuta ushahidi unaonesha shughuli za maisha ya awali.Ikweta ya Jezero inadhaniwa kwamba imekuwa na ziwa kubwa kwa miaka bilioni kadhaa iliyopita.Na mahali ambapo kumekuwa na maji, kuna uwezekano mkubwa kulikuwa na maisha yalioendelea eneo hilo.
Serikali imesema kuwa haitatoa takwimu za maambukizi ya virusi vya corona kwani kufanya hivyo ni kuongeza hofu kwa wananchi hali itakayopunguza kinga za miili yao na kupelekea kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa huo Akizungumza na waandishi wa habari Naibu waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa matumizi ya data za magonjwa yote ni kwa ajili ya kuchakata na kisha kuja na mbinu za kisayansi kukabiliana na magonjwa hayo lakini sio swala la kutaka kila wiki Waziri wa Afya aelezale waliofariki na wagonjwa, kwani kufanya hivyo ni kuwatisha wananchi. “Wanasema Tanzania haitoi data, matumizi ya data za magonjwa yote, ni kwa ajili ya kuchakata na kisha kuja na mbinu za kisayansi kukabiliana na magonjwa hayo lakini sio swala la kutaka kila siku Waziri wa Afya aelezale kwenye TV waliofariki, wagonjwa, waliozikwa ni ujinga mtupu, unatishia taifa na kufanya lisitulie,” amesema Dk. Mollel.Katika hatua nyingine Dkt Mollel amewataka Watanzania kuondoa hofu dhidi ya Virusi vya corona kwani hata nchi zilizochukua hatua kubwa za kupambana na virusi hivyo ndizo zimeonekana kuwa na idadi kubwa ya maambukizi.“Hivi ni nchi gani inaweza kuchukua hatua zaidi na bora za kujikinga zaidi ya Marekani, Uingereza, au nchi zilizoendelea. Leo tunavyozungumza hivi kati ya Marekani na sisi, ni wapi wameumia zaidi na ugonjwa wa COVID-1?” amehoji Dkt Mollel. Kauli hii imekuja wakati ambapo shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa likitoa wito kwa mamlaka nchini. kuanza kutoa takwimu za watu waliambukizwa ugonjwa wa COVID-19, kuhimiza matumizi ya njia za tahadhari zinazotolewa na shirika hilo pamoja na kujiandaa kupokea chanjo dhidi ya COVID 19.Katika taarifa yake ya February 20 mwaka huu, kuhusu mwenendo wa COVID-19 nchini Tanzania, shirika la Afya Duniani (WHO) lilielelezea wasi wasiwasi wake kuhusu idadi ya wasafiri wa Tanzania waliopatikana na kuwa na virusi vya corona Hata hivyo serikali imekuwa ikihimiza zaidi watu kuendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na wizara ya Afya nchini dhidi ya maambukizi ya Virusi vya corona ikiwa ni pamoja na kumuomba Mungu na kutumia tiba asili.
Serikali nchini Tanzania imetangaza kuanza kutumia ndege kunyunyizia dawa makundi ya nzige yaliyovamia wilaya ya Longido na Simanjiro wakitokea nchini Kenya.Taarifa za kuingia kwa makundi hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa na mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaibambe ambaye amesema ndege ya Shirika la Chakula Duniani FAO inayotokea Nairobi inatarajia kuanza kazi ya kunyunyuzia dawa leo. “Kuanzia kesho (22.02.2021) ndege maalum itaanza kazi kupulizia sumu kuua nzige waliovamia maeneo ya Longido na Simanjiro ili wasiendelee kusambaa na kusababisha maafa” alisema Waziri wa KIlimo, Prof. MkendaWaziri Mkenda amesema tayari wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu (TPRI) wapo wilayani Longido na Simanjiro wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Efrem Njau kwa kazi ya kudhibiti wadudu hao waharibifu wa mazao ya kilimo.Aidha ametoa wito kwa wananchi kutookota wala kula nzige watakaokuwa wameuwawa na viuatilifu (sumu) kwenye maeneo yote ambapo ndege hiyo itapita kuua nzige kwani viuatilifu hivyo vinaweza kuwa na madhara kwa binadamu.Pia, ameagiza wataalam wa kilimo na watendaji wa vijiji na kata kutoa taarifa kwa wananchi juu ya uwepo wa kazi ya kuua nzige hivyo wasiwe na hofu watakapoona ndege inaruka chini kwenye maeneo.“Wananchi wakiona nzige wameanguka chini wamekufa wasiwachukue au kula kwa kuwa wengi watakuwa wamekufa kwa sumu” alisisitiza Prof. MkendaWaziri huyo wa kilimo amesisitiza kuwa serikali itahakikisha mazao ya wakulima na malisho ya mifugo hayaharibiwi na nzige ndio maana ametembelea eneo hilo la Longido ambapo amebainisha mafanikio ya kuwadhibiti tangu walipoingia nchini mwezi Januari mwaka huu kwenye baadhi ya maeneo.Hata hivyo, mpaka sasa hakuna na madhara yoyote yaliyoripotiwa kusababishwa na nzige hao kwani eneo lililovamiwa kwa kiasi kikubwa ni pori lakini pia asilimia kubwa ya nzige hao bado ni wadogo.Mwaka jana makundi makubwa ya nzige yalivamia maeneo kadhaa nchini Kenya na Ethiopia na kuibua hofu ya kutokea kwa baa la njaa kutokana uharibifu mkubwa walioufanya.
Taarifa kutoka kwa Huduma ya Wanyamapori Kenya (KWS) ilithibitisha kutokea kwa tukio hilo la twiga wawili 'kupigwa shoti' ambalo lilitokea katika Hifadhi ya Soysambu huko Nakuru mwishoni mwa wiki na kulitaka Shirika la Umeme kubadilisha nguzo ndani ya eneo hilo ili kuzuia vifo vya twiga ambao urefu wao umezidi nguzo zilizopo kwa sasa. Baadhi ya Wakenya wametumia mtandao wa kijamii wa Twitter siku ya Jumapili kuelezea hasira zao baada ya picha za twiga hao waliopigwa shoti hadi kufa kusambaa. Wengine walihoji ni kwanini Shirika la Umeme Kenya halijashughulikia suala la ufupi wa nguzo za nyaya licha ya malalamiko kadhaa kwa miaka miwili iliyopita wakati wengine walikosoa upuuzaji wa spishi za wanyama walio hatarini kama vile twiga wa Rothschild. KWS imesema maafisa wa shirika la umeme la Kenya, wataweka vigingi vinginevya umeme. "Ripoti ya awali inaashiria urefu wa vigingi vya umeme kupitia hifadhi ya Soysambuvi uko chini, kuliko urefu wa twiga," sehemu ya taarifa ilisema. Mhifadhi wa Wanyama, Bi Kahumbu alisema vifo vya wanyama hao vingezuiliwa ikiwa ushauri wa wataalamu ungezingatiwa. "Nyaya hizi za umeme zimekuwa zikiwaua twiga na wanyama wengine.Tathmini ya kuchunguza hatari kabla ya mradi kuidhinishwa inafanywa kiholela. Inasikitisha kwamba hadi hali kama hii itokee ndio hatua ichukuliwe!" aliandika kwenye Twitter yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amesema kuwa serikali haijakataza matumizi ya barakoa katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona bali Watanzania wachukue tahadhari kwa kutumia barokoa zinazotengezwa nchini ikiwemo zile zilizotengenezwa na Bodi ya Dawa (MSD) kwa kuwa barakoa zinazoagizwa kutoka nchi za nje zina mashaka ya kuwa sio salama.Akizungumza hii leo katika Manisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuchukua tahadhari ya virusi vya corona hususani matumizi ya njia za asili ikiwa ni pamoja na kujifukiza katika kukabiliana na janga hilo.“Serikali haijazuia barakoa, lakini tuwe waangalifu katika kuchagua barakoa ipi nina vaa, tutaangamia msifikiri tunapendwa mno vita ya kiuchumi ni mbaya, na ndio maana nawapongeza waliovaa barakoa walizojitengenezea wao,” amesema Rais Magufuli Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kumtanguliza Mungu katika mapambano dhidi ya COVID-19, kwani njia za kibinadamu ikiwemo uvaaji wa barakoa, kutokugusana au kukabiliana, pamoja na kujifungia majumbani (lockdown) hazijasaidia kupambana na janga hilo kwani nchi nyingi zilizochukua hatua hizo bado zinaongoza kwa maambukizi ukilinganisha na Tanzania ambayo haikuchukua hatua hizo hapo awali. “Ndugu zangu nchi nyingi zimeanza kuvaa barakoa, ninyi ni mashahidi katika vyombo vya habari nchi hizo ndizo zinaoongoza kwa watu wengi kufa wengi maelfu sijasema msivae barakoa na wala msini koti vibaya lakini kuna barakoa nyingine sio nzuri”amesema Magufuli.
Umewahi kujiuliza kwanini takribani supermarket zote zina mpangilio unaofanana? Hii sio bahati mbaya. Ni matokeo ya majaribio ya ujanja wa kisaikolojia katika jitihada za kumrubuni mteja ili afanye manunuzi. Baadhi ya mitego wanayotumia ni;1.Hukuchanganya na Wingi wa VituWanauchumi na viongozi wa biashara wanatuambia kuwa chaguo zaidi moja ni sahihi. Lakini ukweli ni kwamba kama ungekuwa na uwezo wa kupata kila unachokitaka ulimwenguni basi ungekuwa na wakati mgumu. Kwa nini? Kwa sababu, kulingana na tafiti, machaguo yasiyo na kikomo hufungua mlango wa majuto, mashaka na kutoridhikaWakati tunakabiliwa na chaguzi nyingi sana, hatuwezi kushughulikia. Kwa hivyo tunaishia kunyakua chochote, au kununua zaidi na kulipa zaidi.Unakuta ‘Supermarket’ ndogo ina wastani wa vitu 6000 vya kuchagua hivyo nafasi ya kuchanganyikiwa ni kubwa kama huwezi kufanya maamuzi sahihi. 2. Akili Yako Hulemewa‘Supermaket’ hutaka kuvutia hisia za kila mtu anayeingia kufanya manunuzi. Mfano:- Huweka Taa kali,rangi zinazong’aaBidhaa mpya zikionekana wazi na vioo vinavyokuwezesha kuona watu wakiwa kazini- waokaji, wauzaji ‘icecream’ kuvutia macho yako.- Bidhaa zote zinaonyeshwa ili zikuvutie na uweze kuzigusa.-Maua safi hunukia puani mwako pindi unapokanyaga mlango wa kuingilia. Keki safi za kuoka, harufu ya icecream vyote hivi hulenga kumvutia mteja.-Sampuli za bure hupatikana kila wakati,na zinahimizwa na wafanyakazi ili uangukie katika mtego wa ladha.3. Hucheza na BeiHii pia ni mbinu ambayo utumika kumrubuni mteja pindi aingiapo supermarket. Mfano unaweza kuwekewa bei ya awali na sasa ambapo mara nyingi huwa ni punguzo hivyo ukakurupuka kununua kuogopa bei ya juu pindi utakaporejea tena.4. Hukutembeza Ndani ya DukaSio bahati mbaya kwamba karibu Supermarket zote huwa na muonekano unaofanana kwa ndani na huwa na wafanyakazi ambao wapo tayari kukuzungusha ndani ya duka kuhakikisha unapata unachohitaji bila kukata tamaa. Mpangilio huo ni sehemu ya mikakati ya kisasa ya kisaikolojia ya kukushawishi kutumia pesa zaidi. Kumbuka sio lazima uangukie kwenye mitego ambayo Supermarkets hufanya. Unaweza kupata kile unachotaka kutoka duka na ukaepuka ujanja wa kisaikolojia ambao umeundwa kumaliza pesa zako kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kufanya manunuzi huku ukizingatia bajeti uliyokuwa umeiandikia, kufanya m,anunuzi kwa msimu n.k
Katika utafiti uliochapishwa na Royal Society of Open Science, Marekani ulichunguza mbwa 18 na kurekodi milio yao kwa kujibu hali katika muktadha tofauti tofauti.Wakati tafiti zingine zimeonyesha kuwa binadamu wanaweza kuelewa mlio wa mbwa, utafiti huo ulikuwa wa aina yake katika kuzingatia milio.Watu arobaini waliulizwa kutambua kila kilio kilimaanisha nini, yaani, woga, uchokozi, furaha, kukata tamaa, au michezo. Asilimia 63 ya washiriki waliweza kutambua kwa usahihi ni kwa nini mbwa alikuwa akibweka. Kati ya asilimia 63 hiyo, wanawake walifanya vizuri zaidi kuliko wanaume, na kama inavyotarajiwa, wale wanaoishi na mbwa majumbani walifanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawana. Kwa nini wanawake walifanya vizuri?Utafiti ulionesha kuwa wanawake wana huruma na hisia kuliko wanaume. Kulingana na tafiti hiyo, wanawake wanaweza huwa na huruma zaidi na wenye hisia kali kwa wengine na hii inawasaidia kuhusisha zaidi muktadha huohuo pindi wanapokuwa karibu na mbwa. Utafiti huu sio wa kwanza kuthibitisha kuwa mbwa anaweza kuwa rafiki bora wa wanawake. Mnamo Disemba, utafiti mwingine uliohusisha washiriki 1,000 kutoka Marekani uligundua kwamba wanawake hulala vizuri karibu na mbwa kuliko watu wengine. Kulingana na utafiti huo, iligundulika kuwa mara nyingi mbwa hakatizi usingizi wa mtu tofauti ukilala karibu na mtu na pia huwapa binadamu hisia za faraja na usalama tofauti na pindi ukilala na mwenza wako.Inasemekana hapo awali kipindi mbwa walianza kuishi na binadamu ni wanawake ambao walianza kuwapa mbwa majina, kuwaacha walale ndani ya nyumba, na waliomboleza walipokufa. Wanaume wanaweza kuwa wamefuga mbwa kwa ajili ya Ulinzi, lakini ni wanawake ambao waliwaonyesha upendo na huruma.
Shirika la habari la nchini Marekani CNN limemtaja kama Pep Gardiola wa mpira wa Afrika kwenye makala inayoelezea mchezo wa nusu fainali wa Mabigwa wa vilabu Duniani kati ya Al Ahly kutoka nchini Misri dhidi ya Bayern Munich ya huko nchini Ujerumani Kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane amekuwa na mvuto kwa makocha wengi barani Afrika kutokana na uwezo wake aliouonyesha kupitia klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika ya Kusini, timu ya taifa ya Afrika ya kusini (Bafana Bafana) kati ya mechi 23 alizoiongoza klabu ya Al Ahly ameshinda mechi 18, ametoka sare mechi 5 na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Bayern Munich. Mbali na Matokeo hayo kocha huyo amesema kuwa klabu ya Simba ni klabu bora na iliyojengeka kwasasa. Akizungumza baada ya kuwasili nchini Tanzania, Kocha huyo amesema kuwa mchezo huo utakua ni mgumu kutokana uimara wa timu zote mbili."Tutazungumza zaidi wakati wa mkutano na waandishi wa habari, lakini utakua ni mchezo mgumu Simba walitufunga wakati uliopita na tunakwenda kufanya marekebisho," amesema Pitso Mosimane.Klabu ya Al Ahly ambao wameshinda mchezo wao wa kwanza, dhidi ya El Mellerk watakua ugenini siku ya Jumanne wakicheza na wenyeji wao klabu ya Simba ambao nao wametoka kushinda katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ac Vita. Klabu ya Simba imeshinda michezo mitatu ya klabu bingwa kati ya mitano iliyocheza.Hata hivyo klabu ya Simba imesema kuwa imejipanga kuhakikisha kuwa inapata ushindi katika mchezo huo ambapo baada ya kauli mbiu ya ‘War in Dar’ kufanikiwa kuwaongoza Simba kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya FC Platnum ya Zimbabwe na kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu hiyo kupitia kwa Ofisa habari wake Haji Manara sasa imetangaza kauli mbiu ya Total War ili itumike kuwapa nguvu wanasimba wote kuelekea mchezo huo. “Hii ni sawa na mtu kuwa porini halafu akutane na Chui, lazima apambane bila kukata tamaa vinginevyo atauliwa, hiyo ndio maana halisi ya kauli mbiu yetu hiyo ambayo itawafanya wachezaji waingie uwanjani wakiamini kuwa hakuna nafasi nyingine zaidi ya kushinda,” amesema Manara.Klabu ya Al Ahly ndio vinara wa Kundi A, huku klabu ya Simba ikishika nafasi ya pili na kufuatiwa na AS Vita na El Merekh ambao mpaka sasa bado hawajavuna alama hata moja. Mbali na ubora wa klabu ya Al Ahly mchambuzi wa masuala ya michezo nchini Gharib Mzinga anaamini kuwa Simba sio klabu ya kudharaulika kwa sasa katika michuano ya kimataifa. "Lakini huwezi kuidharau Simba Sports Club, Simba imeimarika sana sana na faida kwao ni ile mentality ya wachezaji na benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki kwamba katika uwanja wao wa nyumbani ndio sehemu ya kukusanya alama tatu" anasema Mzinga.Mchezo wa Simba dhidi ya Ahly utakua wapili kwao kwenye michuano hiyo hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini DR Congo dhidi ya AS Vita.
Mkutano wa usalama wa Munich ulifanyika kwa njia ya video hapo jana, Februari 19 ukihusisha washirika kutoka mataifa 7 tajiri zaidi duniani.Rais Joe Biden katika hotuba yake kwenye mkutano wa Munich wa masuala ya usalama uliofanyika kwa njia ya video, ameahidi kwamba Marekani itashirikiana na washirika wake wa Ulaya katika juhudi za kukabiliana na changamoto zilizopo, ikiwa pamoja na janga la maambukizi ya corona, ugaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo wa Munich wa masuala ya usalama hufanyika kwenye mji huo wa Ujerumani kila mwakaMkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenyekiti wa zamu, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson. Washiriki wengine walikuwa, Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus.Yaliyojiri katika mkutano huo:1. 1. Biden ametangaza Mwisho wa mtindo diplomasia wa Trump 'Marekani Kwanza' "Marekani imerudi, muungano kati yake na nchi za bara la Ulaya umerudi," Bwana Biden alitangaza. Akijaribu kufutilia mbali miaka minne iliyopita bila hata kumtaja mtangulizi wake, Donald J. Trump, Bwana Biden alisema "hatutazami nyuma."Pia ameonesha nia yake ya kutaka kutetea na kuilinda demokrasia ya nchi yake na kudai kuwa hiyo ndiyo dhamira yake kubwa na kwamba demokrasia haitokei kwa bahati mbaya lazima itetewe, iimarishwe, ilindwe na iendane na mabadiliko ya sasa.Lakini pia ameishinikiza Ulaya kufikiria namna ya kutatua changamoto kwa njia mpya - ambayo inatofautiana na ile ya Vita Baridi ingawa wapinzani wao wawili (china na Urusi) wanajulikana toka kipindi hicho."Lazima tujiandae pamoja kwa ushindani wa kimkakati wa muda mrefu na nchi ya China," alisema, akitaja "Cyberspace, ujasusi bandia na bioteknolojia" kama mambo muhimu katika ushindani. Nchi za magharibi lazima ziweke sheria za jinsi teknolojia hizi zinatumiwa, alisema, badala ya kuiachia Beijing pekee katika kufanya maamuzi. 2. Viongozi wa Ulimwengu Wapanga Mkakati Mpya Baada Utawala wa Bw.TrumpAkiongea katika video Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aliitisha wito kwa viongozi wa Kundi la mataifa 7 Ijumaa alasiri, kushinikiza ushirikiano zaidi na uratibu wa kusambaza chanjo za virusi vya corona kwa mabilioni ya watu katika nchi zinazoendelea. Katika wito huo, Waziri Johnson aliahidi kwamba Uingereza itatoa misaada ya ziada ya chanjo kwa mpango ambao utasambaza dozi katika nchi zinazoendelea. Bwana Biden pia alithibitisha kuwa Marekani itatoa dola bilioni 4 kuunga mkono juhudi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili. 3. Merkel ataka mkakati wa pamoja katika kushughulikia China na UrusiKansela wa Ujerumani, Angela Merkel alitoa wito kwa Marekani na Ulaya kutafuta njia ya pamoja ya kushughulika na China na Urusi, akiongeza kuwa hakuwa na "wasiwasi wowote" unaoashiria kupendelewa kwa maslahi ya upande wowote wanchi za Atlantiki. Alitaka Ulaya na Marekani ziwiane katika kushughulika na Urusi na China, suala ambalo alisema linaweza kuwa kgumu ukizangatia China ni mshindani na mshirika muhimu kwa Magharibi."Katika miaka ya hivi karibuni, China imepata nguvu ya ulimwengu, na sisi kama washirika na wanademokrasia, lazima tufanye kitu kukabiliana na hii," Bi Merkel alisema, akisisitiza ahadi za Ujerumani na Marekani katika kusambaza chanjo katika nchi zinazoendelea ambapo amesema nchi yake itaongeza Euro bilioni 1.5.4. Kiongozi wa Ufaransa anasema ushawishi wa Marekani duniani unapaswa kukubaliana na hali halisiAkiongea kwa katika video baada ya Rais Biden kuhutubia ujumbe wa "Marekani imerudi" kwa mkutano huo, Bwana Macron aliweka wazi kuwa Marekani sasa inapaswa ikubaliane na ukweli kwamba ile dhana ya kutawala Ulimwengu sasa imepitwa na wakati na Ulaya inapaswa "kujisimamia zaidi katika usalama wake."Kwa vitendo, itachukua miaka mingi kwa Ulaya kuimalisha jeshi la ulinzi ambalo litafanya Marekani iweze kujitegemea zaidi. Lakini Bwana Macron ameazimia kuanza sasa akiwa ameazimia kuongeza uwezo wa kiteknolojia wa Jumuiya ya Ulaya ili ipunguze kutegemea Marekani au China.Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia amesisitiza umuhimu wa nchi masikini kupatiwa chanjo na kwa ajili hiyo amependekeza kwa Umaoja wa Ulaya na Marekani, mpango wa kupeleka dozi milioni 13 barani Afrika ili kwanza kuwapatia chanjo wahudumu wa afya wapatao milioni milioni 6.5. 5. Marekani inajiunga rasmi na makubaliano ya hali ya hewa ya ParisMakubaliano hayo ya kimataifa yaliundwa kuzuia janga la joto duniani. Rais Biden amesema kukabiliana na shida ya hali ya hewa ni miongoni mwa vipaumbele vyake vya juu na alitia saini mkataba saa chache tu baada ya kuapishwa katika ofisi mwezi uliopita."Hatuwezi kuchelewesha tena au kupuuza kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa," Bwana Biden alisema. "Huu ni mgogoro wa ulimwengu, uliopo. Na sote tutapata matokeo ikiwa tutashindwa. "6. Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anataka Marekani ijiunge na juhudi za kuratibu makampuni makubwa ya mtandaoKuratibu nguvu za kampuni kubwa za teknolojia itakuwa "hatua muhimu" katika kukomesha vurugu za kisiasa, alisisitiza, akiongeza: "Tunataka muongozo ulio wazi kwamba makampuni ya mtandao yanawajibika kwa maudhui yanayosambazwa, na wanayounga mkono."Maamuzi juu ya maudhui hayapaswi kuachwa kwa “programu za kompyuta”. alisema. Lazima zifanywe na wabunge waliochaguliwa kidemokrasia, hoja ambayo Ufaransa imekuwa ikitoa mara kwa mara.Katika kuunga mkono juhudi za kusaidia nchi zinazoendelea katika kusambaziwa chanjo,Kwa upande wake Bi. von der Leyen alisema Halmashauri ya Umoja wa Ulaya nayo itaongeza mchango wake kutoka Euro milioni 500 hadi Euro bilioni 1.5.7. Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni aonya kuhusu athari za usambazaji wa chanjo usio na uwianoDaktari Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi mkuu wa WHO, Ijumaa alihimiza nchi na watengenezaji wa dawa kusaidia kuharakisha utengenezaji na usambazaji wa chanjo kote ulimwenguni, akionya kuwa ulimwengu unaweza kupata athari kubwa ikiwa nchi zingine zitaendelea na kampeni zao za kujilimbikizia chanjo na kuwaacha wengine nyuma."Usawa katika chanjo sio kitu sahihi tu, lakini pia ni busara zaidi kufanya," Dk Tedros alisema katika Mkutano wa Usalama uliofanika Munich, akisema kwamba kadri inavyochukua muda mrefu kutoa chanjo kwa watu katika kila nchi, ndivyo janga hilo litakaa kinyume na udhibiti.Nchi tajiri zimekuwa zikikosolewa kwa wingi katika wiki za hivi karibuni juu ya kujilimbikizia chanjo na kusahau nchi zenye kipato cha chini na cha kati. G7, ambayo inaundwa na Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Amerika, na EU, ndio jukwaa pekee ambalo jamii zenye ushawishi mkubwa ulimwenguni na uchumi wa hali ya juu huletwa pamoja kwa mazungumzo ya karibu. Matarajio ya Johnson ni kutumia G7 kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama. Kwa kuzingatia hilo, Bw.Johnson alialika viongozi kutoka Australia, India, na Korea Kusini kuhudhuria kama wageni ili kukuza utaalam na uzoefu. Mataifa haya, pamoja na yale katika G7, yanawakilisha watu bilioni 2.2 na zaidi ya nusu ya uchumi wa ulimwengu. Makubaliano ya usalama kati yao yatakuwa na athari kubwa zaidi ulimwenguni, kuonyesha jinsi mataifa yanavyoshirikiana kuwafanya raia wao kuwa salama na wenye mafanikio zaidi.
Kunyemelewa na watani zao wa Jadi Klabu ya simba katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara ndio mzimu unaoutesa Klabu ya Yanga kwa hivi sasa wakati ambapo baadhi ya mashabiki wameonekana kuutupia lawama uongozi wa klabu hiyo kwa kutochukua hatua za mapema kuzuia Janga hilo.Matokeo ya sare katika mechi mbili mfululizo walizozipata Yanga katika michezo yao ya Ligi Kuu Bara yamewaibua viongozi wa timu hiyo ambao wamezitupia lawama mamlaka za soka nchini wakidai kuwa zinahusika moja kwa moja na upatikanaji wa matokeo hayo Akizungumzia shutma hizo katika mkutano na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema, kwa sasa timu yao haitendewi haki na mamlaka zote zinazosimamia soka, kama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kamati ya Waamuzi pamoja na Kamati ya saa 72.Mwakalebela amelalamikia matukio yaliyojitokeza katika mchezo wa Klabu hiyo dhidi ya Mbeya City na kudai kuwa walinyimwa penati mbili za wazi ambazo walistaili kuzipata na zingepelekea wao kushinda mchezo huo na sio kupata pointi moja.Mwakalebela pia amelalamikia mchezo wa timu huyo dhidi ya Kagera sugar akidai kuwa walinyimwa penati ambazo zingewafanya kupata pointi tatu badala ya kupata moja, huku akidai kuwa mamlaka husika kuna timu inayoandaliwa kuwa bingwa."Kama kuna bingwa kaandaliwa basi apewe kombe tujue moja, tunatarajia kamati husika zitatoa maamuzi katika hizo mechi zetu mbili na hao waamuzi wachukuliwe hatua stahiki tusitolewe kwenye mstari wetu wa kutwaa ubingwa msimu huu," amesisitiza Mwakalebela.Mwakalebela amesema, Yanga wametumia gharama kubwa kuiandaa timu hiyo hivyo namna matukio yanayotokea na kufumbiwa macho na vyombo husika yanawafanya kutafsiri vibaya juu yao.Hatahivyo baadhi ya wafuatilizi wa masuala ya soka nchini wanasema kuwa ni haki ya msingi kwa vilabu kuhoji ubora wa uendeshwaji wa ligi kuu pale inapohitajika lakini lazima malalamiko hayo yawe na mantiki na uhalisia. Gharib Mzinga mchambuzi wa masuala ya soka nchini anasema kuwa mwamuzi kuchezesha chini ya kiwango ni suala ambalo hutokea katika mchezo na waamuzi huadhibiwa kupitia kamati husika ya waamuziKimsingi suala la performance ya waamuzi kuwa ndogo ni suala la kitaifa hilo sote tunalifahamu, lakini isionekane tu ni upande mmoja wao ndio wanaonewa peke yao hapana" amesema Mzinga. Yanga ambao kwasasa ni vinara katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara wanatàrajiwa kuingia Dimbani leo kuzisaka pointi tatu nyingine dhidi ya klabu ya Mtibwa sugar kutoka Mkoani Mororgoro.
Rais Dkt John Magufuli amewaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kuaga mwili wa Katibu Mkuu Kiongozi balozi John Kijazi Shughuli za ibada na kuaga mwili huo zimefanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais mstaafu Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu pamoja na Makamu wa Rais. Akizungumza kwenye shughuli hiyo, Rais Magufuli amesema marehemu Balozi Kijazi alikuwa mchapakazi aliyeipenda kwa dhati nchi yake na alikuwa anaheshimu kila mtu bila kujali umri au cheo chake. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewataka Watanzania wasitishike na ugonjwa wa corona na badala yake waendelee kuchukua tahadhari na kumwomba Mungu. "Magonjwa yapo na yataendelea kuwepo Magonjwa ya vifua ya kupumua na kadhalika yatakuwepo hayakuanzia hapa zipo nchi zimepoteza watu wake wengi sisi Tanzania Mungu ametusaidia sana katika kipindi cha mwaka uliopita," amesema Magufuli. Amesema ugonjwa wa corona unaweza kuepukika kwa kuchukua tahadhari na kumwomba Mungu na kuwaomba viongozi wa dini zote kuandaa maombi kwa ajili ya janga hilo na kusisitiza kuwa nchi ya Tanzania haita chukua hatua za kuwafungia watu wake ndani yaani Lockdown kwasababu ya virusi hivyo. SOMA: - Mfahamu Marehemu Balozi Kijazi Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kukemea uenezaji wa taarifa za uongo kuhusu corona ikiwemo ile iliyodai kuwa waziri wa Fedha Dkt Philip Mpango amefariki dunia kwa maradhi ya corona. “Leo nimetumiwa ujumbe na waziri wa fedha Dkt Mpango ambaye amelazwa Dodoma na ninaomba noisome hapa kwa faida ya wale waliokuwa wanatweet Amenitumia leo asubuhi, ameniambia ‘Mheshimiwa Rais, asante sana nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa neema ya Mungu naendelea vizuri, ninakula, ninafanya mazoezi ya kifua na kutembea. Hao wanaonizushia kifo kwenye mitandao niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana. Mheshimiwa Rais, Mungu akubariki na akupe neema na ujasiri zaidi, katika kuliongoza taifa letu katika wimbi hili. Naungana nawe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu, Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Rest In Peace. Waziri Mpango’ Ni huyo ambaye aliambiwa jana amekufa,” alisema Rais Magufuli. Mazishi ya Balozi Kijazi ambaye amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma, yanatarajia kufanyika Februari 20 wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi leo amewaongoza waombolezaji wakiwemo viongozi na wananchi kwenye mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.Mazishi ya Maalim Seif ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo yamefanyika kijijini kwake Mtambwe katika wilaya ya Wete visiwani PembaKabla ya mazishi hayo, mwili wa marehemu maalim Seif uliswalia kwenye uwanja wa Gombani na kabla ya hapo pia katika msikiti wa Maamur jijini Dar es salaam pamoja na viwanja vya Mnazi Mmoja mjini Unguja.Katika mahali ambapo mwili huo ulipita, maelefu ya waombolezaji walijipanga barabarani na kwenye viwanja ambavyo kulikuwa na swala ili kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye ametajwa kama nguzo muhimu ya umoja na mshikamano wa kitaifa. Akitoa salamu za chama, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amesema maalim Seif aliyaishi yale yote aliyoamini na kuwaasa viongozi wengine na vijana kuiga mfano wake na kuahidi kwamba chama cha Act kitayatimiza maono yake na kutoa ushirikiano unaohitajika kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.“Wengi mnafahamu kwamba mimi si mtu wa kukosa maneno, lakini leo nakosa maneno ya kumwelezea Mwenyekiti wangu Maalim Seif Sharif Hamad - nakosa maneno kwasababu Maalim mwenyewe ni maneno,” amesema Zitto.Chama cha ACT Wazalendo kitakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa kinampata Mrithi Maalim Seif ndani ya kipindi wiki mbili.Wengi mnafahamu kwamba mimi si mtu wa kukosa maneno, lakini leo nakosa maneno ya kumwelezea Mwenyekiti wangu, nakosa maneno kwasababu Maalim mwenyewe ni maneno- Zitto KabweFaraj Faridhi ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa ambapo anasema kuwa kuna ugumu wa kuliziba pengo la Maalim Seif katika siasa za upinzani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuthamini utu na haki za watu. “Maalim Seif Sharif Hamad ikumbukwe alikua na misimamo ya kutaka utu wa mtu usipotee au haki ya mtu isipotee, lakini katika siasa za Zanzibar, tumeona tangu mwaka 1995 kwa chaguzi zote mpaka 2020 kulikua hakuna mgombea wa upinzani mwenye nguvu wa kumfikia Maalim Seif na pia ikumbukwe siasa za Zanzibar ni mtu na mtu mwenyewe ni Maalim Seif Sharif Hamad,” amesema FaridhiMaalim Seif amefariki dunia Februari 17 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa tangu Februari 9 kwa matibabu.
Mkurugenzi mkuu wa ligi kuu Uingereza, Richard Masters anaamini mashabiki wanaweza kurejea viwanjani kushabikia timu zao kabla ya msimu huu wa 2020/21 kuisha.Mechi zote za ligi nchini humo zinachezwa bila mashabiki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.Utaratibu wa kuruhusu mashabiki angalau elfu mbili viwanjani uliwekwa baada ya serekali ya Uingereza kuigawa miji kutokana na ngazi na hali ya mlipuko wa COVID-19. Utaratibu huu ulisitishwa ghafla baada ya visa vingi kuripotiwa nchini humo hali iliyopelekea nchi hiyo kuweka tena marufuku ya kutoka nje.Katika mahojiano yake na gazeti la Financial Times Bwana Masters alisema "Nina imani mashabiki watarejea viwanjani""Hakuna mtu anayeweza kutabiri kwasababu hili janga (COVID-19) lina namna nyingi za kukushangaza, ila sisi hatujapoteza matumaini na tunaweza kuona mashabiki kadhaa viwanjani msimu huu"- Richard Masters"Natumaini msimu ujao utaanza haraka na tutaona pia mashabiki katika idadi kamili kama zamani na hapo tutakua tumerejea katika uhalisia wa ligi kuu Uingereza ( Premier League)" Masters aliongeza.(Richard Masters:Mkurugenzi mkuu wa ligi kuu Uingereza)Kwa sasa mechi zote za ligi kuu zinaonyeshwa kupitia vituo mbalimbali vya television ikiwa ni mpango unaofahamika kama 'Project Restart' tangu ligi hiyo iliporejea tena June 2020 na utaratibu huu utadumu hadi mashabiki watakapo rejea viwanjani. Mashabiki wamekosekana viwanjani kwa kiasi kikubwa tangu ligi hiyo iliporejea mwezi June 2020.Mwezi Oktoba 2020 baadhi ya mechi zilishuhudiwa na mashabiki wasiopungua elfu mbili lakini baadae utaratibu huo ulifutiliwa mbali baada ya nchi hiyo kuweka marufuku kutoka nje kwa mara ya pili. Kwa sasa Uingereza ipo katika marufuku ya tatu ya kutoka nje kutokana na COVID-19, Waziri Mkuu Boris Johnson atatoa kanuni mpya za kukabiliana na janga hilo siku ya Jumatatu tarehe 22 mwezi huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, Balozi Mhandisi John William Herbert Kijazi amefariki Februari 17 majira ya saa tatu na dakika kumi usiku katika hosptali ya Benjamin Mkapa akiwa anapatiwa matibabu.Taarifa huyo inaeleza kuwa taratibu za mazishi ya Kiongozi huyo zitatangazwa hapo baadae. Lakini Balozi John William Kijazi ni Nani?Amekuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 - 2016 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.Kati ya mwaka 1996 hadi 2002, Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamizi wa Ujenzi wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.Balozi Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka 1992.Balozi Mhandisi John Kijazi amefariki akiwa ameacha mke, Fransisca Kijazi pamoja na watoto watatu, David, Emmanuel na Richard Kijazi.
Kyenge aliteuliwa na Rais Felix Tshisekedi Jumatatu ya Januari 15 ikiwa ni zaidi ya wiki mbili tangu Waziri Mkuu wa zamani Sylvestre Ilunga ajiuzulu kufuatia kura ya kutokuwa na imani naye kufanyika bungeni mwishoni mwa Januari.Baada ya uteuzi huo Sama Lukonde aliwaambia waandishi habari kwamba kurejesha hali ya usalama ndiyo kitakuwa mmoja ya vipaumbele vyake vya juu, hasa katika eneo la mashariki na Katanga, eneo la uchimbaji madini anakotokea."Usalama, kama munavyojua, ni moja ya vipaumbele, haswa mashariki mwa Kongo na huko Katanga. Pamoja na maswala ya usalama, tuna pia maswala ya kijamii, ile ya maendeleo, maswala ya kisheria na pia swala la elimu kwa wote. Tuligusia mengi kuhusu mageuzi kwani yanahitajika katika sekta kadhaa," alisema Lukonde.Ilunga, mshirika wa Rais wa zamani Joseph Kabila, alikuwa mkuu wa serikali ya muungano. Kujiuzulu kwake kulifuata uamuzi wa Tshisekedi kumaliza makubaliano ya kugawana madaraka na wafuasi wa Kabila baada ya mvutano wa miezi kadhaa kati ya kambi hizo mbili.Naibu waziri wa zamani wa vijana na michezo, Kyenge, 43, hivi karibuni aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya taifa ya madini ya Gecamanine Juni 2019.Mwaka jana, bunge la chini lilimpigia kura ya kumuondoa aliyekuwa spika Jeanine Mabunda, mfuasi mwingine wa Kabila.Tshisekedi aliingia madarakani mnamo Januari 2019 na kutia saini makubaliano ya siri ya muungano na Kabila, ambaye aliwaweka wafuasi wake wengi bungeni katika nchi hiyo ya Afrika ya kati.
Shirika la afya duniani, WHO hapo jana limeridhia mpango wa chanjo ya virusi vya corona ya AstraZeneca kuanza kusambazwa kwenye mataifa maskini ikiwa ni baada ya kuithibitisha na kuona inafaa kwa dharura. Mataifa ya kipato cha chini na kati yanatarajiwa kupata dozi ya kwanza ya chanjo hiyo mwishoni mwa mwezi Februari, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kimataifa wa mgawanyo wa chanjo, COVAX. Shirika hilo linataraji kupeleka dozi milioni 336 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka na hadi bilioni 2 ifikapo mwishoni mwa mwezi Disemba.Covax ilizinduliwa mnamo Aprili 2020 na inaongozwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), pamoja na Umoja wa kushughulikia Chanjo Ulimwenguni. Covax inajulikana kama Covid-19 Vaccines Global Access Facility.Akionyesha ukosefu wa usawa mnamo Januari, mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisema zaidi ya dozi milioni 39 zimetolewa katika nchi zisizopungua 49, wakati 25 tu zikielekezwa katika moja ya nchi zenye kipato cha chini.Ukosefu huo wa usawa unatarajiwa kuendelea, kwani utafiti unaonyesha vipimo vingi vya chanjo vimenunuliwa na nchi zenye kipato cha juu.Nchi zenye kipato cha juu kwa sasa zina chanjo zilizothibitishwa zipatazo bilioni 4.2, wakati mataifa ya kipato cha chini yana dozi milioni 670 tu kulingana na utafiti wa Kituo cha Ubunifu wa Afya cha Duke.Mpango wa Covax ni nini?Covax imepanga kuhakikisha nchi maskini na za kipato cha kati zinazopokea sehemu kubwa ya chanjo.Covax inatumai kuwa, ifikapo mwisho wa 2021, zaidi ya dozi bilioni mbili zitakuwa zimesambazwa nchini kote ulimwenguni huku dozi zipatazo bilioni1.8. zikitarajiwa kuelekezwa kwenye nchi maskini zinazohusika katika mpango huo, zikiwa karibu 20% ya watu wao.
Ndiyo! Ni kiki, wala haihitaji kutazama mara mbili mbili. Wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wapendanao kila mmoja kwa nafasi yake alifanya mbwembwe zake ilimradi kumfurahisha yule mwenye ukaribu zaidi na moyo wake. Tunaweza kusema michoro na emoji za kopa viliteseka sana siku ya jana kwani zilitumiwa hata kwa watu wasio na nia njema na mapendo. Kila mtu alitumia ubunifu na kipaji kwa kadiri alivyojaliwa kuwasilisha hisia zake za huba. Kwa wale tusio na vipaji ilitosha kutumia ujumbe mkuu wa ‘Happy Valentine’ au Heri ya Valentine na kwa vile wapendwa wetu wametukubali bila kuwa na vipaji, walikubaliana na hali. Hata kama wasingekubali ingewapasa kusubiri hadi msimu mwingine kwani ubunifu hauji kwa bahati mbaya. Katika masuala ya mapenzi utakubaliana nami kwamba kila mtu ana kasi yake lakini hata kasi ya Usain Bolt haijazidi kasi ya wasanii. Wasanii wamekuwa mstari wa mbele kuonesha hisia zao bila kujali aina ya hisia. Na kwa hapa nyumbani Tanzania wasanii wetu wanasema ‘HipHop Hailipi’ kwa maana kwamba muziki au kazi ya sanaa inayowasilisha ujumbe usiobeba dhima ya mapenzi utapata wafuasi wachache na kujikuta muwasilishaji/msanii hapati maslahi mapana kama wanayopata wahubiri wa mapenzi. Wasanii wengi wa Bongo Fleva na filamu wamekuwa wajanja wa kucheza na hisia za mashabiki ambao wanaonekana kulevywa na mapenzi. Wasanii wamekuwa wakitunga maelfu ya nyimbo kuizunguka dhima hiyo na kama haitoshi wamekuwa wakitumia mahusiano ya mapenzi kama namna ya kuvuta attention ya mashabiki. Wenyewe wanaita kiki. Wasanii wengi wa-kike kwa wa-kiume wamekuwa wakitumia mahusiano yao au hata kutengeneza mahusiano feki kwa lengo la kuvuta umma kufuatilia kazi zao na kuwafanya waendelee kubaki juu katika kazi yao ya sanaa. Mbinu hii ambayo haiungwi mkono na baadhi ya waumini wa burudani imekuwa ikitumika sio tuu kwa wasanii wa Tanzania bali kila pembe ya dunia. Sijui labda mapenzi ndio kitu chenye mguso na nguvu zaidi kwa binadamu na ndio maana wengi hupenda kupata uzoefu wa watu wa maarufu kwenye mahusiano. Suala la mapenzi kuwa na mguso na nguvu zaidi kuliko kitu chochote laweza kuwa la mjadala wa kidunia. Wengi tunajua jinsi penzi la Beyonce na Jay Z linavyowafanya kufuatiliwa sana duniani. Nani asiyekumbuka penzi la Complex na Vivi au penzi la komando Lady Jay Dee na Gadner? Penzi la Vanessa na Jux? Au basi penzi lililosumbua la Diamond na Wema? Lakini hapa tumulike namna ambavyo kwa mwezi huu unaoitwa na baadhi ya washadadia mapenzi ‘mwezi wa wapendanao’ tumefanywa kusahau uwepo wa UKOVI-19 – ugonjwa hatari unaokatisha maisha ya wengi kote duniani. Katika muziki tukiachana na nyimbo na albamu kali zilizoachiwa mwezi huu. Masuala ya ‘Valentine’ yametikisa sana ambapo Harmonize pamoja na Rayvanny wameendeleza mbinu ya kutumia kiki ya mapenzi kuwafanya kuzungumziwa zaidi Tanzania bara na visiwani. Alianza Harmonize kwa kuimba kipande cha wimbo uliomlenga mwanamke asiyejulikana. Kipande hicho cha wimbo kinachojulikana kama ‘Mtaje’ akiwa anataja sifa za mwanamke anayetamani kuwa naye katika mahusiano na kuwaachia kazi mashabiki wake kutumia sifa hizo kumtambua mwanamke huyo. Harmonize alionekana kulalama kwamba nyota yake haikukubalika kwa Kajala enzi hizo akiwa rafiki na Wema Sepetu ila bado yeye anampenda mbali na kwamba amemzidi umri. “…Hivi niseme ana ngekewa, ama nyota yake kali amenizidi,Ama mjini nimechelewa, mbona wengine wanamponda wanamwita bibi…,” Hayo ni sehemu ya mashairi ya Harmonize akilalama kwenye Mtaje. Mashabiki wenye ufikiri wa haraka tayari walishamtaja Kajala Masanja hata kabla ya kipande hicho hakijamalizika. Wakati mashabiki wakiendelea kufurahia uzuri wa kipande hicho, ghafla picha za wawili hao wakiwa katika dimbwi la mapenzi zikaibuka. Mjadala kuhusu tofauti ya umri wa Kajala na Harmonize sio jambo la kujadili kwani lilishapitwa na wakati – kikubwa wawili hao wanafurahia ufuasi mkubwa na kuendelea kujihakikishi nafasi za ubalozi wa chapa mbalimbali ambazo huko ndiko wasanii hupata pesa za kuendelea kulipa kodi. Kajala (kushoto) akiwa na binti yake Paula kwenye moja ya kazi za ubalozi wa chapa ya taulo za kikeRayvanny ambaye ameachia albamu kali ya ‘Sound from Africa’ angeweza kuendelea kusumbua kwa mwezi mzima bila kujihusisha na familia ya Kajala. Lakini akaona isiwe kesi, kwa nini kiki apate Harmonize peke yake wakati anaweza kulipia gharama za kiki? Wakati watu wakiwa bize kujenga na kuhuisha mapenzi yao katika siku ya wapendanao, Rayvanny naye akaja na mtindo wa kiki aliotumia Harmonize yeye akiimba kipande cha wimbo unaokwenda kwa jina la ‘Valentine’. Katika wimbo huo Rayvanny anakiri kumfungulia moyo binti wa Kajala aitwaye Paula – binti anayesumbua katika mtandao wa Instagram kwa kile wataalamu wa urembo wanachokiita uzuri wa sura na umbo. Sehemu ya mashairi ya Valentine wa Rayvanny yaliyoandikwa kwa ustadi ni inaeleza binti huyu sio mkubwa kiumri ingawa ni mrembo na aliyeumbika vizuri. “…Moyo wake wa thamani amenipa bure, mtoto shepu kaitupa kule,Sio wa zamani 2000 mule mule, kadogo kadogo utasema kapo shule,…” Rayvanny anaendelea kueleza kwamba yuko tayari kutoa mahari kwa famila ya Paula ambaye kwa mujibu wake anasema ana chembechembe za uzuungu na usukuma. “…Ana uzungu chembechembe za MwanzaNitatoa mali kwa mzee Massanja” Hii ya Rayvanny imesambaa haraka kwani mbali na kuimba dedikesheni hiyo ya Siku ya Wapendanao na kukiri kutaka kupeleka mahari kwa mzee Massanja (babu wa Paula) tayari kuna video zinazowaonesha wawili hao wakifurahia mahusiano. Mazungumzo mengi yameibuka katika mitandao kuhusu video hizo na mahusiano hayo jambo lilifanya Kajala kumpa likizo Harmonize na kuanza kushughulikia suala la binti yake. Kwa kutazama mtiririko huu wa matukio ni rahisi kusema kwamba mbinu ya kutengeneza au kutumia mahusiano ya kimapenzi kwa lengo la kuvuta mashabiki ni mbinu inoyokosolewa lakini yenye mafanikio kwa wengi. Wasanii wengi wanaofuatiliwa zaidi ni wale wenye uwezo wa kutengeneza kiki. Kuna wale watakaouliza mbona hujamzungumzia Kala Jeremiah na picha zake za harusi kumbe anakuja na wimbo wa Wewe? Hahaah! Akili za kuambiwa changanya na zako.
Klabu ya Namungo FC imekwama kwa mara ya pili sasa kurejea nchini Tanzania kutokana na kuahirishwa kwa mchezo wake dhidi ya CD De Agosto kutoka katika mji wa Luanda nchini Angola. Taarifa za awali zilieleza kuwa timu hiyo ilipaswa kurejea nchini mapema Jumamosi Lakini mamlaka nchini Angola zilisitisha safari hiyo zikidai kuwa marubani wa ndege ya kukodi ambayo ilipaswa kuwasafirisha wachezaji hao walitakiwa wapumzike. Hata hivyo klabu hiyo kutoka kusini mwa Tanzania ilitarajiwa kuanza rasmi safari yake ya kurejea Dar es salaam mapema leo lakini safari hiyo imekabiliwa na mkwamo kutokana na watu watatu kukutwa na virusi vya corona na kuwekwa katika karantini nchini humo ambapo mamlaka zimewazuia watu hao kuondoka. Mwenyekiti wa timu hiyo, Hassan Zadidu amewataka Watanzania kuiombea kwani inakumbana na changamoto ambazo kwao ni ngumu kuzikabili kutokana na mazingira huku akidai kuwa suala la wachezaji wawili na afisa mmoja katika msafara huo kukutwa na virusi vya corona ni la uzushi“Lakini kwa bahati mbaya sana kitu wanachotumia ni cha uongo wanasema wamewapima test ya kwanza wako positive lakini wanasema wamewapima test ya pili wako positive lakini tulipowauliza kwa njia ya simu wakasema hawajawapima kwa mara ya pili kwahiyo ni uongo tu na udanganyifu,” amesema Zadidu.Baadhi ya wachezaji wamesema kuwa hawakupata chakula chochote tangu walipowasili zaidi ya maji na matunda huku wakidai kuwa wanateseka na kupitia katika mazingira magumu Shirikisho la soka Barani Afrika CUF liliahirisha mchezo wa kombe la Shirikisho baina ya timu hizo mbili uliopangwa uchezwe Jumapili ya tarehe 14 February mwaka huu, kutokana na msafara wa timu ya Namungo kutakiwa kukaa karantini kutokana na kadhia hiyo CAF Imesema kuwa italifikisha suala hilo kwenye kamati husika kwa ajili ya uamuzi. Klabu ya Namungo iliingia katika hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa Agregate ya 5-3 dhidi ya Al-Hilal-Obeyed baada ya timu hiyo kushindwa kucheza mchezo wake wa marudiano wakati CD De Agosto ya Angola ikifikia hatua hiyo baada ya kufungwa goli moja kwa bila dhidi ya Kaizer Chiefs kwenye mchezo wakufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika Nchi ya Angola ni miongoni mwa mataifa ambayo yanatekeleza makatazo na tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona amabapo kufikia February 10 nchi hiyo imeripoti visa 3262 vya Covid 19 na watu 57 na mpaka sasa wamefariki nchini humo.
Mapema leo, iliripotiwa kuwa Namungo FC ilizuiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Luanda nchini Angola ikidaiwa baadhi ya wachezaji wamekutwa na Virusi vya Corona.Namungo FC imekumbana na sintofahamu hiyo baada ya kutua katika uwanja wa ndege nchini Angola kwa ajili ya mchezo unaofanyika kesho Februari 14, 2021 dhidi ya Primeiro De AgostoMsafara wa Namungo FC umekwama uwanjani hapo kwa madai ya baadhi ya wachezaji kupimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amelielezea tukio hilo kuwa ni Siasa za Kimichezo na kusema, "Sisi kama Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje tunalifanyia kazi jambo hilo ili Timu hiyo iweze kushiriki michezo na kurudi nyumbani"Aidha, Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Tanzania Yusuph Singo pia ametoa tamko akisema wanajitahidi kwa ukaribu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania Nchini humo ili kulitatua suala hilo."Hatuko kimya na sisi kama Serikali tumeshituka na kushangazwa na hilo lakini tunalifanyia kazi tunawasiliana na wenzetu walioko huko," amesema.Wachezaji wa Timu ya Namungo waliondoka nchini hapo jana wakielekea nchini Angola kwa ajili ya mchezo unaofanyika kesho, Februari 14, 2021.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wamewatoa kimasomaso mashabiki wake baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa kwanza wa kundi A Michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Katika mchezo uliochezwa usiku wa Ijumaa Februari 12 katika dimba la Mashahidi jijini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Simba wamewashangaza wenyeji kwa kabumbu safi na hatimaye kuzoa alama zote tatu muhimu baada ya kushinda kwa goli moja kwa mkwaju wa penati. Simba walipata mkwaju wa penati dakika ya 60 ya mchezo kufuatia shambulizi la nguvu walilofanya katika lango la wenyeji wao AS Vita. Mshambuliaji Chris Mugalu aliwaibua wanamsimbazi kidedea baada ya kupachika mkwaju huo nyavuni na kuwapa goli pekee la mchezo huo. Simba ambao wamepangwa katika moja ya kundi gumu zaidi la michuano watatupa karata yao ya pili na mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri mnamo Februari 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Ushindi wa Simba unawaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika hatua ambayo si ngeni kwao kwani wameshacheza mara nne katika hatua hiyo na zote wakishindwa kufika nusu fainali.
Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha za aina mbalimbali jumla yake ikiwa ni silaha 199 na risasi 360, ikiwa ni pamoja na AK47 10, Pistol 16, Shortgun 39 na magobore 134.Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Msemaji wa Jeshi la Polisi ASCP David Misime amesema kuwa jumla ya watuhumiwa 177 Kati ya watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na wanaume 170 na wanawake 7. Ambapo wamekamatwa wakitumia silaha hizo katika matukio mbalimbali ikiwemo ya unyan’ganyi wa kutumia silaha, mauaji, uwindaji haramu, ujangili na kumiliki silaha kinyume na sheria. Katika hatua nyingine Jeshi hilo la polisi limefanikiwa kukamata Madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na bhangi ni kilo 13,230.22 mirungi kilo 11,804.864 cocaine kilo 4.52 heroine kilo 70.5 ambapo watuhumiwa waliokamatwa na madawa hayo ya kulevya ni 9,265, kati yao wanaume walikuwa 8,514 na wanawake 751. Pia Jeshi hilo limekamata pombe haramu ya moshi (gongo lita 69,295.30, pamoja na mitambo 379 ya kutengenezea pombe hiyo ambapo, jumla ya watuhumiwa 7169 walikamatwa ambapo wanaume 4647 na wanawake ni 2522.Kwa upande wa uhalifu kupitia mitandao ya simu kwa 2020 makosa yaliyoripotiwa ni 4850 watuhumiwa waliokamatwa ni 634 ambapo wanaume ni 490 na wanawake ni 144. Watuhumiwa waliokamatwa baadhi wamekutwa wametenda uhalifu huo zaidi ya mara mojaKesi zilizopata mafanikio mahakamani 2020 kwa maana ya watuhumiwa kupatikana na hatia na kupewa adhabu ni 4499.Jeshi la Polisi limesema kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano walioupata kutoka kwa wananchi ambapo wameonekana kuwa na muamko mkubwa katika kubaini, kuzuia na kutoa taarifa za kiuhalifu.
Kenya imeagiza dozi milioni 24 za chanjo ya chanjo hiyo ambayo inatarajia wiki ya pili ya mwezi Februari Licha ya wasiwasi wa hivi karibuni uliopelekea Afrika Kusini kusitisha mipango ya kuanza utoaji chanjo ya AstraZeneca na Oxford kwa madai ya kuwa utafiti umeonesha kuwa chanjo hizo hazina ufanisi katika kuzuia magonjwa mepesi na ya wastani kutoka kwenye aina mpya ya virusi,Nchi hiyo ambayo ina jumla ya idadi ya watu milioni 47 imesharipoti visa 97,398 vya maambukizi ya corona na vifo 1,694.Waziri wa afya, Mutahi Kagwe alinukuliwa na gazeti la Standard mnamo Alhamisi iliyopita akisema chanjo hizo zitaanza kutua mwezi ujao.Serikali imeagiza chanjo hizo kupitia mpango wa Umoja wa Afrika unaolenga kuhakikisha mataifa ya Afrika hayaachwi nyuma, Kagwe alisema.Wafanyakazi wa sekta ya afya na wafanyakazi wengine muhimu kama walimu watapewa kipaumbele katika ugawaji wa chanjo hiyo,waziri alisema ingawa hakuweka wazi ni kiasi gani chanjo hiyo itagharimu.Licha habari ya wasiwasi kuhusu chanjo ya AstraZeneca kusambaa, jopo la Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema faida za chanjo ya corona iliyotengenezwa na AstraZeneca na chuo kikuu cha Oxford huzidi madhara yote yanayoweza sababishwa na chanjo hiyo hivyo dozi hiyo inafaa kwa matumizi.
Inatoka sehemu ya kwanzaBaada ya serikali kuonekana kutotia nguvu kumuokoa Moro kwa kutofanya makubaliano na kundi hilo, ni dhahiri maisha ya Moro yalikuwa hatarini. Kelele na msukumo wa watu kuiomba serikali kufanya nalo mazungumzo hazikusikilizwa. Hata kelele za Papa Paul VI za kuomba serikali ifanye mazungumzo na kundi hilo ili kunusuru maisha yake, hazikufua dafu.Basi barua ya mwisho kutoka kwa Moro katika mfululizo wake wa barua, ilikwenda kwa mke wake, iliandikwa Mei 7. Ilikuwa barua ya kumuaga na dhahiri ikibeba simanzi na kukata tamaa: "Wameniambia kwamba si muda mrefu wataniua, nakubusu kwa mara ya mwisho", ilisema sehemu ya barua hiyo aliyoandikiwa mkewe kipenzi, Eleonora Chiavarelli, ambaye baadaye aliwapiga marufuku viongozi wa serikali na chama cha DC kuhudhuria mazishi ya mumewe kwa kudai walizembea makusudi kushughulikia uhai wake kwa kuwa walitaka afe. Kweli, siku mbili mbele, mwili wake ulikutwa umetelekezwa garini katikati ya viunga vya Rome, katika barabara ya Caetani, ukiwa umetobolewa kifuani kwa risasi.Ndiyo, ushikiliwaji mateka wa kiongozi mkubwa wa nchi kwa siku 54, tena ndani ya nchi, na baadaye mauaji yake, ilikuwa ni kitendawili kwa nchi hiyo iliyokuwa tenge kiusalama wakati huo. Kitendawili kilichoacha maswali kuliko majibu, ya je, ni kweli kundi la Red Brigade ndilo lililomteka na kumuua? Na kama siyo, nani alikuwa nyuma yake? Ni nani hasa alitaka Moro afe ili kuinusuru Italia na mkwamo zaidi wa kisiasa? Kwanini Marekani, Uingereza, NATO, na serikali ya Italia hawakutia juhudi kumuokoa Moro kama walivyofanya miaka mitatu mbele, 1981 kwa Mmarekani aliyekuwa akihudumu NATO Italia, Jenerali James Lee Dozier aliyetekwa na kundi hilo na kuokolewa na kikosi maalumu cha NOCS cha Italia? Kwanini serikali ya Italia imeweza kutegua kitendawili kwa kufanya uchunguzi na kupata majibu kwa mashambulizi na wale wote waliotendewa ubaya na Red Brigade, lakini imeshindwa kwa kiongozi mzito kama Moro?Basi katika kujibu kitendawili hiki cha mauaji ya Moro, kumeibuka nadharia nyingi kukihusu. Lakini mbili zimepata mashiko kiasi chake. Nadharia ya kwanza inayosema mauaji ya Moro yana mkono wa mataifa ya nje yenye nguvu yaliyovutana kiitikadi (lucidi superpowers) - Marekani na Umoja wa Kisovieti sanjari na mashirika yao ya kijasusi ya CIA na KGB, au na askari wa siri wa NATO wa "Operation Gladio". Mtu wa kwanza kuiongelea nadharia hii, ni mwandishi nguli wa habari za uchunguzi na upelelezi- juu ya siasa, uhalifu na makundi ya uhalifu - Mino Pecorell, aliyekuwa akiandika katika gazeti la "Osservatore Politico".Mara baada ya utekaji na mauaji ya Moro, mwaka uliofuata, Mei 1978, Pecorelli aliandika katika gazeti lake la "Osservatore Politico" juu ya nadharia hii ambayo alidai kuhusika kwa mataifa yenye nguvu(lucid suoerpowers) kwa madhumuni ya kulinda kile alichokiita misingi ya mkutano wa Yalta 1945(Logic of Yalta) na kutoiruhusu Italia kuangukia mikononi mwa Moscow. Mwandishi huyu alikuwa mtu wa kwanza kutaja hadharani mtandao wa siri wa kijasusi na kijeshi wa NATO - "Gladio" na kuuhusisha na kadhia hii ya Moro. Pia alikuwa katika mlolongo wa kuandaa nyaraka kuhusu jambo hili kiundani.Pecorelli, ambaye alikuwa na mtandao mkubwa wa marafiki kutoka kundi la "P2- Masonic Lodge", na ambaye alikuwa ni mwandishi pekee aliyeweza kupata siri nyingi na nyeti za mashirika ya kijasusi na vyombo vya usalama na serikali, aliuawa na Mafia kwa risasi nne Machi 20, 1979 mjini Rome, kwa amri ya Waziri Mkuu wa kipindi hicho aliyejihusisha na Mafia, Giulio Andreotti. Pecorelli aliuawa akiwa ndani ya gari lake aina ya "Citroë CX". Aliuawa ili kuzima kile kilichodaiwa alijua mengi kuhusiana na sakata la Moro. Nadharia ya pili ni ile inayoihusisha serikali ya Italia kuhusika na kifo cha hasa kwa matendo yake ya kutotilia uzito jambo la kuokoa maisha ya Moro. Matendo yake, kama kusitisha kufanya mazungumzo na Red Brigade kwa madai ya kuwa serikali haiwezi kulipigia magoti kundi hilo. Pia kupuuza taarifa nyeti za kule alikofichwa wakati akishikiliwa mateka. Taarifa ya Romano Prodi, Profesa wa chuo kikuu cha, ambaye Aprili 2, 1978 wakati Moro yupo matekani, alikutana na wakufunzi wengine sita wa chuo hicho nyumbani kwa Profesa Alberto Clo karibu na mji wa Bologna. Lengo la kutano lao, lilikuwa ni kufanya uaguzi kwa kuiomba mizimu ya mababu wa chama cha DC kiwaambie kule aliko Moro.Katika uaguzi huo, mzimu wa Prodi ulimtajia maeneo matatu fikrani mwake - Virtebo, Bolsena na Gladoli. Maeneo haya yote matatu, yapo kaskazini mwa mji wa Lazio, lakini kuna kaeneo ambako si maarufu kanaitwa Via Gladoli 96 kapo mji wa Rome - mji ambao ndio haswa iliaminika Moro anashikiliwa. Prodi hakuwahi kulifahamu jina Gladoli, lakini mzimu ulimgahamisha fikrani. Alitoa taarifa hizi za uaguzi katika makao makuu ya chama cha DC mjini Rome, idara ya masuala ya jinai ya chuo cha Bolgna, na Polisi.Lakini jambo la kushangaza, iliwachukua polisi hadi siku nne kuchunguza eneo hilo la Via Gladoli mjini Rome, ambapo hawakubaini kitu. Lakini Aprili 18, eneo hilohilo ambalo polisi hawakukuta kitu, iligundulika jengo ambalo lilikuwa ngome ya Red Brigade, na mmoja wa viongozi wao aliishi katika jengo hilo. Hata kama Moro hakushikiliwa katika jengo hilo, lakini Prodi alikuwa sahihi kulihusisha eneo la Via Glafoli na Red Brigade. Lakini je, mizimu yake ilijuaje? Achilia mbali polisi kujuzwa fununu za Profesa Prodi za kwamba Moro alikuwa eneo la Via Gladoli, hilo tisa. Kumi, ni miaka miwili mbele baada ya kadhia ya Moro, ni taarifa ya mwandishi wa habari, Luca Villoresi Juni 1980 katika gazeti la "La Republica", naye alipata taarifa nyeti za ilipokuwa mahakama ya siri ya Red Brigade - alipokuwa ameshikiliwa Moro kwa siku 54. Eneo hili kusini mwa Rome, linaitwa Via Montalcini. Baada ya andiko lake, Villoresi hakuitwa ili hata kulisaidia jeshi la polisi kwa aajili ya uchunguzi. Ilikuwa kimya! Aligundua kuwa polisi walijua eneo hili tangu siku ya kwanza alipotekwa Moro, lakini hawakuchukua hatua kulivamia.Pia, Villoresi aligundua kuwa gari iliyosemekana ni ya shirika la kijasusi la Italia, ambayo ilifungiwa vifaa vya umeme vya kiupelelezi, na ambayo hata wakati wa tukio la utekaji wa Moro ikisemekana kuwepo eneo la tukio, basi ilikuwepo eneo hilo la Via Montalcini. Villoresi alijua viongozi wa wakuu wa chama cha DC na serikali kama waziri wa mambo ya ndani, Francesco Cossiga na Waziri Mkuu, Giulio Andreotti, wanajua ukweli lakini wanafinyangafinyanga suala hili ili kuuficha ukweli wa sakata la Moro. Na hata wale waliojaribu kuibuka nakuonesha njia juu ya sakata hili, walizimwa. Huenda ni kweli walitaka Moro afe.Akinukuliwa na gazeti la "Indipendent" la Uingerza la Octoba 22, 2011, Villoresi aliandika katika "La Rebublica": "Sakata la Moro halijaleta ufumbuzi sahihi zaidi ya kuzalisha uongo mwingi. Nafikiri ni vugumu sasa kuelewa nini kilitokea", aliandika. "Kuna watu wanaoujua ukweli, lakini hatuwezi kujua kama wanatuambia ukweli". Ni dhahiri Villoresi aliwarejelea Cossiga na Andreotti kuujua ukweli, lakini hawakutaka kuusema. Hata baada ya kufariki kwa viongozi hawa, bado kitendawili cha Moro kimebaki palepale.Lakini jambo lingine linaihusisha serikali ya Andreotti, ni kwa wanachama wa Red Brigade waliokamatwa baadaye wakisemekana kuhusika na kadhia hii ya Moro. Walikuwa jela miaka nenda rudi, pasi na serikali kuanzisha kuwahoji ili kupelekea uchunguzi juu ya jambo hilo. Kwanini uchunguzi ulitupwa kapuni wakati pakuanzia ni hapo? Hatujui.Pia nadharia ya kuhusika kwa serikali inakaziwa na mauaji ya Jenerali Carlo Alberto Dalla Chiesa Septemba 3, 1982. Jenerali Chiesa alifanikiwa sana kuwakamata na kusambaratisha ngome za Red Brigade kuliko yoyote. Mei 1, 1981, aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi wa Palermo katika kisiwa cha Sicily ili akaudhibiti mtandao wa Mafia. Unajua kwanini Chiesa alipelekwa Sicily na Waziri Mkuu Giulio Andreotti? Sicily ilikuwa ni ngome kuu ya Mafia, na katika viongozi waliotokea Italia kuwa na mahusiano na Mafia, basi ni Andreotti. Kupelekwa kwa Chiesa Sicily, alipelekwa katika mdomo wa mamba makusudi ili auawe. Na kweli, aliuawa na Mafia kwa amri ya kiongozi wao Salvatore 'Toto' Riina, miezi minne mbele tangu ateuliwe. Yasemekana Jenerali Chiesa alikuwa mmoja wa watu waliojua kiundani kuhusu sakata la utekaji na mauaji ya Moro.Ndiyo, sakata la Aldo Moro ni mazalia ya msuguano wa vita baridi iliyoweka ombwe la kisiasa kwa Italia, nchi ambayo iliathiriwa pa kubwa na msuguano huo kuliko nchi yoyote ya Ulaya. Moro anabaki kuwa mwathirika wa msuguano huo, akiwa kama daraja la maridhiano. Akiwa na ndoto ya kuiona Italia isiyopasuka kati kiitikadi, bali yenye umoja. Akiwa na ndoto ya kutimiza kile alichokiita maridhiano ya kihistoria(historical compromise) katika nyakati za hatari. Lakini ndoto hii ilikufa siku aliyotekwa, na ilizikwa siku aliyouawa. Hata ule ushirikiano wa wa maneno tu, wa DC na PCI, ulikufa palepale. Na ukawa mwanzo wa kifo cha chama cha PCI kilichojifia taratibu sanjari na anguko la Umoja wa Kisovieti.Katika msuguano huu wa siasa za vita baridi kwa Italia, hauwezi kuongelewa bila kutajwa kwa sakata la Moro, daraja la maridhiano lililobomolewa kabla hata ya kuvusha maridhiano yenyewe. Na kitendawili chake, cha nani hasa aliyebomoa daraja hili? Ingali masikioni mwetu tunalisikia jina la kundi la mrengo wa kushoto-mbali, la Red Brigade. Ni kundi la namna gani hili? Basi tuendelee.Kuzaliwa na kufa kwa kundi la Red Brigade, na harakati zake.----------------------------------------------------------------------------------------Wakati utawala wa dikteta wa kifashisti, Benito Mussolini unahitimishwa rasmi nchini Italia mwaka 1943, baada ya miongo miwili ya figisu za bila siasa za upinzani - za kudhibiti vyama vya siasa, kufunga na kuua wapinzani wake au kuwakimbiza uhamishoni - na mika miwili mbele(1945) vita kuu ya pili ya Dunia ikifikia tamati; ilishuhudiwa mwanzo ulioleta matumaini wa ukurasa mpya wa siasa za vyama vingi na ushindani nchini humo. Siasa hizi zilianza kujengwa kwa kuandika katiba mpya mwaka 1947 iliyopitishwa na Bunge la katiba Disemba 22, na kuachapishwa katika gazeti la serikali Disemba 27. Katiba iliyovunja mamlaka ya Kifalme, na kupeleka mamlaka kwa wananchi kwa kuwa rasmi Jamuhuri, iliandikwa kwa umakini kuzuia nchi hiyo kurudi tena katika udikteta wa kifashisti au mwingine wowote. Na mwaka uliofuta(1948), ulifanyika uchaguzi mkuu ambao ulishuhudia chama cha Democrazia Cristina(DC), au Christian Democrat cha mrengo wa kati kikishinda na kushika serikali, na baadaye kiendelea kushinda kwa zaidi ya miongo minne mbele kwa msaada wa Marekani na washirika wake kwa hofu ya vita baridi.Vyama vya mrengo wa kushoto ambavyo vilidhibitiwa barabara na serikali ya kifashisti ya dikteta Mussolini, husani chama cha kikomunisti cha Partito Comunista Italiana(PCI), au Italian Communist Party, na kile cha kisoshalisti cha Partito Socialista Italiana(PSI), au Italian Socialist Party, na vyama vinginevyo, hatimaye navyo baada ya miongo miwili vilirudi katika ulingo wa siasa vikishiriki uchaguzi huo. Uchaguzi ulioonekana kama neema ya ukurasa mpya kwa nchi hiyo, ulififia ghafla. Kwani ulikuwa mwanzo wa sakata la vita baridi iliyoingilia kati siasa hizo mpya na kuigeuza Italia kama chumba cha mvutano wa vita hivyo kwa Ulaya - kati ya Marekani na washirika wake, dhidi ya Umoja wa Kisovieti, na kuipelekea nchi hiyo katika ombwe kuu la kisiasa kwa mapambano ya makuu ya kitabaka.Mapambano ya kitabaka - kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa, yalizua vurugu, migomo na maandamano ya mara kwa mara ya wanafunzi, wafanyakazi na asasi za kijamii. Na katika mapambano haya ya kitabaka, ndipo kuliibuka makundi yenye misimamo mikali ya kisiasa. Na hapa, liliibuka kundi maarufu lenye misimamo mikali ya kisiasa ya mrengo wa kushoto-mbali(Marxist-Leninist), la Red Brigade, au kwa kiitaliano, "Bigate Rosse(BR)", ambalo taratibu lilienda mbali zaidi likiendesha mapambano yake kwa kufanya mashambulizi yaliyotumia mbinu za kigaidi ili kutimiza malengo yake ya kuipeleka Italia mrengo wa kushoto.Naam, kuibuka rasmi kwa Red Brigade kunaanzia Octoba 20, 1970 kwa wachumba wawili na wanaharakati wa mrengo wa kushoto, wanafunzi wa " Sociology" wa chuo kikuu cha Trento, Renato Curcio na Mara Cagol, sanjari na rafiki yao Alberto Franceschini, mara baada ya kuhamasishwa na harakati; na maandiko ya wapiganaji wa mrengo wa kushoto sehemu mbalimbali Duniani kama Mao Zedong, Lin Biao, Che Guevara, Carlos Marighella na Abraham Guillen, walikutana mwaka huo na kuunda kundi hili kwa siri ambalo shughuli yake hasa ilianza kuonekana mwaka uliofuatia. Na baadaye mwaka huo uliofuatia(1971), alijiunga kijana mwingine mtukutu, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Milan, Mario Morreti, ambaye ilisemekana kuwa ni 'afisa kipenyo' wa shirika la kijasusi la Marekani la CIA, bila kundi hili kujua. Na huyu ndiye aliyoongoza kundi hilo kumteka waziri mkuu, Aldo Moro baadaye mwaka 1978.Red Brigade lilijiona zaidi kama mazalia ya kundi la wafanyakazi lililoitwa "Autonomia Operaia", kundi lingine, si la mapigano, bali la harakati(Etra-Parliamentary Movement) za misimamo mikali ya mrengo wa kushoto, ambalo liliipinga serilikali ya DC, na hata wale viongozi wa mrengo wa kushoto au wa ushirika wa wafanyakazi waliojinasibisha na serikali. Basi katika makundi yote ya awali ya mrengo wa kushoto kabla ya Red Brigade kuzaliwa, basi kundi la "Autonomia Operaia" ambalo harakati zake zilitawala sana katika miji ya Milan na Turin, ndilo lililokuwa na mtazamo wa mapambano ya zaidi ya harakati - kutumia silaha kufanya mapinduzi na kuipeleka nchi mrengo wa kushoto - lilitamani sana jambo hili. Na kwa miazamo huu uliokuwa na mvuto kwa Red Brigade, basi nao walijiona ni mazalia ya "Autonomia Operaia", na si ajabu hata shughuli zao nyingi, licha ya kusambaa nchi nzima, lakini zaidi zilijikita katika miji hii mkubwa miwili, na baadaye wanachama wake wengi wakitokea "AO".Basi kundi hili la Red Brigade liliundwa kwa kile inachodaiwa kushindwa kwa chama cha PCI cha mrengo wa kushoto, ambacho ndicho kilichokuwa mguu wa wafanyakazi wa kusimamia mapambano yao ya mabadiliko. Liliundwa kwa malengo makuu mawili. Kwanza, kufanya mashambulizi kwa kutokomeza kile walichokiita adui wa wafanyakazi - ubepari. Kwa mtazamo wa kikomunisti, waliona kuwa wafanyakazi ni daraja la mapinduzi, mfumo wa kibepari ni adui wao, serikali iliyokuwepo madarakani ni kama mbwa-mlinzi wa mfumo wa kibepari, na Chritian Democrats ndiyo chama chao(cha mabepari). Hivyo, ili kupambana na adui 'ubepari', mwanzoni mwa maisha ya kundi hilo walijenga misimamo mikali ya mrengo wa kushoto-mbali kwa wafanyakazi, kwa kupandikiza wanachama wao ndani yake waliokuwa wanaharibu mashine za viwanda, mali za viongozi wa ushirika walioungana na mabepari, na ofisi zao.Pili, walikuwa na lengo la kuamsha ari ya mapambano, ya mapigano ya kutumia silaha ili kufanya mapinduzi kuunda taifa la mrengo wa kushoto baada ya mbinu za maandamano na migomo kutoleta ufanisi, na hatimaye kukata uanachama wa Italia chini ya NATO na Marekani ambao ndio mzazi wa ubepari. Ambapo ili kufanikisha hili, mihimili ya serikali ya Italia, mali na watumishi wa NATO nchini Italia, mali za Marekani, viwanda vyake, makampuni yake, na raia wake ambao ni viongozi wa NATO na jeshi, walilengwa na mashambulizi ya Red Brigade.Mwanzoni kabisa wakati kundi hili limeundwa, halikuwa na mtazamo wa kufanya mashambulizi ya kigaidi, zaidi ya mapambano ya kisiasa ya kutumia silaha na kupandikiza ari ya mapinduzi kwa wafanyakazi na wanafunzi ili kuipindua serikali na kuitenga na NATO, kwa kuunda serikali ya mrengo wa kushoto. Hata mashambulizi yake yalifanywa kwa umakini mkubwa ili kuepusha kuumiza au kuua wale wasio na hatia kwa nia kuzuia taharuki na mitazamo tofauti kwa jamii. Lakini hadi kufikia mwaka 1974, kundi hili lilibadili mbinu ya mapambano kwa mashambulizi yao kuwa ya kigaidi zaidi, na hasa baada ya mwaka huo kufanya shambulizi kali lililowaacha mahututi wanachama wawili wa "Movimento Sociale Italiano(MSI)", kundi la kifashisti la mrengo wa kulia-mbali. Kubadili mbinu za mapigano kuwa ya kigaidi kulianza kupunguza uungwaji mkono wa wafanyakazi kwa kundi hili kwa baadaye, wakijitenga nalo.Kubadilika kwa kundi hili kuwa la kigaidi zaidi ni kutokana na wanachama wake - wanafunzi na wafanyakazi waliokuwa na malengo ya kisiasa kujiondoa taratibu kundini, ambapo wanachama wapya waliojiunga nalo, wengi ni walikuwa ni wanafunzi waliocha vyuo na kujiunga na harakati, watukutu wa mtaani, na waliokuwa wafungwa wa kisiasa wenye misimamo mikali ya mrengo wa kushoto. Hivyo kundi likawa na misimamo mikali zaidi kwa wanachama wapya kukutana na wanachama wa zamani walioibukia katika matendo ya mwanzo ya uharibifu wa mali na mashine za viwanda vya mjini Milan kama Sit-Siemens, Pirelli, na Magnet Marelli; na kile cha Turin - Fiat - ambacho kilikumbwa na mashambulizi na uharibifu wa mara kwa mara. Mashambulizi ya viwanda yalikwenda sanjari na uharibifu wa magari ya viongozi wa ushirika wa wafanyakazi walioonekana kikwazo kwa kufuata maagizo ya serikali. Na mashambulizi mengine waliyaelekeza makao makuu ya ushirika na ofisi za biashara, na baadaye utekaji wa viongozi wa serikali na wafanyabiashara, uporaji, na mauaji. Na utekaji wa kwanza kabisa wa kundi hilo, ukianzia mwaka 1972 kwa "foreman" wa kiwanda cha Sit-Siemens kutekwa na kushikiliwa kwa dakika kadhaa kabla ya kuachiwa.Mikakati na mipango yote ya kundi hili, ilipangwa na ngazi ya juu ya utawala "Strategic Directorate(DS)" na ngazi za chini zikichukua mipango hiyo kwa aajili ya utekelezaji, lakini kukitawaliwa na ukuta mkubwa wa usiri, wa mawasiliano kati ya "Strategic Directorate" na ngazi za chini. Mfumo wa kiutawala wa kundi hili uliundwa mwaka 1974 na "DS", waasisi wa kundi hili ukiwa kama vile wa kijeshi. Katika ngazi ya juu kabisa ya utawala, ilianza na "Strategic Directorate" ambayo kwa mujibu wa ripoti iliyokuwa ya siri ya CIA("The Red Brigades: A Primier") ya 1982, na ambayo iliwekwa wazi 2008, inadai mamlaka za Italia zilikadiria kuwa ngazi ya "Strategic Directorate" ya Red Brigade ilikuwa na watu kumi, lakini mamlaka kamili ilikuwa mikononi mwa watu wasiozidi watano, waasisi wa mwanzo wa kundi hili. Watu hawa walikutana mara chache sana kwa mwaka, kutoa maagizo, kuunda sera na mikakati.Chini ya "DS" ilifuatia kamati tendaji ("Executive Committee") ambayo ilifanya kazi kama makao makuu ya kutafsiri na kuhakikisha yale yanayotoka ngazi ya "DS" yanafanyika. "Executive Committee" ilikuwa na majukumu ya kutoa kibali kwa mashambulizi yaliyokwenda kufanywa na ngazi iliyofuata ya "Columns", ambapo ikiwa shambulizi lililotakiwa kufanyika ni kubwa, basi "EC" walibeba jukumu hilo wao la kufanya shambulizi hilo ili kuepusha taharuki katika jamii. Pia walikuwa na majukumu kama kusimamia masuala ya kifedha hasa kwa kupokea bajeti za "Columns" na kutoa amri kwa kitengo cha "Logistic Front" kutafuta pesa hizo, na zilitafutwa kwa uporaji wa benki, kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, na kumteka mtu kwa mabadilishano ya fedha.Chini ya "Executive Committee", ilifiatia ngazi ya utawala iliyoitwa "Columns", ambazo zilisambaa katika miji mbalimbali. Kila "Column" ilikuwa na mamlaka katika eneo lake kwa aajili ya kutekeleza maagizo ya "Executive Committee". Hizi " Columns" zilikuwa Rome, Milan, Venice, Naples, Turin na Genoa, na baadaye zilitanuka zaidi katika miji mingine. Pia ilikuwepo "Column" ya jela, na hii ilitokana na wafungwa wa kundi hili waliokuwa kifungoni, pia waliunda "Column" yao kwa siri kwa kupata wanachama wapya ndani ya magereza. Maeneo ambayo hayakuwa na "Column", yaliongozwa "Regional Executive Committee".Na "Cell" ilikuwa ngazi ya mwisho kabisa ya utawala ya kundi hili. Ambayo kila "Cell" ilikuwa na magaidi watatu hadi watano. Brigade mmoja, alipewa jukumu la kuongoza "Cell" mbili zilizokuwa na jumla ya wanachama 15 au zaidi. Na huyu Brigade alitoa taarifa na kuwajibika katika ngazi ya "Column".Katika mtiririko huu wa utawala wa kundi hili, mipango yao isingekwenda bila ya kuwa na kitengo cha cha usaidizi cha "Front" kilichofanikisha mikakati yao kusonga. Kitengo hiki kilikuwa na matawi mawili - "Front of the Mass" na "Logistic Front". Tawi la "Front of the Mass" lilikuwa na jukumu la kukusanya taarifa za kiintelijensia na tafiti; na ndani yake kukiwa na vitengo maalumu vitatu viliyokusanya taarifa za mashambulizi kila kimoja eneo lake. Ambapo kitengo cha "Factory Brigade", kilikusanya taarifa upande wa viwanda, "Political Party Brigade", kilikusanya taarifa upande wa siasa, na "Triple Brigade" kilikusanya taarifa upande wa vyombo vya dola - polisi, mahakama na magereza.Tawi la "Logistic Front" lilikuwa na jukumu la kusaidia "Columns" zote kwa kutafuta silaha, kuainisha maeneo(shabaha) ya kushambulia, kufanikisha vifaa vya mawasiliano, matibabu kwa wapiganaji wake wanaojeruhiwa katika mapambano, usajili wa siri wa wanachama wapya, na kuhakikisha mishahara kwa wanachama wake wa ngazi za juu. Labda swali linaweza kuwa, ni wapi tawi hili lilipata fedha na silaha kwa ajili ya kufanikisha haya? Katika uchunguzi wa CIA na mamlaka za Italia, zilibaini kuwa kundi hili halikupata moja kwa moja msaada wowote wa kifedha na silaha kutoka kwa serikali ya Umoja wa Kisovieti kama ilivyodhaniwa, bali lilipata msaada wa silaha kutoka makundi ya wapiganaji ya mrengo wa kushoto kutoka Umoja wa Kisovieti, na wapiganaji wa Kipalestina wa kundi la "Palestina Liberation Organization(PLO)". Na fedha, walizipata kupitia uporaji wa Benki, uuzaji wa dawa za kulevya(mara chache), na utekaji wa wanasiasa na wafanyabiashara kwa aajili ya fedha. Mfano mzuri ni utekaji wa Vallarino Gancia mwaka 1974, mfanyabiashara wa kiwanda kwa aajili ya kutaka fedha.Basi ikiwa ni mwaka huohuo wa 1974 mwezi Septemba, baada ya kuunda mfumo wa utawala wa kundi hili, viongozi wake wawili wakuu na waasisi, ambao walikuwa katika ngazi ya "Strategic Directorate", Renato Curcio na Alberto Franceschini, walikamatwa na Jenerali Carlos Alberto Dalla Chiesa(baadaye aliuawa na Mafia) kwa msaada wa 'afisa kipenyo' Silvano Girotto. Wawili hawa walihukumiwa kifungo cha miaka 18 jela. Curcio alitoroshwa gerezani na kikosi cha makomando wa Red Brigade wakiongozwa na mkewe, Mara Cagol(aliuawa mwaka 1975), lakini alikamatwa tena baadaye.Baada ya kukamilisha kuunda mfumo wa utawala na ikishuhudia kutanuka kwa kundi hili katika miji ya Rome, Genoa na Venice, mwaka uliofuata wa 1975, walichapisha muongozo wao uliokuwa na dhamira kuu ya kushambulia 'moyo' wa serikali - mihimili na watendaji wake, kwa sababu ya serikali kuwa mwavuli mkuu wa makampuni ya kibepari yaliyowanyonya wafanyakazi. Na kuanzia mwaka huo, mashambulizi ya kundi hili yalikuwa makali mno kwa serikali hadi kuelekea mwishoni mwa mika ya 1970. Na hasa mashambulizi yalitiwa chachu zaidi mwaka huo wa 1975 baada ya Mara Cagol, kuuawa na polisi katika majibizano ya risasi baada ya polisi kutaka kumkomboa mateka aliyeshikiliwa na kundi hili. Pia, polisi wawili waliuawa katika majibizano hayo ya risasi.Oparesheni ya mashambulizi ya kundi hili yalipangwa kwa majira na yakiwa na ujumbe maalumu. Hasa, katika majira ya miezi ya mwanzo mwa mwaka(spring) na miezi ya mwishoni mwa mwaka(fall). Kwa mfano, uongozi wa juu wa kundi hilo(Strategic Directorate), walipanga miezi ya mwanzo mwa mwaka, ilikuwa kushambulia 'moyo' wa serikali. Na si ajabu Machi 16, 1978, Waziri Mkuu mstaafu, Aldo Moro alitekwa na baadaye kuuawa siku 54 mbele. Hivyo hivyo, kwa upande wa miezi ya mwishoni mwa mwaka, ilipangwa kuwa mashambulizi yaelekezwe zaidi kwa NATO na washirika wake ili kufikisha ujumbe kwa nchi za Magharibi. Pia, si ajabu kuwa, Disemba 17, 1981, wanachama wake wanne walijifanya mafundi bomba na kuingia katika jengo la raia wa Marekani, na makamu Kiongozi wa jeshi la NATO la ardhini ukanda wa kusini mwa Ulaya, Jenerali James Lee Dozier. Ambapo alitekwa huku mkewe akifungiwa na kamba katika jengo hilo. Dozier alishikiliwa kwa siku 42 kabla ya kuokolewa Januari 28, 1982 na kikosi maalumu cha Polisi cha Italia cha NOCS.Kundi hili liliongeza kasi ya utekaji kadiri miaka ilivyosonga. Na baadhi ya mateka walihukumiwa na mahakama ya siri ya kundi hili, iliyoitwa "People's court". Na wengine walihukumiwa kifo na kuuawa, kama Aldo Moro. Lugha ya kisheria kama ile waitumiayo serikali kuhukumu wahalifu, ilitumika panapohitajika kumuua mateka wao ili kulipa uhalali jambo hili na kuilinda taswira yao kwa jamii. Badala ya kusema ameuawa, walisema " amehukumiwa kifo".Achilia mbali watu wenye majina makubwa kama Moro na Dozier, pia majaji, ma-meya, askari, na wafanyabiashara - nao walikuwa wahanga wakubwa wa mashambulizi ya kundi hili ambalo lililopotoka katika lengo lake baada ya kupenyezwa na majasusi wa nchi za Magharibi na kulivuruga kuanzia ndani. Mathalani, mwaka 1979, mwanasheria na mkufunzi wa chuo cha Genoa, Fausto Cuocolo alivamiwa chuoni na kuuawa wakati akisimamia mtihani. Mashambulizi makubwa kwa muhimili wa sheria ulisababisha hata mawakili kuogopa kusimamia kesi zao pindi walipokamatwa.Kunzia mwa mwaka 1978 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1980, mara baada ya utekaji wa watu wakubwa kisiasa; kama Moro na Dozier, serikali ikishirikiana na mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi MOSAD, CIA na M16, na "operation Gladio" ya NATO walizidisha kasi kupenyeza majasusi wao katika kundi hili na kulivuruga kuanzia ndani na viongozi wao wengi, waasisi kukamatwa, na wengine kukimbilia nchini Ufaransa. Na si ajabu, mwaka 1981, kundi hili lilipasuka katikakati kwa makundi mawili. Kundi la kwanza lililokuwa na uungwaji mkono na wanachama wengi liliongozwa na Barbara Balzerani, lilitwa "Communist Combatant Party", na kundi la "Union of Combatant Communists" likiongozwa na Giovanni Senzani.Mgawanyiko wa makundi haya mawili, kila moja liliendelea kufanya mashambulizi kwa kivyake. Ikiwa ni pamoja na mauaji ya Lemon Hunt mwaka 1984, afisa wa jeshi wa Marekani; mauaji ya Lando Conti mwaka 1986, Meya mstaafu mji wa Florence; mauaji ya Reborto Ruffilli mwaka 1988, Seneta na mshauri mkuu wa Waziri Mkuu Ciriaco de Mita katika masuala ya Ulaya. Mauaji haya ya viongozi yalikwenda sanjari na mauaji ya watu wengine wengi wa kawaida.Red Brigade lilikufa rasmi mwaka 1988 baada ya kuacha lenyewe mapambano na wanachama wake wengi kulikimbia kundi hilo. Na wakati huo Umoja wa Kisovieti ukelekea mwishoni. Kuna baadhi ya sababu zinaweza kuainisha kwa nini kundi hili halikuweza kutimiza malengo yake ya kuipeleka Italia mrengo wa kushoto.Kwanza, katika taarifa ya siri CIA ya April, 1982 "The Red Brigade: A Primier", wanagusia maandiko ya Carlos Marighella ya mwaka 1969, yanaokwenda kwa kichwa cha "Min-Manual Of Urban Guerrilla Warfare", ambayo ndiyo hasa miongoni mwa yaliyoshawishi mbinu za kundi la Red Brigade. Katika maandiko yake, Marighella anachukua wazo la kuwekeza nguvu katika mapigano nje ya mji kuliko na jamii za wakulima ili kufanikisha mapinduzi yaliyoainishwa katika maandiko ya Che Guevara na Mao Zhedong, na yeye kubadili mbinu hizo kuwekeza zaidi mapigano mijini. Lakini jambo moja, makundi ya wapiganaji ya mrengo wa kushoto, likiwemo Red Brigade na yale ya Dunia ya tatu, hawakuweza kuelewa lengo la Marighella katika maandiko hayo.Marighella katika maandiko yake, si kwamba anataka kusiwepo na mapigano sehemu za nje ya mji, bali alilenga mapigano ya mjini yangeweza kuhamisha nguvu za vikosi vya serikali na kuwekeza nguvu hizo kuzima mapigano ya mjini, na wakati huo wapiganaji wa mrengo wa kushoto wakijiimarisha zaidi nje ya miji na hivyo kuenea sehemu zote mijini na nje ya miji na kuvishinda vikosi vya serikali kwa urahisi. Kwa upande wa Red Brigade hawakuliganya hili huenda ni kukosa lengo la maandiko ya Marighella. Wao waliwekeza mapambano yao mjini tu, na kusahau sehemu za vijijini ambako kulikuwa na wafuasi wengi wa itikadi za mrengo wa kusho nchini Italia, hasa wakulima.Pili, kushindwa kwa kundi hili kufanikisha lengo lao kulitokana na mbinu za mapigano walizochagua, kuwa za kigaidi zaidi kuliko zile za mapigano ya kisiasa. Na zaidi mbinu hizi hazikueleza ni vipi zinavyoweza kuipindua serikali ya kibepari na kuisimika serikali ya kijamaa. Mbinu kama mashambulizi kwa raia wasio na hatia, utekaji hasa ule wa Aldo Moro uliomuhuzunisha kila mtu achilia mbali mrengo wake wa kiitikadi, uporaji wa mabenki na uuzaji wa dawa za kulevya ziliwakimbiza wanachama wa kundi hilo hasa wafanyakazi na kuona limekengeuka katika lengo lake.Tatu na mwisho, bila shaka kundi hili lilijua wazi aina ya mapambano waliyochagua yatakuwa ya muda mrefu na yenye vikwazo vikubwa katika wakati huo wa vita baridi. Wakati ambao propaganda, mikakati ya majasusi, mauaji na kila aina ya uchafu ulitumika kila upande kuvutia kwake. Ni wakati huu ambao kundi hili liliingiliwa kwa siri na 'maafisa vipenyo' na majasusi wa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi kuhakikisha wanaliua kundi hili na kuiepusha nchi hiyo kuangukia katika itikadi za mrengo wa kushoto. Na si ajabu kuwa hata mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na kundi hilo, yalikuwa ni kwa mkono wa majasusi waliotaka kuvuruga lengo na kuchafua taswira ya kundi hilo katika jamii. Na walifanikiwa.Hivyo basi, kunaweza kuwa na sababu nyingi, lakini kundi hili llililokuwa kuu ukanda wa Ulaya nyakati hizo, lilijifia mwaka 1988 sanjari na anguko la Umoja wa Kisovieti. Baadaye kukaibuka makundi madogo madogo ya kigaidi nchini humo yaliyoakisi mienendo ya Red Brigade. Lakini kifo cha kundi hili, kinaacha alama mbaya katika historia ya vitabu vya Italia - utekaji na mauaji ya Waziri mkuu mstaafu, Aldo Moro.Kwa ushauri, napatika twitter kwa jina la @OscarMwaisoloka MarejeleoGisborg, P.(1990). A History Of Contemporary Italy: Socialist and Politics 1943-1998; London. Penguin Books Ltd.CIA. "The Red Brigade: A Primier", 1982. (PDF) Gumbel, A. (2011,October 22). The riddle of Aldo Moro: was Italy's establishment happy to see him die? Independent. Retrived from https://www.independent.co.uk/news/the-riddle-of-aldo-moro-was-italy-s-establishment-happy-to-see-him-die-1149073.html
Ilikuwa ni Mei 9, 1978, majira ya mchana wa saa saba katika mji wa historia ya kale, wa Rome. Ambapo polisi walinasa mawasiliano muhimu ya simu kwa wakati huo, kwa Italia. Mtu asiyejulikana alipiga simu kwa mmoja kati ya wasaidizi wa Waziri Mkuu mstaafu aliyekuwa matekani, na ikiwa ni siku 54 zikiwa zimepita. Mpigaji alisema: "katika barabara ya Caetani kuna gari jekundu lina mwili wa Moro", kisha alikata simu. Kutoka makao makuu ya Polisi Rome, maafisa wake, haraka walikimbia kuelekea eneo tajwa. Walilikuta gari hilo aina ya Renault-4 likiwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara ya Michalangelo Caetani, katikati ya mji wa Rome. Eneo ambapo gari hilo lilitelekezwa, ilikuwa jirani sana na makao makuu ya vyama viwili katika mji huo - umbali wa yadi 300 kutoka makao makuu ya chama cha Waziri Mkuu aliyetekwa, cha Christian Democratic Party, au kwa kiitaliano "Democrazia Cristina (DC)", na yapata yadi 200 hadi makao makuu ya chama pinzani, na yaliyokuwa na ulinzi mkali masaa 24/7, ya chama cha Italian Communist Party, au "Partito Comunista Italiana(PCI)".Polisi walifika eneo hilo na kuweka utepe wa rangi nyeupe na bluu kuzuia shughuli yoyote katika kiunga hicho lilipotelekezwa gari hilo, huku wakichukua tahadhari zote kulifungua. Askari wa idara ya zima moto wa jiji hilo walifungua kwa uangalifu mkubwa gari hilo na kukata mfumo wa umeme wa gari hilo kwa kukata nyaya baada ya kipande fulani cha bodi.Ni kwanini hasa walichukua tahadhari kulifungua gari hilo? Hofu ya mabomu ya kutegwa. Hofu ya mabomu ya kutegwa ilikuwa kuu kwa Italia kipindi hicho wakati nchi hiyo imekaa tenge kiusalama. Usalama uliodhoroteshwa na mvutano mkubwa wa kitabaka katika nyakati hizo za vita baridi - kwa mamaandamano, migomo na vurugu za mara kwa mara katika zilizozalisha makundi yenye misimamo mikali ya itikadi za kisiasa, na yale ya siri kama P2 Masonic Lodge, sanjari na sekeseke la mtandao wa Mafia. Makundi haya, yote kwa mara mojamoja yalitumia mabomu ya kutegwa yakiwalenga wapinzani wao na watumishi wa serikali, hasa askari na majaji. Basi polisi walipofanikiwa kulifungua, ni kweli, ndani yake katika buti kulilazwa mwili uliotokwa pumzi, wa Aldo Moro, waziri mkuu mstaafu wa Italia, ukiwa umevishwa suti nadhifu ya rangi ya bluu iliyokoza, shati la mikono mifupi na tai nyeusi, na kwa juu koti kubwa na refu. Ni kwamba, suti hiyo ni ile aliyovaa asubuhi ya tarehe 16 Machi ya mwaka huo - siku 54 nyuma aliyotekwa akiwa njiani kwenda Bungeni.Ndani ya gari hilo, mwili wake ukilazwa Katika buti, kichwa chake kilifunikwa kwa blanketi. Na pembeni yake kulikuwa na mfuko wa plastiki ukiwa na vifaa vyake vidogo - saa, wembe, na vinginevyo. Alilala juu ya dimbwi la damu zilizoanza kukauka, lakini zikinuka ubichi. Damu zilizotoka katika matundu kumi ya risasi kifuani mwake. Kwa taarifa ya polisi, ilionesha aliuawa kwa kupigwa risasi jana yake. Taarifa za polisi zinaonesha alipigwa risasi kabla ya kuvalishwa koti hilo refu na kupakiwa garini, kwa kuwa koti hilo halikutobolewa na hata tundu moja la risasi. Zaidi, ilihisiwa huenda alipigwa risasi mazingira ya fukwe katika mji huo na kisha mwili wake kuburuzwa kabla ya kupakiwa garini, kwa kuwa katika pindo za miguu ya suruali yake kulikutwa mchanga mwingi wa fukwe.Haraka sana, hata nusu saa haikuisha, habari za kupatikana kwa Moro zilisambazwa kama upepo na redio za ijiji la Rome, na Italia yote, lakini sasa akiwa marehemu. Mshtuko na simanzi juu ya mauaji yake viliighubika nchi hiyo. Wafuasi wa chama cha Moro, cha DC walielekea makao makuu ya chama hicho mjini humo huku wakilia na kulaani vikali kundi lenye misimamo mikali ya kisiasa la mrengo wa kushoto-mbali, la Red Brigade ambalo ndilo lililohisiwa, kabla ya siku mbili mbele lenyewe kukiri kumteka, na baadaye siku 54 mbelele kutekeleza mauaji yake baada ya serikali kushindwa kufuata masharti ya kundi hilo kumuokoa kiongozi huyo mkuu wa chama cha DC na Waziri Mkuu mstaafu wa nchi.Wakati wafuasi wa chama cha DC wakijaa katika makao makuu ya chama hicho, umbali mfupi, makao makuu ya chama cha PCI hapakuwepo watu, bali walinzi wa chama hicho waliofurika mara dufu wakiwa katika mavazi ya kiraia huku bendera ikipepea nusu mlingoti. Hueda walijianda kukabiliana na hamaki za vurugu za makundi ya mrengo wa kulia-mbali kulipa kisasi kwa kuharibu mali za ofisi hiyo kwa kuwa kundi hilo limechipua mabawani mwa chama hicho cha kikomunisti? Haifahamiki. Lakini si ofisi hizo tu za vyama ambazo bendera ilipepea nusu mlingoti, bali majengo yote ya serikali na ofisi za vyama vyote vya siasa, nchi nzima.Hadi kufikia majira ya saa tisa na robo, mwili wa Moro ulitolewa garini. Kiongozi wa kanisa Katoliki jirani na eneo hilo, aliubariki kwa kuunyunyizia maji matakatifu kabla ya kupakiwa katika 'ambyulensi' nyekundu ya jeshi la zima moto, na kisha kuondoka kwa kasi eneo hilo huku nyuma msafara wa polisi ukifuata. Mwili wa Moro ulihifadhiwa katika taasisi ya sheria ya madawa ya Chuo kikuu cha Rome kabla ya maziko.Moro alitekwa asubuhi ya saa tatu ya tarehe 16 Machi, kabla ya mauaji yake siku 54 mbele. Alitekwa siku muhimu akielekea Bungeni katika kikao kilichokuwa kinakwenda kupiga kura ya imani kwa baraza la mawaziri la serikali ya Waziri Mkuu Giulio Andreotti. Lakini jambo muhimu zaidi na la kihistoria lilikuwa linakwenda kutokea Bungeni siku hiyo, ni kwa chama cha PCI si tu kwenda kupiga kura ya kuiunga serikali kwa mara ya kwanza katika historia, pia kuingizwa rasmi katika serikali ya ushirikiano na chama tawala cha DC. Suala la maridhiano na ushirikiano wa vyama vya DC na PCI katika serikali ya kitaifa, na uliobatizwa jina la "Historical Compromise", ni jambo lililopiganiwa sana na Moro akishirikiana na katibu mkuu wa chama cha PCI, Enrico Berlinguer. Hivyo Moro akielekea Bungeni siku hiyo ya utekaji wake, bila shaka alikuwa mwingi wa imani kuwa suala alilolipigania linakwenda kutimia siku hiyo. Hakika hakujua madhila yanayokwenda kumpata mbele kutokana na suala hilo.Kwa suala hilo, tayari Moro alijitengenezea hatari ya maisha yake, na wala si Berlinguer. Kwanini? Kwakuwa yeye, akiwa kama Rais wa chama cha DC, Waziri Mkuu mstaafu, na mtu mwenye ushawishi chamani na nchini, ndiye aliyekuwa daraja la makubaliano kati ya DC na PCI kushirikiana kiserikali. Na wale wasiopenda ushirikiano huu walinuia kuinusuru Italia kuelekea mrengo wa kushoto endapo mawaziri wa PCI wakiingia serikalini na huenda baadaye chama hicho kushika serikali. Na ili kuzuia ushirikiano huu kutokea, basi ni kumuondoa Moro aliyeonwa adui namba moja. Ili kuona hatari ambayo Moro alikuwa anajitengenezea juu ya maisha yake, yapasa kutazama jinsi ushirikiano huu ulivyochukuliwa kwa mtazamo wa kiusalama, wa NATO na namna ulivyoonwa na nchi za Magharibi katika kuvuruga mpangilio na uwiano wa nguvu za kisiasa kwa Ulaya, na kati ya Washington na Moscow.Kwanza kabla ya kugusia mtazamo hasi wa Magharibi juu ya hiki walichokiita "historiacal compromise" ya vyama hivi viwili, Uingereza walikuwa wamefikiria mapema mpango wa siri wa kufadhili mapinduzi ambayo yangeweza kukiondoa kabisa katika siasa chama cha PCI na makundi yake ya mrengo wa kushoto. Na hii si kwasababu ya "historical compromise", bali imani ya wapiga kura kwa PCI kupaa siku hadi siku. Hii ni mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1976 ambao ulileta picha tofauti ya chama cha PCI kuonekana kuanza kuaminika na wapiga kura na umaarufu wake kupaa. Katika uchaguzi huo, ilishudiwa kwa chama cha PCI kufanya vizuri kabisa katika historia za chaguzi nchini humo kwa kuongeza asilimia kufika 34.4 kutoka 33.8 za uchaguzi uliopita, na huku chama cha DC, kwa jambo lisilo la kawaida, kilianza kuporomoka kwa asilimia kwa kupoteza imani kwa wapiga kura baada ya rushwa na uchafu mwingine kukimeza chama hicho.Kupaa na kukubalika kwa PCI na wapiga kura, ilikuwa kengele ya hatari kwa nchi za Magharibi. Na hasa walihofu kwa DC kuanza kupoteza mvuto na kutengeneza mazingira ya kuangushwa mbeleni kwa sanduku la kura. Uingereza iliona kama kushinda kwa PCI katika chaguzi zijazo, basi ilikuwa ni kuipeleka nchi hiyo mrengo wa kushoto na kuwa chini ya Moscow na kuhatarisha usalama wa NATO. Hivyo, ili kuwazuia PCI, basi nikufadhili au kuunga mkono mapinduzi dhidi yake, kwao ilikuwa sahihi. Kama sivyo, basi kupenyeza majasusi watakao kivuruga chama hicho, au kufadhili makundi ya kigaidi ya mrengo wa kulia-mbali, kwa fedha, silaha na mbinu ili kuzuia vuguvugu la siasa za mrengo wa kushoto nchini humo.Mpango wa mapinduzi uliopangwa na Uingereza mwaka 1976 na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo dhidi ya wakomunisti, ulifichuliwa baadaye sana kwa kuchapishwa Januari 13, 2008 katika gazeti la Italia la "La Republica". Katika taarifa ya gazeti hilo, inadai wizara ya mambo ya nje ya Uingereza kipindi hicho ilijadili suala hilo la mapinduzi kwa usiri kuhofia siri kuvuja. Lakini baada ya kuchekecha mpango wao huo, waliona hatari ya mapinduzi inaweza kuamsha ari ya makundi ya mrengo wa kushoto kujibu mashambulizi kivita na hivyo kuipelekea nchi hiyo katika damu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kusababisha USSR kuingilia kati kijeshi na kuichukua nchi hiyo. Hivyo basi, mpango huo uliahirishwa.Ndiyo, achilia mbali mpango wa Uingereza wa mapinduzi Italia, basi turudi katika la usalama wa NATO kwa ushirikiano wa vyama hivi hasimu, na vikuu viwili katika serikali ya Italia, nchi mwanachama wa NATO, ndio ambao haukupokelewa kwa sura kunjufu kuliko hata kupaa kwa umaarufu kwa chama cha PCI. Si Washington tu, hata Moscow walioupokea vibaya ushirikiano huo katika nyakati hizo za fukuto la vita baridi. Kwamba chama cha DC cha mrengo wa kati na misingi ya kikatoliki, na kilichokuwa kinafadhiliwa na kuungwa mkono tangu mwaka 1947, na Marekani pamoja na washirika wake wa nchi za Magharibi chini ya umoja wao wa NATO - wa kujihami dhidi ya Umoja wa Kisovieti (USSR), eti kiunde serikali ya pamoja na chama cha kikomunisti cha PCI kilichokuwa kinafadhiliwa na Umoja wa Kisovieti(USSR) chini ya chama chao cha Comunist Party of the Sovieti Union(CPSU)? Licha ya kwamba ilikuwa ni kama kuchanganya mafuta na maji, lakini ushirikiano huo ulionwa kuwa hatari kwa usalama wa NATO, kwa endapo mawaziri wa PCI wakapatiwa nafasi serikalini itakuwa rahisi kwao kupata siri za kiusalama za NATO - za vituo vyake vya 'nyuklia' vilivyokuwepo nchini humo na mbinu za kivita, na kizivujisha kwa USSR - Moscow. Usalama wa kituo cha jeshi la majini cha Marekani cha "Sixth Fkeet Land Base" katika pwani ya Naples kingekuwa hatarini. Pia, ushirikiano huo ulionwa kuwa utakwenda kuvuruga uwiano wa nguvu za kisiasa kati ya Washington na Moscow kwa Italia yenyewe na Ulaya kwa kuvuruga makubaliano ya mkutano wa Yalta ya mwwka 1945.Achilia mbali mapokeo mabaya ya ushirikiano huo kutoka pande zote za Washington na Moscow, bali pia viongozi wa chama cha DC, kanisa katoliki, na makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kushoto-mbali na kulia-mbali, hawakuutaka, hasa kundi la Red Brigade waliouona ushirikiano huo haukai chungu kimoja, na ni ishara ya kumomonyolewa misimamo, imani na itikadi za chama hicho cha kikomunisti kwa kukituliza kusimamia misingi yake ya kupigania maslahi ya wafanyakazi, wanafunzi na makundi mengineyo katika nchi hiyo, kwa sababu kikiwa serikalini kitakuwa na tonge mdomoni, hivyo kuwa kimya.Lakini huenda kwa maono ya Moro na Berlinguer waliuona utengamano wa kiusalama wa Italia ni muhimu zaidi kwa ushirikiano wa vyama hivyo ili kutuliza mvutano wa kitabaka kuliko mtazamo wa Marekani,Uingereza na NATO juu ya jambo hilo. Kwa upande wake, Moro alikuwa na imani na ushirikiano huo kwa kuwa chama cha PCI kilianza kubadilika. Hasa mara baada ya chama hicho kuuanza kuacha taratibu misimamo yake mikali ya kikomunisti ya miaka ya 1940, 1950 na 1960, ya kuchochea mvutano wa kitabaka kwa madhumuni ya kushinda serikali, na sasa kuanza kuhubiri sana demokrasia. Na hili lilijidhihirisha kuelekea ushirikiano wa vyama hivyo wa "Historical Compromise", kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1970, PCI kilianza kujitenga taratibu na Moscow ili kutengeneza imani kwa Washington na NATO.Kilianza kujitenga na Moscow baada ya chama hicho na vile vingine vya kikomunisti kutoka nchi za Hispania na Ufaransa kuanzisha wimbi jipya la siasa za kikomunisti zilizoitwa "Eurocommunism" au "Neocommunism", zilizohamasisha demokrasia, misingi ya Magharibi, na ambazo hasa zilifaa kwa jamii ya watu wa Ulaya, tofauti na siasa za udikteta wa kikomunisti za Moscow. Na hata Washngton kwa nyakati tofauti, walianza kukifikiria chama hicho kuingia serikalini na miaka ya mbele kushika serikali, lakini bado hofu yao ilikuwa palepale, chama hicho kinaweza kuiepeleka nchi hiyo mrengo wa kushoto. Na ilikuwa aghalabu hisia za watu kuwatuhumu Washington na London kuingilia chaguzi za Italia kukisaidia chama cha DC kushinda na kutokutoka madarakani tangu mwaka 1947 zilikuwa kuu.Ndiyo, basi nchi hiyo ilikuwa tenge kiusalama hasa kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1960 hadi mwishoni mwa 1980 kwa mapambano mkubwa ya kitabaka. Kusema kweli Italia ndiyo nchi pekee kwa Ulaya iliyokumbwa na athari za vuguvugu la vita baridi kwa kushuhudiwa mapambano makali ya kitabaka ambayo hayakutokea kwa nchi yoyote barani humo. Na kipindi hiki cha mapambano ya kitabaka kwa nchi hiyo kilibatizwa jina la "The Years of Lead", kwa makundi ya kigaidi yenye misimamo mikali ya kisiasa kutumia fursa za mapambano haya, kwa kila moja kupandikiza vurugu ili kushinikiza serikali kuipeleka nchi upande wake kiitikadi. Ni kipindi kilichoshuhudiwa maandamano, migomo na vurugu za mara kwa mara zisizoisha miaka nenda rudi, ya wanafunzi waliotaka mabadiliko ya elimu, wafanyakazi wa viwandani waliotaka mazingira mazuri ya kazi na ongezeko la mishahara kufuatia mapinduzi ya viwanda, na asasi za kijamii. Kilikuwa ni kipindi cha sintofahamu ya kisiasa kwa nchi hiyo, na usalama wake ulikuwa shakani.Makundi ya wafanyakazi na vijana yenye misimamo mikali ya itikadi za kisiasa kama yale ya mrengo wa kushoto ya; "Autonomia Operaia", "Potere Operaia", na "Gruppi Communisti Rivoluzionari", sanjari na yale makundi ya kigaidi yenye misimamo mikali ya itikadi za kisiasa, kama lile la mrengo wa kushoto-mbali, la Red Brigade; na kulia-mbali, la kifashisti la Italian Social Movement(MSI), na yale makundi au magenge ya siri na yenye vinasaba vya mrengo wa kulia kama; P2 Masonic Lodge, Mafia, na makundi ya NATO yasiyojulikana yaliyoendesha oparesheni ya siri ya "Gladio operationi" ya kupinga kuenea kwa vuguvugu la siasa za mrengo wa kushoto Italia. Yote kwa pamoja, yalitumia fursa hii ya migomo na maandamano ya wanafunzi na wafanyakazi kwa kila moja kuvutia upande wake kiitikadi hasa kwa kudhohofisha misingi ya kidemokrasia kwa mashambulizi ya kiahalifu.Udhohofishwaji wa kidemokrasia uliochochewa na makundi haya ungelipelekea mazingira kama si ya nchi kupasuka katikati, au kupinduliwa na jeshi kama Chile, basi nchi kuelekea kuwa ya udikteta wa Kifashisti ya mrengo wa kulia-mbali na hivyo kuwa kama nyakati za Benito Mussolini (1919-1943).Mathalani, kwa mfano kundi la kigaidi la MSI la mrengo wa kulia-mbali, kwa madai ya kuwasaidia polisi, lakini ikiwa ni chuki dhidi ya mrengo wa kushoto, mara kwa mara lilitumia silaha za moto kuzima maandamano ya wafanyakazi na vijana kutoka makundi madogo madogo ya mrengo wa kushoto na kushoto-mbali, kama "Potire Operaia", "Lotta Continua", "Avanguardia Operai", "Gruppi Comunisti Rivoluzionari", "Partito di Unita' Proletaria", na "Autonomia Operaia". Pia lilifanya mashambulizi kulenga mihimili ya serikali kushinikiza nchi kuelekea mrengo wa kulia-mbali. Vivyo hivyo, kwa upande wa kundi la kigaidi la mrengo wa kushoto-mbali la Red Brigade, baada ya kudai chama cha PCI kimeshindwa kusimamia misingi yake kwa kujitenga na kusaliti wimbi la mabadiliko ya kuipeleka nchi mrengo wa kushoto, lilichukua jukumu la kutumia mashambulizi kufanikisha kile walichoshindwa PCI.Basi mtu wa kwanza kuiona hatari ya nchi hiyo kuvunjika vipande viwili kwa mvutano wa matabaka, ni katibu mkuu wa chama cha PCI, Enrico Berlinguer ambaye aliungwa mkono baadaye na Moro. Berlinguer alinasihi sana ushirikiano wa kivyama na makundi ya kijamii ili kuleta umoja na maelewano yanayoweza kuepusha makundi yasiyopenda demokrasia kuchochea zaidi vurugu kuifanya nchi hiyo kuangukia katika mikono ya kidikteta. Na kwa hali ilivyokuwa Italia, ni dhahiri Berlinguer aliiona hatari hii kunukia nchini humo hasa mara baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Chile, kwa serikali 'kisoshalisti' iliyochaguliwa kidemokrasia, ya Rais Salvador Allende, kupinduliwa mwaka 1973 na kundi la jeshi chini ya Augusto Pinochet, baada ya makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi kusababisha vurugu mara kwa mara kwa kutumia fursa ya mapambano ya kitabaka.Berlinguer, ambaye Machi 1972 alichaguliwa na mkutano mkuu wa chama chake cha PCI kuwa katibu mkuu, kwa mwaka uliofuata, Mei 1973, alianza kundaa mazingira ya ushirikiano kwa kuandika mfululizo wa machapisho ya insha katika gazeti la chama hicho, la "Rinascita", akinasihi ushirikiano wa kitaifa kwa ngazi ya makundi ya kijamii na kivyama, hasa vyama vitatu vikuu - DC, PCI, na kile cha kisoshalisti cha Italian Socialist Party, au "Partito Socialista Italiana (PSI)". Belinguer alinasihi katika moja ya insha yake "tunajua, na kwa jambo hili la Chile imejidhihirisha tena namna matendo yasiyo ya kidemokrasia yanavyoweza kumomonyoa misingi ya kijamii na taifa"(Ginsborg 1990, uk.355)Licha ya Belinguer kunasihi maridhiano, lakini alijua wazi chama chake cha PCI hata kingelishinda kwa zaidi ya asilimia 50 wakati huo, kisingelipewa serikali na chama cha DC kilichoungwa mkono na Marekani, lakini aliona mambo matatu kwa PCI kuingia katika serikali ya ushirikiano wa kitaifa na chama cha DC. Kwanza, taratibu kutatengeneza mazingira ya baadaye ya kuaminika kwa chama hicho kushika dola. Pili, kujiweka mbali taratibu na umoja wa Kisovieti kwa siasa zake za udikiteta wa kikomunisti. Tatu, kujisafisha katika macho ya jamii kwa kujiweka mbali na kundi la kigaidi lililomea mabawani mwa chama chake, la Red Brigade ambalo lililaumiwa na jamii kwa mauaji na utekaji likinuia kuipeleka nchi mrengo wa kushoto kwa mtutu baada ya chama cha PCI kushindwa kazi hiyo. Nne na kuu zaidi, alinasihi sana ushirikiano huu ili kuiepusha inchi hiyo kuvunjika vipande viwili au kutokea mapinduzi ya kijeshi kama yale ya Chile, na ambapo vyama vya mrengo wa kushoto vingalipotea zaidi kuliko kuinuka kama hali hiyo ya Chile ingalitokea.Na hatimaye ushirikiano huu kati ya DC na PCI ulianza rasmi nje ya serikali mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1976 ulioshuhudia chama cha PCI kufanya vizuri katika historia ya chaguzi za nchi hiyo hasa mara baada ya kupigiwa kura kwa wingi na; wafanyakazi na makundi ya vijana. Katika uchaguzi huu, vyama vikuu vitatu viligawana alilimia 82, na kuviachia vyama vingine vidogo vidogo asiliamia 18. Lakini hakuna hata kimoja kilichokuwa na uhalali wa kuunda serikali bila ya ushirikiano na chama au vyama vingine baada ya kila kimoja kukosa sifa kwa kutofikisha theluthi mbili ya kura kama ilivyotakiwa kikatiba. Katika vyama hivyo vitatu, chama cha DC kilipata asilimia 38 ya kura, PCI kilipata asilimia 34, na PSI kilipata asilimia 10.Ieleweke kwamba, katika chaguzi zote, chama cha DC kimefanya mashirikiano na chama cha kisoshalisti cha PSI sanjari na vyama vingine tofauti na PCI. Lakini katika uchaguzi huu, chama cha PSI kilijitoa kushirikiana na DC baada ya kuona kura zake zinaporomoka kila chaguzi. Na sasa katika uchaguzi huu vyama vya mrengo wa kushoto, vyaPSI na PCI viliungana na hivyo kufanya idadi ya kura zao kufikia asilimia 48. Chama cha DC hata kingeungana na vyama vingine vilivyojikusanyia asilimia 12, bado kisingeweza kufikia theluthi mbili ya kura, hivyo kililazimika kuungana na vyama vya mrengo wa kushoto, na hapa ndipo DC kilipokihitaji chama cha PCI.Octoba 1976, mara baada ya uchaguzi mkuu, na ikiwa ni mara ya kwanza, chama cha PCI kiliunga mkono sera ya "Austerity Programme" ya serikali ya Waziri Mkuu Giulio Andreotti. PCI waliunga mkono sera hii wakiwa bado hawajaingizwa serikalini, walikuwa wanapalilia mazingira jambo hilo kutimia siku za usoni ili kufikia kilele ya kile walichokiita "historical compromise". Sera ya "Austerity Programme" iliyokuwa inawakandamiza wafanyakazi, ililenga kupambana na mkwamo wa kiuchumi ulioikumba Italia kunzia mwanzoni mwa miaka ya 1970. Sera hiyo ilikusudia kuongeza gharama ya mafuta asilimia 25, gharama ya gesi asilimia 20, na gharama ya mbolea asilimia 15. Na baada ya wiki moja mbele, serikali ya Andreotti ilitangaza kuongeza gharama ya umeme, simu na posta, na haya yalifanyika bila kupandisha mishahara kwa miaka miwili. Hali hii ilipelekea migomo na maandamano ya wafanyakazi katika baadhi ya miji, na hapa ndipo chama cha DC kilipowategemea PCI kuwatuliza wafanyakazi kwa kuzungumza na viongozi wao, kwa kuwa ilikuwa rahisi kwa PCI kusikilizwa na wafanyakazi kuliko serikali.PCI waliendelea kupalilia mazingira ya kutafuata kuingia serikalini kwa kuonesha ushirikiano kwa serikali ya chama cha DC - ya Andreotti, kwa kuacha kupiga kura ya kuipinga serikali yake Bungeni kama ilivyokuwa mika ya nyuma. Si kwamba walipiga kura ya kuunga mkono, bali waliacha kabisa kupiga kura ya kupinga. Na hili la kutopiga kura ya kupinga, walilifanya kuanzia, baada ya uchaguzi mkuu mwaka 1796 hadi 1978 wakati ambao ilidhaniwa ndiyo haswa chama hicho kilikwenda kuingizwa serikalini, na ambapo kwa bahati mbaya mambo yaligeuka baada ya mauaji ya Moro kutokea akielekea Bungeni kwa aajili ya suala hili ya suala la kura ya imani seriakali, na hili la "historical compromise". Naam, basi asubuhi ya Machi 16 ya utekaji wa Moro, msafara wake ukiwa katika magari mawili, gari aina ya Fiat 130 ya bluu, ambayo alipanda Moro mwenyewe na askari wa wawili wa jeshi la "Carabinieri" - Dominico Ricci aliyekuwa dereva, na Oreste Leonardi aliyekuwa kiongozi wa walinzi wake. Nyuma gari hilo lilifuatia gari aina ya Alfa Romeo Alfetta iliyokuwa na polisi watatu - Francesco Zizzi, Giulio Rivera na Raffaele Iozzino.Msafara huu ulipokuwa unaingia barabara ya Via Fani karibu na uwanja wa michezo wa "Rome Olympic Satdium", ulizuiwa na magari madogo manne aina ya Fiat, nyuma na mbele na mbele, ya wapiganaji zaidi ya 10 wa kundi la Red Brigade waliokuwa na silaha nzito za moto mithili ya jeshi. Msafara wa magari mawili ya Moro yalishambuliwa kwa jumla ya risasi 91 zikitoka katika aina mbalimbali za bunduki, na 45 zikiondoa uhai wa walinzi wake watano bila yeye kuguswa na risasi hata moja! Kisha akachukuliwa mateka katika moja ya gari lao na kutokomea naye kusikojulikana. Ni tukio ambalo halikuzidi dakika tatu, na lilifanyika katika oparesheni kuu ya kijeshi ya askari wenye mafunzo ya hali ya juu - ya kufanya mauaji pasipo kumdhuru mtu waliyekusudia kumteka katikati ya mashambulizi ya 'mvua' za risasi!Baada ya tukio hili la mauaji na utekaji, siku mbili mbele, tarehe 18, kundi la Red Brigade lilikiri kuhusika na tukio hili. Utekaji wa Moro ulizua kelele kila pembe ya Italia za kuachiwa kwake zikiambatana na migomo kadhaa kutoka chama cha wafanyakazi. Serikali ilisambaza polisi na wanajeshi wapatao 4000 katika jiji la Rome kumsaka nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa, sanjari na helkopta za polisi zilizopita angani mara kwa mara.Tarehe 3 Aprili, polisi wakipita nyumba kwa nyumba, waliwakamata waliosemekana kuwa wanachama wa Red Brigade, na baadhi wanachama wa chama cha PCI. Lakini waliachiwa baada ya masaa 48 kwa amri ya mahakama kwa kutokuwa na uthibitisho.Juhudi zote za serikali ya Andreotti kujaza polisi na wanajeshi kila pembe ya Rome, kukamata wale inaowaita wanachama wa Red Brigade, kumtafuta Moro nyumba kwa nyumba, na helkopta za polisi kupasua anga, ilikuwa ni kazi bure, ama ama 'dananganya toto', hasa baada ya serikali kupuuza taarifa nyeti zilizotolewa na baadhi ya watu waliohisi kule alikofichwa, zaidi, kukataa kufanya mazungumzo na kundi hilo ili kunusuru maisha yake.Mnamo Machi 19 na Aprili 4, barua kutoka kwa Moro akiwa matekani kwenda kwa viongozi wa serikali ya Italia, kuomba kufanya mazungumzo na kundi hilo hazikutiliwa mkazo ama zilipuuzwa kwa sababu wanayoijua wao. Kwa mapuuza haya ya serikali, basi Moro alikutwa na hatia katika mahakama ya siri ya kundi hilo iliyoitwa "People's court" na kuhukumiwa kifo, na ikisubiriwa siku ya kutekeleza adhabu hiyo. Aprili 24, tena, ili kumuachia huru na kunusuru maisha ya yake, Red Brigade walidai wafungwa 13 wa muda mrefu waliokuwa gerezani mjini Turin, ambao ni wanachama wa kundi hilo na viongozi wao, waachiwe huru ili uhai wa Moro usalimike. Bado serikali ilikataa na kudai haiwezi kupiga magoti kwa kundi hilo, na kwamba nchi hiyo inaongozwa na sheria, na sheria za nchi tu, ndizo zitakazomuokoa Moro. Wazo hili la kutolipigia magoti kundi hilo, liliungwa mkono na viongozi wa chama cha PCI kikitafuta kujiweka mbali na kundi hilo ili kujisafisha katika macho ya jamii na nchi za Magharibi, na kupalilia zaidi njia ya kuingizwa serikalini.Bofya hapa kusoma sehemu ya pili ya hadithi hii
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi tofauti na kuongeza mishahara. Akijibu swali la Mbunge wa Konde kupitia chama cha ACT Wazalendo, Khatibu Said Haji aliyetaka kujujua ni lini serikali itaongeza mishahara kwa wafanyakazi nchini katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni Dodoma, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna njia nyingi za kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwemo kuwapandishamadaraja na kuwapunguzia kiwango cha kodi. Majaliwa ameongeza kuwa hakuna haja ya kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi hadharani kwani kunaongeza gharama za maisha na kusababisha vitu vingi kupanda bei bila sababu ya msingi."Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi katika maeneo mengine ambayo ni zaidi ya mishahara, na niwaombe wafanyakazi nchini wasikate tamaa kwa kusubiri watangaziwe hadharani," amesema Majaliwa.
Ripoti mpya iliyotolewa Jumatano na kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) imedai kuwa "kuvaa barakoa mbili" sambamba na kuvaa barakoa inayokutosha inaweza kupunguza makali ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.Watafiti wamegundua kuwa kuvaa barakoa ya kitabibu huku ikifunikwa na barakoa ya kitambaa inaweza kupunguza asilimia 92.5 ya chembechembe za virusi vitakavyoingia mwilini.Ingawa bado CDC haijapendekeza rasmi kuvaa barakoa mbili, Mkurugezi wa kituo hicho, Dk Rochelle Walensky alizungumza jumatano ya tarehe 10 februari akidai kuwa watatoa muongozo mpya wa namna ya uboreshaji wa barakoa ili ziweze funika vizuri pindi zinapovaliwa. "barakoa inaweza kuwa na changamoto," Mkurugenzi Rochelle Walensky alisema katika mkutano uliofanyika White House akielezea mwenendo wa virusi vya corona. "Sayansi iko wazi. Kila mtu anahitaji kuvaa barakoa anapokuwa kwenye umati wa watu au anapokuwa nyumbani kwake au akiwa na watu ambao sio sehemu ya familia yake."Utafiti huu wa CDC ulifanya ulinganifu kati ya mtu ambaye hajavaa barakoa, mtu aliyevaa barakoa ya kitambaa yule aliyevaa barakoa ya kitabibu na mwingine akavaa zote mbili; barakoa ya kitabibu ikifuatiwa na barakoa ya kitambaa ambapo Utafiti huo uligundua wakati watu wanavaa barakoa ya kitabibu iliyofunikwa vizuri iliyofunikwa vizuri na barakoa ya kitambaa wanaweza kupunguza makali ya kusambaa kwa virusi vya corona. Kituo cha kudhibiti magonjwa, Marekani kilipendekeza watu waanze kuvaa barakoa za vitambaa tangu mnamo Aprili 2020, mwezi mmoja baada ya Marekani kushambuliwa vikali na janga la corona.
Jurgen Klopp amempoteza mama yake mzazi Elisabeth Klopp ambaye amefariki akiwa na miaka 81 na kuzikwa siku ya Jumanne Februari 9 nchini Ujerumani. Klopp ameshindwa kushiriki maziko ya mama yake kwa sababu Ujerumani wamezuia wasafiri wote kutoka Uingereza kuingia Ujerumani kutokana na mlipuko wa aina mpya ya kirusi cha corona nchini Uingereza. Meneja huyo wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza ameomboleza kifo cha mama yake kwa kusema kwamba mama yake alikuwa mtu wa pekee sana katika maisha yake. Hata hivyo, Klopp ameviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kwamba hali ya mlipuko wa Covid-19 itakapotengemaa atafanya sherehe ya kuenzi maisha ya mama yake. Awali mwezi huu Klabu ya Liverpool ilinyimwa ruhusa ya kuingia Ujerumani kucheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya 16 bora katika michuano ya klabu bingwa Ulaya (UEFA) kutokana na zuio la wasafiri kutoka nchi zenye aina mpya ya virusi vya corona. Mchezo wa Liverpool na RB Leipzig hautachezwa Ujerumani na badala yake utachezwa Februari 16 katika uwanja wa Puskas jijini Budapest nchini Hungary.
Kampuni ya Twitter imepuuza agizo la Waziri Mkuu wa India Narendra Modi la kuzifungia akaunti za Twitter ambazo anadai zinachochea maandamano ya Wakulima wanaolalamikia Sheria kuwakandamiza na kuwapa faida Wafanyabiashara.Serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi ilitaka twitter iondoe akaunti zipatazo 1,100 na machapisho yanayosambaa mtandaoni yanayodai uongozi unawanyonya wakulima na kuongeza kuwa baadhi ya akaunti zinafadhiliwa na maadui zake kutoka Pakistan.Licha ya kuwa hapo awali Mtandao huo wa kijamii uliondoa baadhi ya akaunti mapema wiki iliyopita, Twitter imesema inaamini agizo hilo linakiuka Sheria za India za Watu kuwa na uhuru wa kutoa maoni hivyo hawatozifungia.Akielezea uamuzi wake katika chapisho la blogi, Mtandao wa twitter umeweka wazi kuwa uamuzi wake ni kwa lengo la "ni kutunza misingi na kutetea uhuru wa kujieleza".Twitter imeripotiwa kuzifungia account zinazozidi 500 lakini ikaziacha zile za Wanaharakati, Waandishi na za Wanasiasa.Wakulima nchini India wamekuwa wakiandamana nje ya mji mkuu, New Delhi, kutaka mageuzi ya kilimo tangu Novemba 26, licha ya kukumbana na vizuizi vya polisi.Polisi wamesema maafisa 300 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa maandamano hayo huku mamia ya waandamanaji wakiripotiwa kujeruhiwa na kifo cha mkulima mwenye umri wa miaka 26 ambaye trekta lake lilipinduka baada ya kugonga kizuizi cha polisi.Serikali imeamua kuzima mtandao katika maeneo ya nchi hiyo ikiwa ni juhudi za kuzuia maandamano, hatua inayotumiwa mara kwa mara kuzuia wapinzani.
Tamko la kuahirishwa kwa bunge la Ghana limekuja kufuatia ongezeko la maambukizi kati ya wabunge na wafanyakazi na linataraijia kurejea tena baada ya wiki tatu.Spika Alban Bagbin aliliambia bunge siku ya Jumanne ya tarehe 17 kuwa wabunge 275 na wafanyakazi 151 kati ya 500 walipata virusi vya corona.Spika pia aliwataka wabunge wengine na wafanyikazi wa bunge kupima corona ikiwa bado hawajafanya hivyo.Bagbin alisema uamuzi wa kusimamisha shughuli ulifanywa baada ya kuzungumza na uongozi wa bunge.Alisema kamati ya uteuzi wa bunge itaendelea kukutana na wateule wa nyadhifa za wizara katika utawala wa Rais Nana Akufo-Addo, ambaye alichaguliwa tena mnamo Desemba. Ghana imekwisharekodi zaidi ya kesi 72,300 za maambukizi ya corona na vifo 472, kulingana na takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.
Robert Pershing Wadlow ni nani?Wadlow alizaliwa mnamo Februari 22, 1918 huko Alton, Illinois akiwa na uzito wa kilogram 4, mwenye afya tele na furaha akionekana kama watoto wengine. Akiwa na umri wa mwaka mmoja Robert Wadlow alianza kukua kawaida lakini tofauti na watoto wengi, alikua haraka sana na alipofikisha umri wa miezi 6, tayari alikuwa na uzito wa kilo 13 (wastani wa kawaida kwa mtoto wa kiume huwa ni nusu yake) huku akiwa na kilo 20 urefu wa futi 3 pindi alipotimiza mwaka mmoja.Wakati Wadlow akiwa na umri wa miaka 5, alikuwa na urefu wa futi 5, inchi 4 akivaa nguo ambazo za rika la vijana. Chakushangaza pindi Wodlow alipotimiza miaka 8, alikuwa tayari mrefu kuliko baba yake (akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 11).Robert Wadlow akiwa amesimama na familia yake Alipotimiza umri wa miaka 13, alikua Skauti Mrefu zaidi ulimwenguni kwa futi 7, cm 4 akivaa sare maalum kwani vipimo vya nguo vya kawaida visingefaa.Nini kilipelekea awe na Urefu Kupita Kiasi?Hapo baadae akiwa na umri wa miaka 12 madaktari waligundua kuwa Wadlow alikuwa na hali ambayo kitaalamu ilifahamika kama hyperplasia iliyosababisha ukuaji wa haraka na wa kupindukia kwa sababu ya kiwango cha juu cha homoni za ukuaji mwilini. Inasemekana kama Wadlow angezaliwa leo, labda asingekuwa mrefu kiasi hicho kwani sasa kuna upasuaji wa kisasa na dawa ambazo zinaweza kukomesha ukuaji usio na udhibiti bahati mbaya wakati huo madaktari waliogopa kumfanyia upasuaji kwakuwa Imani ya kuweza kumsaidia ilikuwa ni ndogo.Wadlow aliachwa aendelee kukua lakini licha ya kimo chake kuongezeka, wazazi wake walijaribu kufanya maisha yake kuwa ya kawaida kadri walivyoweza.Shule zilimtengenezea madawati maalum, zikiongeza nafasi chini ili asikae kwa tabu darasani. Na kwa kuwa Wadlow alikuwa mkubwa zaidi akifuatiwa na wadogo zake (ambao wote walikuwa na urefu wa wastani na uzani), alitarajiwa kucheza na ndugu zake lakini haikuwa hivyo kwani wadlow alipendelea zaidi kazi ya kupiga picha.Ingawa alikuwa mzima kiafya katika miaka yake ya ujana, baadae alianza kukumbana na matatizo kiafya yaliyosababishwa na urefu uliokithiri, miguu yake ilianza kufa ganzi suala lililopelekea kutoona malengelenge au maambukizo. Mwishowe, pia alihitaji magongo ya kuvaa miguuni yakifahamika kama (braces) na fimbo ili vimsaidie kutembea.Mnamo 1936, kundi linalojulikana kama Ringling Brothers lilimuona Wadlow na kupendekeza wazunguke nae katika matamasha yao hasa wakati pindi watoto wadogo wakiwa wanafanyamatamasha yao. Kwa furaha yao Wodlow alikubali kufanya nao ziara.Robert Wadlow akilinganisha ukubwa wa viatu na mtoto wa kundi la Ringling BrothersWodlow alikuwa na uwezo wa kuvutia umati mkubwa kila mahali alipokanyaga wakati wa maonesho hayo ya “Circus”. Haikupita mda mrefu Wodlow akawa mtu mashuhuri kama siyo shujaa wa mji wa Alton.Ingawa maisha ya mtu mrefu zaidi duniani yalikuwa ya kufurahisha, lakini pia yalikuwa magumu sana. Katika Nyumba, sehemu za umma, na vitu vya nyumbani hakukuwa na vitu maalum kwa ajili yake hivyo ilibidi afanye makubaliano na marekebisho ili apate mbadala.Wodlow alikuwa akivaa magongo miguuni (braces) ili aweze kutembea vizuri cha kusikitisha magongo hayohayo ndiyo yaliyopelekea anguko lake. Ilikuaje?Kutokana na ganzi katika miguu yake, Wadlow alishindwa kugundua shida katika mguu yake ambaye ilitokana na magongo aliyokuwa akivaa miguuni ambayo yalimkandamiza na kumchubua kifundo cha mguu mnamo mwaka 1940.Wakati Wadlow alikuwa akionekana katika Tamasha la Michigan’s Manistee National Forest Festival, hakugundua kuwa alikuwa na malengelenge kwenye mguu ambayo yalimsababishia homa kali. Wodlow alikimbizwa hospitali ambako alifanyiwa upasuasi wa dharula na kuongezewa hela.Jambo la kusikitisha madaktari walishindwa kuokoa maisha ya Wadlow. Maneno yake ya mwisho yakiwa, "Daktari anasema sitarudi nyumbani kwenye ... sherehe," akimaanisha sherehe ya kumbukumbu ya ndoa ya bibi na babu yake.Ingawa alifikwa na umauti akiwa na umri mdogo, Robert Wadlow aliacha urithi mkubwa. Tangu 1985, sanamu ya shaba ya Wadlow imesimama kwa kujigamba huko Alton, kwenye maeneo ya “University School of Dental Medicine” na katika Jumba la kumbukumbu ya Historia na Sanaa ya Alton. Wageni huweza kuona picha za Wadlow pamoja na jozi chache za viatu vyake, dawati lake la shule, kofia yake ya kuhitimu na joho.Sanamu la Robert Wadlow likiwa limesimama katika makazi alimukuwa akiishi Alton, Illinois.Kwa sasa sanamu zingine za Wadlow zimewekwa katika Jumba la kumbukumbu la ‘Guinness World Records’. Kumbukumbu hizo mara nyingi hujumuisha fimbo kubwa ya kupimia, kwa hivyo wageni wanaweza kushangaa jinsi Wadlow mrefu alivyosimama na kuweza kujilinganisha nae.Hata hivyo ni mabaki machache tu yaliyobaki kama ukumbusho wa Wadlow kwani muda mfupi baada ya kifo chake, mama yake aliharibu takribani vitu vyote vilivyowahi milikiwa na marehemu ili kulinda heshima yake na kuepusha watu wenye tamaa ya kutaka kupata faida kutokana na hali ya mwanae. Jambo zuri ni kuwa hadithi yake ya kusisimua inabaki, picha zake nzuri zimebaki vile vile. Mpaka sasa hakuna mtu aliyewahi kufikia urefu wa Wadlow na wakati huu, inaonekana hakuna uwezekano kwa mtu kuja kuvunja rekodi hiyo.